Ubunge Afrika Mashariki, CHADEMA hawapati kitu

Ubunge Afrika Mashariki, CHADEMA hawapati kitu

Kama TL wakawaida tulizeni makalio sasa.tabia ya kumfuatafuata na kuwasumbua majaji wetu kwa kesi za kipuuzi ikome kuanzia leo .
Akiwa na tuhuma lazima atachukuliwa.Na wewe kalisha makalio usingilie SERIKALI.
 
Mimi navyoona vyama sio hoja ila hapa naona kama wagombea walipelekwa na ACT ni vichwa vya maana hata kama tungetoa vyama wakawa wanagombea wagombea bila kujua vyama Prof Kitila naona yuko vizuri kuliko Masha na Wenje
 
Kanuni zinazoongoza mabunge ya Afrika Mashariki inasema wabunge watakaowakilisha nchi zao katika bunge la Afrika Mashariki watatoka katika makundi mawili, chama tawala (chama dola) na vyama vya upinzani.

Kutokana na Zitto Mwami na Naibu Spika kusoma kanuni vyema sasa wagombea wote wa upinzani watakuwa katika kapu moja. Tayari Chadema imewapeleka Lau Masha na Wenje. ACT inawapeleka Prof. Kitila Mkumbo na Wakili Albet Msando. NCCR imempeleka Mama Ndurikio. CUF makundi yote ya Maalif na Lipumba wamepeleka wagombea...

Kwa uhasama wa kivyama kati ya CCM na CHADEMA kuna kila dalili Prof. Mkumbo na Msando wakashinda...

Note: Hukumu ya Komu haiko applicable katika uchaguzi huu

ed0812c387bc444eae505e8b098c3373.jpg
UMESEMA UKWELI NA HIVYO NDIVYO ITAKAVYOKUWA: NI WAGOMBEA WA ACT NA CUF YA LIPUMBA NDIO WATAPITA - MASHA NA WENJE OUT
 
Mnachekesha nyie mamburula mara ngapi mmempeleka mahakamani anawaburuza? Majaji wamechoka na kesi uchwara mnazomfungulia kila siku.
Mburula utakua wewe usiyejua kua kwenye kesi Kuna kushinda na kushindwa Cha msingi haki itendeke tu.
 
hahahhahaha ccm bhana naona mnajitia moyo kuwa mnaikomoa chadema
Sasa maana ya upinzani si ni kukomoana? Unataka ccm wamkomoe nani kama si chadema kwani ndiye mpinzani wake mkuu? Na chadema kwani huwa wanamkomoa nani kila kukicha kama si ccm?
 
Kuna ajenda kubwa nyuma ya chama cha Act wazalendo inayoongozwa na Zitto na Kitila katika issues ya Ubunge wa Africa mashariki, na wanao chezesha mchezo huu ni ccm , walichofanikiwa mpaka sasa ni Cuf kupata katibu mkuu mpya, na kupata wagombea watatu wa Ubunge wa EALA.
Wakati huku mnaendelea kupambana na Zitto na kitila huku Cuf wanafanya yao Kwa kupeleka majina matatu ambayo yatadainiwa na katibu mpya Sakaaya Kwa katibu wa bunge Kashilala.
Hi game umechezewa very professional, kitila sio kama anatoka Ubunge wa EALA kazi yake ni kuwavuruga watu wasiitizame Cuf Daaaaah Siasa ni mchezo mchafu mmnoo.
 
Back
Top Bottom