Ubovu wa CT scanner MNH-Maoni ya mtaalamu!

Ubovu wa CT scanner MNH-Maoni ya mtaalamu!

Mswahili ukimruhusu ajitetee hautamuweza wewe fukuza watalaumiana mbele ya safari
 
Mswahili ukimruhusu ajitetee hautamuweza wewe fukuza watalaumiana mbele ya safari

Ni kweli mkuu...lakini waswahili wote kwa hadhi zote lazima washughulikiwe!

Inawezekana waswahili wa wizarani walisikilizwa na huyu mswahili wa MNH akawajibishwa!
 
Ni kweli mkuu...lakini waswahili wote kwa hadhi zote lazima washughulikiwe!

Inawezekana waswahili wa wizarani walisikilizwa na huyu mswahili wa MNH akawajibishwa!

Wahenga walisema Samaki Mmoja akioza!
 
Na serikali ni vizur iwajibike koz lile deni lake kwa msd ndo limechangia sana kudhoofisha muhimbili
 
Na serikali ni vizur iwajibike koz lile deni lake kwa msd ndo limechangia sana kudhoofisha muhimbili

Naam mkuu ...hata swala la ukosefu wa dawa inabidi wawajibishwe wengi sio mmoja tu
 
Kuna uzembe mkubwa sana kwenye udhibiti wa mapato ya moja kwa moja ya taasisi mbalimbali
Mashule, vyuo, zahanati na hospitali, Tanapa, mahakama, polisi nk ni taasisi za serikali ambazo zina mandate ya kukusanya mapato moja kwa moja.
Udhibiti wa mapato hayo ni tatizo kubwa sana...
 
mleta uzi umenena vema sana!! Ila kwa swala la directorna afukuzwe tu maana yeye ndo aliekua full incharge wa muhimbili...hao ma procurement officers na panya wengine ilikua kaz yake kuwaajibisha but coz aligawana nao ten paseee acha imcost!! about wizara bado director hakufanya enough effort so aende zake huko
 
Aje na kwetu huku Amana Temeke na mwananyamala maana nako huko ni vioja vitupu,Hospital I inaongozwa AMO halafu chini yake kuna Specialist,sijui wanajadili nae nini.wanaweka watu kwa faida wanazozijua wao.
 
Hawa mafundi wa CT scan wanasomea chuo gani? Usijekuta hata mafundi hatuna hadi watoke Nairobi, tizama hizi photocopy za maofisini mafundi kila siku wanavuta hela na haziponi sembuse hizo fotocopy za mwili.
 
Yap...kuna samaki wengi wsliooza wameachwa bila kuondolewa!

Lazima unapata nao chai hao umeacha tu kutumwagia mboga.

Kuna yayoyojifichaga pia na wafanya bidii kuleta huduma hawaonekani sababu wanakuwa kikwazo kwa walaji.
 
kama kweli tunataka mabadiliko ya kweli lazima bunge lifanye marekebisho makubwa ya katiba na sheria mbalimbali katika wizara mbalimbali. nchi hii kila idara ina tatizo sio ardhi, uchukuzi, elimu,afya, na hata maji. maamuzi mengi yanachukuliwa na wachache mawizarani na kupelekea kuingia mikataba isiyo na maslahi kwa umma kisa 10%.
 
Raisi wetu ana nia nzuri na taifa hili lakini naona kwamba kuna baadhi ya watendaji serikalini watamkwamisha,
na sipati picha Wazili wa afya atakayemchagua kama ataendana na kasi ya Raisi wetu.

ikimpa mwakiembe pm, hawatayumbishwa.
 
Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL] basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL]

Umenena vyema kwa kweli kama taifa tunatakiwa kuacha kushabikia hizi mbwembwe za kisiasa na badala yake watu hususan waandishi wa habari watafute facts ktk haya yanayoendelea. Kwa mtazamo wangu matatizo ya watu wanyonge yametumiwa ili wale wale ambao walikuwa wanaacha kutimiza wajibu wao wa kutoa fedha za malipo ya wakandarasi kujijenga kisiasa.
Mathalani kutangaza kufuta bodi iliyo maliza muda wake ni kujitafuta umaarufu wa kisiasa (cheap popularity). Hata sasa kwa mujibu wa sheria zetu za manunuzi wakandarasi hao wasipolipwa mashine hizo hazitatengenezwa.
 
