Shishye
JF-Expert Member
- Feb 26, 2009
- 269
- 1
Kuna jambo linanitatiza kwa muda sasa, nimefikiria sana jibu lake silipati. Nimeona niliweke hapa mbele yenu muweze kunisaidia. Mtu anapoamua kugombea ubunge anakuwa na kazi yake anayoifanya labda mkulima, mfanyakazi au biashara. Je akishaupata huo ubunge, kuna sheria yoyote inayomtaka aachane na shughuli alizokuwa anazifanya? Nimekuwa nikiona waajiriwa wengi wakiacha kazi au kuchukua likizo bila malipo pindi wapatapo ubunge, mfano Prof. Mgombelo kipindi kilichopita alikuwa mbunge na aliacha kufundisha chuo muda wote wa ubunge wake. Wapo pia akina Victor Mwambalasi ambaye alikuwa ameajiriwa kwenye kampuni binafsi na ameendelea na kazi hiyo hata baada ya kuwa mbunge. Wapo pia wafanya biashara kadhaa kama Karamagi wanaoendelea na bishara zao na wakati huo huo ni wabunge. Swala langu ni kuwa, unapokuwa mfanyakazi sehemu fulani na huku ni mbunge; kama mbunge unatakiwa kusimamia utendaji wa taratibu na sheria za nchi na utekelezaji wa maswala mbalimbali; kama mwajiriwa wakati mwingine wewe uko katika utendaji au maslahi yako yanaathirika kwa utekelezaji wa sheria fulani. Napata shida kujua kuna mwongozo gani katika hili. Good governance inahusika hapa, na inakuwaje?