Ubunge wa darasa la 7 na form 4 mwisho 2020

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Habari wana Jf,

Naanza kwa kusema ni kweli katiba imeruhusu sifa ya Muwakilishi wa wananchi ajue kusoma na kuandika tu na sio degree lakini;
Matatizo ya wabunge ambao hawakupata elimu ya juu katika kujenga hoja na kutoa michango bungeni tumeyaona,wengi wamekuwa wakirusha vijembe na kusema maisha binafsi ya wenzao badala ya hoja za msingi.

Ni kweli kuna lile swali tunalojiuliza "waliosoma wametufikisha wapi"? Ila natoa tahadhari kama muwakilishi wako wa jimbo hata kaishia form 4 linapokuja swala la kujadili masuala mazito yanayowahusu kama uchumi ,teknolojia ,mifumo ya elimu huko bungeni yeye huwa sawa na bubu anachoishia ni kugonga meza tu. Sidhani kama mtu wa darasa la 7 anaweza kubishana na data za waziri wa fedha wakati hata decimals na percentage kwake ni msamiati

Nadiriki kusema hili limeifanya siasa ya nchi yetu kuwa ya vijembe na sio hoja ndio maana wabunge wetu wanaongea kutengeneza clip na kurushiana maneno mtandaoni.

Elimu inaweza kumpa mbunge urahisi wa kwenda nje na kukutana na wafadhili wakakaa meza moja na kuongea lugha moja ya "kimaendeleo" simaanishi kingereza na wakaelewana.

Tutake tusitake bi lazima tukubaliane na mabadiliko ya karne hii,bila elimu utaburutwa.

Namalizia kusemasidharau amabao hawajasoma ila najaribu kumtafuta atakayehoji nnachotamani ahoji hata vitabu vya dini vimesema "HAWAWEZI KUFANANA WALIOSOMA NA AMABAO HAWAJASOMA"

Katiba imeruhusu ila sisi wananchi tukatake "WABUNGE WA STANDARD 7 NA FORM 4 MWISHO 2020"
 
Back
Top Bottom