Mara nyingi ilizoeleka kusoma kwenye social media au sehemu mbalimbali kuona au kusikia mabasi ya umma alimaarufu hapa nchini kama daladala ya huko majuu au kwa wakoloni yakiwa na huduma ya intaneti ya bure (free Wi-Fi)
Wakati huo ukitafakari hilo hapa nchini tukiwa na mradi namba moja barani Africa wa mabasi ya umma ya mwendo kasi, bado huduma hiyo haikuweza kuongezwa kwa wapandaji wa mabasi hayo, ikiwa bado tunasoma na kusikia ni huko kwa mkoloni (ulaya) tu ndo unaweza kukuta huduma hiyo.
Ajabu leo kama siyo jana na juzi nilijaribu kupanda daladala kutokea tegeta kuja posta nikakutana na tangazo kwenye kioo free Wi-Fi!!, nilimuuliza konda akanipa jibu huduma ipo kazi kwako kama charge ya simu yako iko fully anza kuchart!!.
Aseee, niliona ni mfano mzuri na hatua nzuri kwa daladala za route hii ndefu kuweka huduma hiyo, ukizingatia usasa wa teknolojia ya sasa.
BIGup sana mmiki wa T 919 DFR Tegeta -Kivukoni.