Alafu inawezekana ubungo kwenda kariakoo ilikuwa mbali sana wakati huo naona na barabara ilikuwa ya moramu.Kweli mlifaidi sana enzi hizo so natural,chai ya maziwa ikiwa inatoka kwenye mabomba UDSM na Nyama za makopo za Tanganyika Perkers.
Kipindi hicho hata trafic police kumuona barabarani ilikuwa ni bahati mbaya. Taxi peugeot 304 milango yake ilifunguka kutokea mbele kuelekea nyuma na hakukuwa na dereva kijana.