Jana nimeingia DSM kutoka kijijini kwetu Masasi na kufika Ubungo Stendi saa moja na nusu usiku. Nilichokikuta pale ni aibu, hakuna utaratibu kabisa kwenye kuingia na kupaki mabasi na magari madogo yanayokuja kuchukua abiria pale.
Pili nilifadhaishwa na jinsi ambavyo hawa watoa huduma hapa wamekazania kukusanya pesa kwanza kibabe na kwa maringo pasipo kujali uhuru na haki za watu wengine.
Nini kinaendelea hapa, mimi nilifikiri baada ya kurudi kwenye mikono ya serikali ya Jiji miundombinu na huduma nyingine zingeboreshwa lakini naona hakuna jipya zaidi ya kukomaa kwenye kukusanya ushuru kwa vita na mbwembwe