Mkuu..huu ndio ukweli katika sekta hii ya afya ct scan na MRI ni mifano tu ya tatizo kubwa katika sekta hii.

Mtafuteni Dr Ulimboka alipo anaweza kuelezea upuuzi wote, , tatizo madaktar toka Jk awapige Mkwara hata maadili yenu hamtaki kufanya
 
umenikumbusha 2013 wakati nipo MNH hakuna diclofenac twaambia wagonjwa wakanunue nje.. hali ile mi ilinikera sababu wagonjwa wa idara yangu wanahitaji sana dawa za maumivu.. nkamuuliza intern pharmasist mmoja akanambia ... muhimbili inatakiwa ichukue dawa kwa supplier flani nimesahahu nadhani ni MSD na si kwengineko na kama hawana ndio imekula kwetu , na pia kulikuwa na Tatizo hospitali inadaiwa... supplier amesitisha zoezi la kuleta dawa...

hii mikataba huwa watu wanaingia huku wakipewa pesa ndio maana wanaingia mikataba mibovu!!,....

mwisho wa siku tunakuja kupata lawama madactari tunabania dawa,, tuna maduka nje ..... makatili mgonjwa ana maumivu hatuwapi dawa.... et cal

kwa utawala huu wa awamu ya 5 mambo yatabadilika i hope Insha Allah

MSD ni taasisi ya serikali chini ya wizara ya afya na ndio yenye mandate ya kununua na kusambaza dawa ktk hospitali,vituo vya afaya na zahanati za serikali nchi nzima kwa kutumia fedha zinzotengwa ktk bajeti.

Mwaka 2013/4 wakati wafadhili walipositisha misaada kwa sababu ya kashfa ya escrow, serikali ilishindwa kuwasilisha kwa wizara mbali mbali fedha zilizotengsa ktk bajeti, hii ikiwa ni pamoja na Wizara ya Afya. Hivyo Wizara ya Afya ikashindwa kuilipa MSD fedha za dawa ilizosambaza ndio maana hospitali zote nchi nzima zikakosa madawa. Hata sasa bado MSD wanaidai mabilioni ya fedha ndio maana ktk hospitali za umma upo uhaba sa dawa.

Kinachofanyika sasa na watawala ni kujaribu kuwasahaulisha wananchi kiini cha hospitali za umma kukosa dawa na vifaa tiba kuwa ni kashfa ya escrow iliyosababisha misaada kukatwa na serikali kushindwa kuwalipa watoa huduma wake na kusukumia hospitali binafsi na maduka ya dawa matope.
 
Hakuna cha kuwatetea hao wezi wa muhi2 fukuza kazi tu,ct scan za private mbona zinafanya kazi? Hilo ni genge la wezi.
 
Picha ninayo ipata ni kuwa hakuna mzembe atakayepona

Huko mawizarani wazembe wote watafute milango ya kutokea

Si muda mrefu chanzo cha matatizo kadhaa kitaaanza kujulikana kama ni mikataba mibovu au watendaji mmoja mmoja au lah. Mtu akipigwa chini yeye mwenyewe au watu tutaanza kujadili ana nini hasa chanzo. Halafu kwa kuwa rais ana nia ya dhati kurekebisha nchi hii atafanyia kazi chanzo cha tatzo

Tuna mapungufu mengi. Subir tuwekane sawa kwanza
 
Tusifanye kampeni za siasa kwenye afya za watu. Kutimua wengi si hoja. Kubadili mfumo ndio tija. Hao utakaowabadilisha hawatoki angani. Ni Wa TZ walewale. Labda serikali iingie mkataba na madaktari na management ya hospitali binafsi kwa kipindi cha miezi sita waje watusaidie kutengeneza mfumo Wa huduma za hospitality lzetu. Baada ya miezi 6 wawe wanakuja kila mwezi Mara mbili ili kuangalia kama bado tupo ndani ya mfumo wao. Ni Wazo kwa Magufuli na watz wapendao mabadiliko.
 
Back
Top Bottom