DOKEZO Ubunge Afrika Mashariki rushwa tupu ndani ya CCM

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
335
495
Tayari Chama Cha Mapinduzi kimepitisha majina ya wanachama wake watakaopigiwa kura za maoni na kamati ya wabunge wa CCM kwaajili Ubunge wa Africa mashariki (EALA).

Mchakato huu tayari umegubikwa na rushwa za kutisha, ambapo wagombea wa nafasi hiyo wanalazimika kutoa rushwa kubwa kushawishi kupigiwa kura na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo chetu kimenasa jinsi rushwa inavyotembea jijini Dar es Salaam na Dodoma ambapo wagombea wanawahonga wabunge ili kupata kura.

Tumejiridhisha pasina shaka kwamba wabunge wana njaa kupita maelezo hivyo wanadai kupewa rushwa ili kutoa kura zao. Kiasi cha rushwa kinachotolewa ni kuanzia sh 1,000,000/= hadi sh 3,000,000/= kwa Mbunge mmoja.

Mpaka sasa mgombea anayetajwa kutoa rushwa kufuru ni Dkt. Ngwaru Maghembe mtoto wa Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe. Ambaye anatajwa kutoa Sh 2,000,000/ hadi 3,000,000/ kwa kila Mbunge . Ngwaru anatajwa kuanza kutoa rushwa kwa wabunge tangu mwaka 2021 na wabunge wamethibitisha hilo.

"Aisee huyu Ngwaru anatoa pesa na amedhamiria kununua Ubunge kwa gharama yeyote na ameteka wabunge wote," alidokeza Mbunge wa Jimbo moja la Nyanda za Juu Kusini. Ngwaru Maghembe anafanya fujo zote hizi bila woga na tayari amepitishwa kugombea nafasi hiyo na chama chake.

Hii ni salamu na ishara ya wazi kwamba siasa za rushwa na ukubwa wa mfuko ndani ya CCM zimerudi upya, hivyo wanyonge wajiandae kisaikolojia. Na hiyo ni dalili kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, ndani ya CCM ni mnada wa ushindani wa ukubwa wa mifuko Ili upate uongozi.

CCM chini ya Samia Suluhu Hassan, Godfrey Chongolo na Abdurhaman Kinana imeanza kutoa taswira halisi huko mbele tuendako, ambapo rushwa ndiyo itakuwa sifa na mtindo wa kupata uongozi.

Utaratibu wa kutoa kitu chochote kwa wajumbe ndio utaratibu unaokubalika ndani ya CCM. Huwezi kupita katika kinyang'anyiro chochote kile bila ya kuwapooza wajumbe kwa kutoa chochote kile kwao kuanzia ngazi ya shina mpaka taifa.

Rushwa ni sehemu kubwa ya hamasa kwa wajumbe wenye dhamana ya kuchuja majina ya wagombea. Wala jambo hili halina ubishi.

Ili jina lako lipite ni lazima utoe rushwa kubwa kuliko wagombea wenzako, na "this is very acceptable rule of thumb" hata kama haipo kimaandishi, bali ipo kihisia zaidi ndani ya chama hiki.
 
Nampongeza sana Pascal Mayalla kwa kutoshiriki mchezo wa rushwa za uchaguzi. Inaonekana uwezo wake kwenye kujenga hoja ni tishio kwa wahafidhina wanaoamini kwenye siasa za figisu figisu.

Hizi habari za rushwa zipo na zimetamalaki kuanzia chaguzi za ndani za CCM kuanzia ngazi ya tawi hadi mkoa.

Rushwa inatembea kama nini huko, lakini hatimaye vyombo vinavyohusika vinafumbia macho haya madudu kwa sababu ni kama wanalinda hadhi za wakubwa endapo hatua zikichukuliwa.

Dawa ya Tanzania ni kukabidhi nchi kwa chama mbadala chenye nia njema na nchi hii ili kuweza kupata mwanzo mpya wa maendeleo na mustakabali wetu
 
Tayari Chama Cha Mapinduzi kimepitisha majina ya wanachama wake watakaopigiwa kura za maoni na kamati ya wabunge wa CCM kwaajili Ubunge wa Africa mashariki (EALA ).

Mchakato huu tayari umegubikwa na rushwa za kutisha, ambapo wagombea wa nafasi hiyo wanalazimika kutoa rushwa kubwa kushawishi kupigiwa kura na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo chetu kimenasa jinsi rushwa inavyotembea jijini Dar es Salaam na Dodoma ambapo wagombea wanawahonga wabunge ili kupata kura.
Je huyu ni wakala👇
 
Tayari Chama Cha Mapinduzi kimepitisha majina ya wanachama wake watakaopigiwa kura za maoni na kamati ya wabunge wa CCM kwaajili Ubunge wa Africa mashariki (EALA ).

