Ubunge jimbo la Sikonge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubunge jimbo la Sikonge

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tumsifu Samwel, Jun 3, 2010.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmoja ya wagombea ubunge kwenye jimbo la sikonge ni balozi David Kapya ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la UNHCR na sasa yupo Office ya rais mstaafu Benjamin W. Mkapa.
  View attachment 10705

  Kesho ndio anaanza ziara ya kutembela jimbo la Sikonge na kukutana na wazee na wapambe wake..

  Itakuwa siyo vibaya tukajadili jimbo ili na sifa za wagombea ubunge kwenye hili jimbo..
   
 2. E

  Edo JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hajachelewa kweli huyu kuenda sasa? Mwambie asiende na maji ya chupa mikutanoni ! au kwenye mizunguko ya kuwaona wapiga kura watarajiwa
   
 3. d

  damn JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  anaonekana kiumri yuko sawa kiumri na mzee Malechela. au kwa kuwa sijafaa miwani!!!!!!!!!???
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenichekesha sana kwa hili. Unanikumbusha mgombea mmoja niliwahi kukutana nae Tabora mjini mwaka 2000. Yeye alikuwa anatembea na muhogo mbichi mkubwa halafu anaumenya kwa meno kila aendapo, alikuwa anaongea na kile kinyamwezi cha ndani hasa ila alifanikiwa kupata ubunge kwa kipindi kimoja kabla hawajamshitukia kuwa ni mtu wa fix 2005.
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nakumbuka mgombea mmoja huko maeneo ya longido alikuwa akitembea huku kavaa rubega na akiwa anavuta ugoro wake
   
 6. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu, mzee Malechela alisema wao ndio wanahitajika bungeni ili kuweza kutoa ushauri , nadhani ndio maana na Balozi Kapya ameona akamuunge mkono ili watoe ushauri zaidi kwa serikali.
   
 7. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Mungu wangu. David Kapya mbona hakuniambia nimshauri jamani??Njia ya kwenda bungeni ina michongom
  a na mshimo mengi kweli. Yule bwana mdogo Mkumba is very smart. Atamweza kweli?
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu kazi ya Mbunge siyo kuishauri serikali, bali ni kuisimamia serikali na kuikosoa. Ushauri unaweza kukubaliwa ama kukataliwa. Lakini linapokuja swala la kuisimamia serikali, ni kwamba lazima serikali itekeleze yale ambayo inapaswa kuyatekeleza.

  Haya mambo ya ushauri ndiyo yamefanya hoja za Richmond na Ufisadi zimekufa kibudu. Ukiweka kipengele cha ushauri ndipo unapoipa serikali mwanya wa kufanya yale wanayoona yanafaa hata kama yako kinyume, maana huwezi kuwafanya lolote.

  So mtu yeyote mwenye mawazo ya kwenda kuishauri serikali, sidhani kama anafaa kuwa Mbunge. Mbunge anatakiwa awe na ujasiri wa kuisimamia serikali na pia awe na vision ya kupeleka maendeleo jimboni kwake na si vinginevyo. Ni namna gani atashirikisha wananchi, serikali na wafadhili ili kuhakikisha huduma za jamii zinawafikia wananchi?
   
 9. c

  chibhitoke Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu kazi kubwa, pia yupo kijana mwanasheria wa Zanzibar Insurance- Benjamin Lupia naye pia anagombea na anaungwa mkono sehemu nyingi sana huko Sikonge
   
 10. K

  Keil JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nkumba is not smart, alikuwa na advantage moja kwamba alikuwa anabebwa na baba yake kwenye kura za maoni. Mzee Nkumba alipoteza uenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora kwenye uchaguzi wa 2007, so Bwana mdogo Said Nkumba hana ujanja.

  Kama umekuwa ukifuatilia mijadala, Nkumba amekuwa akilia kila siku kwamba Rostam Aziz ana agenda ya kummaliza. Wengine wanasema kwenye uchaguzi wa CCM 2007, RA alikataa kumuunga mkono Mzee Nkumba S. Nkumba, na matokeo yake Mzee alipoteza uenyekiti.

  Kwa maoni yangu, kiti cha Ubunge Jimbo la Sikonge ni kama vile kiko wazi na mwaka huu Nkumba hawezi kuvuka kwenye kura za maoni. Mojawapo ya sababu za kutovuka ni ugomvi uliopo kati ya Nkumba na RA. Wengi walio kwenye nyadhifa za CCM mkoani Tabora wako pro-RA.

  Siyo hilo, bado kuna maswali mengi ambayo yanahitaji majibu: Nkumba amefanya nini kwa kipindi cha miaka 10 ambayo amekuwa Mbunge? Barabara bado mbovu na hazipitiki nyakati zote. Barabara ya kutoka mkoani kwenda jimboni kwake (Wilaya ya Sikonge) ni matatizo matupu na hakuna ambaye anaongelea ujenzi wake.

  Mwaka huu JK alienda Kitunda, akakwama ikabidi chopper itumwe kwenda kumchukua huko ambako alikuwa amekwama. Huko alikokwama ni barabara kuu inayounganisha mkoa wa Tabora na Mbeya na sehemu kubwa ya barabara hiyo inapita jimboni kwa Bwana Nkumba. Kama barabara hiyo ingeweza kuwa inapitika kirahisi mwaka mzima, Sikonge ingekuwa na maendeleo ya kibiashara kwa kuwa ili mtu aende Mbeya, lazima aende kwanza Tabora mjini, apande treni mpaka Itigi, then apande mabasi. Au aende mpaka Dodoma au Morogoro, then apande mabasi kwenda Mby. Kwa hiyo biashara inakuwa ngumu sana.

