Ubovu wa CT scanner MNH-Maoni ya mtaalamu!

Ubovu wa CT scanner MNH-Maoni ya mtaalamu!

Kuna mambo mengi Tz ni Top down approach na ufanisi ni 0 ?. Unapewa Resoponsibilities ila full authority 0? tureview haya mambo. Mikataba mingi ya equipment ina unnecessary strings ili kudominate bussness, wanasign bila kisoma. Wakurugenzi Wakuu wengi hawataki kushuka toka viti vyao. Wagonjwa wanalala chini huko MD or ED hashuki kutembelea anafurahia kiyoyozi na mashangingi na bize safari za nje kudaka Per Diems. Shame! Hand on on everything!Uzoefu wa JPM kule ujenzi na Tanroads hakika utatusaidia hasa kwenye mikataba ya kimataifa, procurement and close followup on gvt bussiness. Bravo JPM.
 
BOss wa muhimbili alizoea kufanya kazi kwa mfumo - alalamike kuwa mashine hazifanyi kazi ahamishwe - kuweni na macho ya kuoa mbali kwenye utawala wa JK -ukifanya vizuri unahamishwa -ukifanya vibaya unahamishwa vile vile
 
Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya #HAPAKAZITU basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA #HAPAKAZITU
Very, very and very good presentation
 
Lakini kama utaona ziara ya magufuli hajatoa uamuzi pale pale hospital, na alikuwa akiuliza maswali pia, mbona hayakuja majibu kama haya? Na wao wanamjua alivyo!! Kwangu mimi naona ni utetezi tu, kuna uzembe mkubwa wizara nzima sio muhimbili tu

Nakubaliana na wewe.
 
Kila siku afadhali ya jana, haya hatuyataki, mhimbili wacha wakipate cha moto tu, wakiaachwa watajidai sana.
 
Badilisha mfumo, badilisha timu inayoendesha huo mfumo kama haifanyi kazi vizuri - siyo mtu mmoja mmoja. Hiki ndicho Magufuli anapaswa kufanya. Hii kuibukia shirika moja moja, then kutimua bosi mmoja/wawili wa shrika wakati sote tunafahamu kuwa maamuzi ya serikali yamekuwa yanaenda kwa ngazi huku yakihusisha wengi na teuzi nyingi za hao 'wabovu' zikianzia hukohuko ikulu, is a political stunt to say the least and won't get us very far. Naunga mkono nia ya Magufuli lakini naona kama strategy bado ni tatizo.

Nilivyomuelewa mtoa mada ni kwamba Je? huyo wa Muhimbili alichukua hatua gani baada ya tatizo kutokea?? Nina uhakika akimuoneysha barua Magufuli aliyoandika wizarani kuhusu hilo tatizo basi angepona au kama angemuonyesha magufuli income inayoingia pale Muhimbili kuwa haikutosha kuvitengeneza naamini leo angekuwa kazini kwake, KILICHOTOKEA NI KWAMBA Majibu aliyompa rais hayakuridhisha, vikao vyao vinacost mpaka 3m posho tu, wakati ct scan na MRI MATENGEZO YAKE NI 3M Hiyo hiyo, Hata mimi nakufukuza, Huyu baba yani kila siku namtia kwenye maombi amenigusa sana yani unamuhisi kabsaa anagusa wananchi wa hali ya chini kama rais alivyosema wanafanya makusudi ili wagonjwa waende kwenye hospital binafsi. Mungu aendelee kumlinda na aendelee miaka yote 10.
 
unayosema yanawezekana yana ukweli kwani msemaji wa muhimbili anasema wanasubiri mtaalamu toka philips aje atengeneze nikajiuliza waliwezaje kuagiza mashine bila kuaandaa watu wa kuitengeneza
nafikiri Magufuli anatakiwa kuwa member humu ili tumsaidie kujua asiyoelezwa na wasaidizi wake
 
Magufuli kabla hajawa rais nadhani alikuwa anajua kila sekta na uchafu wake, kama mliiona ile clip amesema kuna dr. aliwahi kuharibu hizo mashinde halafu anawaelekeza kwenye hospital yake binafsi, kwahiyo msidhani hayo anayofanya ni vitu alivyowaza ndani ya week moja tangu aapishwe, huyo mzee anajua anachofanya kuna aliondolewa hapo kupelekwa wizarani hatujuia anaenda chukua nafasi ya nani huko wizarani ni wazi bado kasi inaendelea.
 
Wizara ya afya ina matatizo wala wasiingizie hospital,ni kawaida ya wakubwa wanaoteuliwa na rais kubebana,matatizo yapo mengi sana mfano huduma za bima ya afya kwa watumishi kwa hospital za serikali mfano muhimbili ni kama adhabu fulani watumishi wa serikali wanalalamika kila kukicha kwa kukosa huduma za kuridhisha kwenye hospital za serikal.Hiv sasa kuna kamchezo kanafanywa na hospital binafsi via bima ya afya.Siku hizi watumishi wa serikal na wategemez wao wanajazana pale kairuki,aghakan n.k.hii nalo linabidi liangaliwe
 
sikuwa tanzania kipindi hicho... nilikuja MNH 2013 nkafanya kazi mwaka nkaona mazingira hayanirihusu na ni magumu vitendea kazi hakuna , mgonjwa anakufa sababu dawa ambayo ina 3000 nje.... nkaona isiwe shida nkaondoka bongo tena ..

magufuli akirekebisha tunaweza kurudi

Daktar Ulimboka Yuko wapi?
 
What Dr. JPM is showing is leadership style.

By the time anaapisha Baraza la Mawaziri watakuwa wana picha ya namna mkuu wao anataka kufanya ktk kutatua kero za wananchi ktk sekta mbalimbali.

Haina maana kuwa atakuwa anazunguka hivyo forever na haina maana pia kuwa ataacha. Mazingira at that material time yataamua.

Queen Esther



Mkurugenzi wa MNH angewezaje kwenda IKULU tena ya Kikwete kuishtaki Wizara yake? Kesho yake angepata uhamisho Lindi. Naamini alipeleka taarifa kwenye Bodi ambao nfio wangelifikisha kwanza Wizarani, kama halikutatuliwa wangepeleka IKULU. Dr Magufuli hawezi kutatua matatizo yaliyolimbikizwa na mtangulizi wake, tayari kuna tafiti ya kero zote, aunde Baraza Lake la Mawaziri, aingie nao mkataba na utendaji kazi uanzie chini kuja juu, apate weekly report. Atuzungukia taasisi ngapi nchi nzima?
 
Siku magufuli akikanyaga tu pale Dawasco kimara basi namnunulia mbuzi maana kuna watu wazembe sijapata kuona chini ya jua
 
Well said.

Wahusika pelekeni macho yenu kwenye hizi private hospitals na bima ya Afya. Kuna watu wanavuta ili wauwe kabisa hospital za Serikali. Wahusika ni hao walioko jikoni.

Queen Esther

Wizara ya afya ina matatizo wala wasiingizie hospital,ni kawaida ya wakubwa wanaoteuliwa na rais kubebana,matatizo yapo mengi sana mfano huduma za bima ya afya kwa watumishi kwa hospital za serikali mfano muhimbili ni kama adhabu fulani watumishi wa serikali wanalalamika kila kukicha kwa kukosa huduma za kuridhisha kwenye hospital za serikal.Hiv sasa kuna kamchezo kanafanywa na hospital binafsi via bima ya afya.Siku hizi watumishi wa serikal na wategemez wao wanajazana pale kairuki,aghakan n.k.hii nalo linabidi liangaliwe
 
Back
Top Bottom