Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,030
- 59,684
Hii stendi ni chafu mno.
Haijakaa kimpangilio. Ukiwa unamsindikiza mtu kuna ada unayotakiwa kulipa (shilingi 200 kama sikosei). Lakini cha ajabu kwenye lango la kuingilia hakuna ubao unaosema wasindikizaji wanatakiwa kulipia.
Kama upo ama wameuweka siku za karibuni au haupo sehemu unapoweza kuonekana kiurahisi. Kwa ujumla kila kitu kimekaa shaghalabaghala tu hapo.
Halafu pananuka kichizi.
Nikitilia maani uwiano wa idadi ya watu wanaopita hapo kwa nikilinganisha na sehemu nyingine; mbona hapo pana uafadhali!!
Mara ya mwisho nimecheck kama wiki tatu hivi, vyoo vilikuwa na maji na viko katika kiwango cha kutumika kwa mtu aliyebanwa!!! Kumbuka kuna pahala penye mikusanyiko nimefika, yaani hata kama haja imekubana, unconsciously unajikuta umepata ahueni baada ya kuona mazingira yenye kinyaa chakupindukia pahala pa kujisaidia.
Wizi wa vitu pia umepungua, maana hawaruhusu tena wapokeaji kuingia ndani ya uzio kiurahisi kama ilivyokuwa mwanzo. Mabasi pia yanaondoka on time kuanza safari zake.
Uchafu kama unavyoonekana hapo kwenye picha ni matokeo ya hulka za wengi wetu. Ndivyo tulivyo; haswa Dar na 'umjini-umjini' kama sifa'!!! Inaudhi sana na ni kero kubwa.
Jiji lote la Dar ni dampo ya uchafu. Mie sioni hata sehemu yenye afadhali. 2010 Dar ilikuwa jiji la 7 kwa uchafu duniani na ya tatu kwa uchafu Afrika sidhani kama kuna ahueni yoyote iliyotokea 2011. Wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele.
Wala hujakosea mkuu. Mwaka jana niilipokua Dar desemba nilishangaa hata nikawa najuta kuwasili Bongo mchana kweupeee!!
Mchizi nilikua niko juu ya daladala trying to get the home feeling na amini usiamini kulikua na jamaa kasimama barabarani akikojoa mtaroni laivu!!!...Mwenzio mbona nikamaka kwa mshangao na abiria alikyekua amekaa ubavu wa pili akaniuliza "hivi wewe ni mgeni hapa mjini." namii nikawmambia ndivyo na ndo nimelandi kutoka Marekani. Jamaa akacheka kisha akanijibu "karibu nyumbani, utazoea tu". Nilishangaa na nikakataa kauli yake eti "nitazoea'....there is no way in hell nitaozea kumwona mtu mzima hoyvoo, dudu nje akimwaga jojo kadamnazi mitaa ya Sinza.
Kisha kuanzia mitaa ya Mikocheni hadi Kawe ndo hapafai kabisa maana ni arufu mtindo mmoja!!! Maji taka hayazolewi na hata wakifanya kuzoa ni upuzi mtupu. Jamaa wanatoa uchafu ndani ya mtaro na kuuweka right at the top. In simple common sense, when it rains wont all this trash go right back into the drains jamani!!!? Nilipohoji nikaambiwa jama wanafanya hivyo maksudi ndo waweza kuhifadhi kibarua for the next day...Gaaadem!...Yaani Bongo kivyakevyake aisee. Kisha maeneo yenyewe nd'o barabara inayopitiwa na matasha na nikahooji tena kwani hawaoni hali ilivyo hususan kukinyesha. Nikaambiwa ukilinganisha na swala la kwamba jamaa wanaendesha mashangingi fuli-kipupwe, kwani wanaipata hio harufu?...najua ushapata jibu hapo!
Kisha ukiingia mjini wakati mambo ya umeme yanaleta kasheshe utajuta!...Kelele ya majenereta ni kama kuzimu! Yaani waliohujumu wananchi wa Tanzania kwa skendo za ishu za umeme hawakuwatenedea wananchi haki...but then again, who cares.
Kisha hapo Ubungo nitawaachia wenyewe wajadli. Kama Nyani alivyosema hapo juu watu wanaosindikiza abiria wanatozwa hela lakini
hujui hela inaenda wapi au ni ya nini. There is no official communication for that matter. Kisha kila mtu ni mwizi/tapeli hususan kipindi cha krismasi na shamrashamra za New Year. Utauziwa tikiti na jamaa kisha mkishamalizana na umekaa kwenye nafasi yako, anatokea konda mwengine anakudai hela zaidi. Ukijaribu kumtafuta aliyekukapa tikiti humuoni. Mwenzenu niligoma kushuka basi la Tanga kwa upuzi huo. Jamaa ilibidi nimmwagie kimombo na kumsuta mbaya sana. Tatizo langu lilkua usumbufu tu wa hawa matapeli. At the end of the whole saga tukawa washkaji mpaka kubadili namba za simu na niikapata kupiga tripu zengine mbili na jamaa hadi Mombasa na kurudi Dar.
Bongo tambarare wakuu...akili mukichwa!
Ivuga, katika vitu ambavyo sisi watanzania wengi hatupendi kuambiwa ni ukweli kuusu mitazamo yetu hasi ya maisha.
Tu wabishi sana, imani potofu pasipo kufikiri, uchafu uliokithiri, kutokuwajibika, tabia za kuombaomba kila kukicha.
Hatutaendelea kamwe, labda tutawaliwe tena.
Serikali ya Halmashauri ya jiji kweli hapo nyumbani ipo?Uchafu mijini namna hii Ahhh jamani nchi yetu haina viongozi.
So, what did the photographer do? Au ndio hivi kakupa uje kutwambia? And what are YOU planing to do?
sasa kwa nini hawataki kuuondoa?kodi wanapeleka wapi jamani.Nikitilia maani uwiano wa idadi ya watu wanaopita hapo kwa nikilinganisha na sehemu nyingine; mbona hapo pana uafadhali!!
Mara ya mwisho nimecheck kama wiki tatu hivi, vyoo vilikuwa na maji na viko katika kiwango cha kutumika kwa mtu aliyebanwa!!! Kumbuka kuna pahala penye mikusanyiko nimefika, yaani hata kama haja imekubana, unconsciously unajikuta umepata ahueni baada ya kuona mazingira yenye kinyaa chakupindukia pahala pa kujisaidia.
Wizi wa vitu pia umepungua, maana hawaruhusu tena wapokeaji kuingia ndani ya uzio kiurahisi kama ilivyokuwa mwanzo. Mabasi pia yanaondoka on time kuanza safari zake.
Uchafu kama unavyoonekana hapo kwenye picha ni matokeo ya hulka za wengi wetu. Ndivyo tulivyo; haswa Dar na 'umjini-umjini' kama sifa'!!! Inaudhi sana na ni kero kubwa.
Then YOU do something. Sijasema ukuzoe ule uchafu but try to use your right as a citizen to exercise some agency...oo i even dont know what to say...our country is just amazing ...may be we love kipindupindu...and i dont understand our journalists. these guys are using this bus terminal everyday but you cant hear em saying anything.
umenikumbusha huo utaratibu upo hadi leo kwani? mana loh! ulikua unaniboa kinoma yaniHii stendi ni chafu mno.