Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Mama mmoja baada ya purukushani na kukurukakara nyingi,alifanikiwa kuingia ndani ya DSM la ubungo-g/mboto.Mama alipoingia ndani ya daladala alidaka chuma la juu kuji-support bila hata kuangaza macho kama kuna siti iliyo wazi.Mara kijana mmoja akamgusa bega na kumwonyesha siti iliyo wazi.Mara baada ya kukaa,yule mama akaanza kulia.Alipohojiwa kwanini analia,akajibu,"huwezi kuamini mwanangu,huu mwaka wa tatu toka nihamie gongo la mboto,sijawahi kupata siti kwenye daladala ninaporudi nyumbani,yaani hata siamini kama nimepata siti".