Mchakato huu tayari umegubikwa na rushwa za kutisha, ambapo wagombea wa nafasi hiyo wanalazimika kutoa rushwa kubwa kushawishi kupigiwa kura na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo chetu kimenasa jinsi rushwa inavyotembea jijini Dar es Salaam na Dodoma ambapo wagombea wanawahonga wabunge ili kupata kura.

Tumejiridhisha pasina shaka kwamba wabunge wana njaa kupita maelezo hivyo wanadai kupewa rushwa ili kutoa kura zao. Kiasi cha rushwa kinachotolewa ni kuanzia sh 1,000,000/= hadi sh 3,000,000/= kwa Mbunge mmoja.

Mpaka sasa mgombea anayetajwa kutoa rushwa kufuru ni Dkt. Ngwaru Maghembe mtoto wa Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe. Ambaye anatajwa kutoa Sh 2,000,000/ hadi 3,000,000/ kwa kila Mbunge . Ngwaru anatajwa kuanza kutoa rushwa kwa wabunge tangu mwaka 2021 na wabunge wamethibitisha hilo.

"Aisee huyu Ngwaru anatoa pesa na amedhamiria kununua Ubunge kwa gharama yeyote na ameteka wabunge wote," alidokeza Mbunge wa Jimbo moja la Nyanda za Juu Kusini.
Ngwaru Maghembe anafanya fujo zote hizi bila woga na tayari amepitishwa kugombea nafasi hiyo na chama chake.

Hii ni salamu na ishara ya wazi kwamba siasa za rushwa na ukubwa wa mfuko ndani ya CCM zimerudi upya, hivyo wanyonge wajiandae kisaikolojia. Na hiyo ni dalili kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, ndani ya CCM ni mnada wa ushindani wa ukubwa wa mifuko Ili upate uongozi.

CCM chini ya Samia Suluhu Hassan, Godfrey Chongolo na Abdurhaman Kinana imeanza kutoa taswira halisi huko mbele tuendako, ambapo rushwa ndiyo itakuwa sifa na mtindo wa kupata uongozi.

Lini rushwa ya nafasi za za kugombea ndani ya Ccm ilisitishwa kwa mda?
 
" CCM kuna Mafisi" JK
Kazi ya fisi nadhan unaijua au fisi akiiingia mahali nini kinatokea

1662829151499.png
 
Mkuu naona Kama unamchafua tu Ngwaru Maghembe,pamoja na yote yule jamaa yupo vizuri kuanzia Elimu mpaka Ujenzi wa hoja.Ata Maswali anajua kujibu,nakumbuka awamu yake ya kwanza na ya pili alifanya vizuri kushawishi wabunge wampigie kura.Sikatai utoaji wa Rushwa CCM ni utamaduni lakini jamaa ni mzima kichwani.
 
Acha kuchafua majina ya watu na chama chetu, wewe Kama umezidiwa huko achia ngazi, pambana kupata kura kwa wajumbe, siyo umeshindwa kuwashawishi wajumbe halafu unakuja kuchafua watu hapa na chama chetu, usituchafulie chama chetu kwa udhaifu wako wa kushindwa kuwashawishi waheshimiwa wabunge

Pili acha kuwachafua wabunge wetu kwa kusema wananjaa, lini ulikuta wameshindwa na njaa ukawalisha chakula?
 
Hii ni salamu na ishara ya wazi kwamba siasa za rushwa na ukubwa wa mfuko ndani ya CCM zimerudi upya, hivyo wanyonge wajiandae kisaikolojia. Na hiyo ni dalili kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, ndani ya CCM ni mnada wa ushindani wa ukubwa wa mifuko Ili upate uongozi.
Nina maoni mawili
1. CCM haijawahi kujitenga na rushwa hata siku Moja
2. Heri Ubunge wa rushwa kuliko Ubunge wa Mtanzania mmoja kujifungia mahali na kuwachagulia Majina ya Wabunge anaotaka yeye
 
Rushwa inatembea kama nini huko, lakini hatimaye vyombo vinavyohusika vinafumbia macho haya madudu kwa sababu ni kama wanalinda hadhi za wakubwa endapo hatua zikichukuliwa.
Nao wanapenda rushwa kuliko hata maisha yao
 
Back
Top Bottom