  Wilaya ya Sikonge imekaa kushoto sana na wanahitaji sana barabara hiyo. Urambo wamekaa kushoto, lakini reli inawasaidia pindi ikiwa inafanya kazi. Pia sasa hivi wana barabara nzuri na inapitika mwaka mzima. Wilaya za Igunga na Nzega wameunganishwa na barabara kuu (Dar - Mwanza). Ni wilaya ya Sikonge tu ndiyo ambayo imebaki kama kisiwa. Inahitaji Mbunge mwenye vision na atakayeweza kuibana serikali ili wajenge hiyo barabara. Hilo linaweza kufanyika kwa kushirikiana na wabunge wa Chunya, Mbeya mjini na Mbeya Vijijini ambao wanaweza kufaidika na ujenzi wa barabara hiyo.
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Best si nilikueleza kuwa ukishaingia jf kutoka ni ngumu? unakumbuka juzi ulipiga mwano dunia nzima ukitaka utoke hapa jamvini? Anyways nafurahi kuendelea kukuona hapa jamvini. Back to the mada, kuhusu huyu jamaa si mbaya akigombea ila kwa umri mh kazi ipo. Tatizo ukigombea kupitia chama hiki hainiingii akilini kama kweli utaweza kweli kupambana na ufisadi kutoka ndani!
   
 12. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #12
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Genekai, umenifananisha na twin wangu.
   
 13. telele

  telele Member

  #13
  Jun 4, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Mwaka huu kazi kubwa, pia yupo kijana mwanasheria wa Zanzibar Insurance- Benjamin Lupia naye pia anagombea na anaungwa mkono sehemu nyingi sana huko Sikonge Mwaka huu kazi kubwa, pia yupo kijana mwanasheria wa Zanzibar Insurance- Benjamin Lupia naye pia anagombea na anaungwa mkono sehemu nyingi sana huko Sikonge"

  umefanya utafiti kuthibitisha kuwa huyo jamaa anaungwa mkono na watu wengi au ni ushabiki tu wa wapambe wake wanaotaka kumlia hela zake alizodunduliza? Nkumba bado ana nguvu sikonge japo RA anamfitini sana.
   
 14. E

  Edo JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Nkumba yuko na kina Mwakembe; hivyo lazima apambane na RA
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Huyu Nkuba ni weak! kafanya nini kule Sikonge sitaki hata kumwona - wilaya maskini kupita kiasi wakati kuna asali na mbao za mininga ameshidwa hata kutafuta soko kuwasaidia wananchi wa wilaya hii - vijana wamejichokea. mi nafikiri arudi akafundishe primary - we need young and aggressive person.

  Kilimo cha Tumbaku - kimeshakufa soko bovu
  Asali - Nyingi hakuna soko
  Mbao za mininga - Haziwasaidii wananchi wa wilaya hii
  Barabara Mbovu, Jimbo halina hata barabara hata moja inayopitika muda wote ni kama kisiwa.

  Ni kati ya wilaya za mwisho kabisa ki maendeleo.
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Loohh, Vadugu vane (wandugu zangu),

  Huu mjadala kwa kweli ulinipita kushoto na asante Keil kwa kunishtua. Nilishindwa kuupata hadi nikatumia jina la huyo mzee David Kapya.

  Kumbe Sikonge ina watu wengi tu. Mie nilifikiri tumechoka sana na hatuna watu wanaoweza kuisaidia Sikonge yangu hii.

  Huyu Mzee na Nkumba nadhani wote hawafai. Too sad Yongolo hawezi kugombea kwani eti na sisi Wanyamwezi tuna ka URAIA.

  Walimkatalia baba yake na kisa tu kuwa Yongolo ni Wahamiaji. Upuuzi wa hali ya juu. Tunakubali kuwa na Nkumba kama Mbunge na kisa tu kwa sababu ni Mzawa na jamaa ni kweli kabisa ni MWALIMU WA SHULE YA MSINGI.

  Ngoja nipate more datas na ntachangia zaidi hii kitu.
   
 17. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unaweza kutupa sababu za wewe kusema Nkumba Na Kapya hawafai?
   
 18. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Sikonge,

  Hivi Keil naye wa maeneo hayo?

  Wachambueni hawa wakuu wa Sikonge basi ili tuwaelewe, au mna nguvu ya kuchambua ya Kyela tu?

  Nilikuwa nafikiri Sikonge mko hoi kabisa, naona mna watu wengi tu wazuri.

  La mgambo karibu linalia.
   
 19. m

  mwanamilembe Member

  #19
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Sikonge

  Mimi hao wanyamwezi waliniacha hoi mwaka 2000 pale walipomkata Jaji Lameck Mfalila wakampa huyo Saidi Nkumba
   
 20. K

  Keil JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mtanzania,

  Mimi nina multiple-citizenship ya Rungwe, Kyela na Sikonge. Kwa hiyo zikija siasa za Rungwe Mashariki na Magharibi nitachangia, zikija za Kyela nitachangia na zikija za Sikonge pia nitachangia. Michango yangu ni ya ku-identify weaknesses ili mhusika aweze kuzifanyia kazi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake na wananchi waliomchagua.
   
Loading...