Ubovu wa CT scanner MNH-Maoni ya mtaalamu!

Nakuunga mkono mkuu. Wachangiaji wengi humu siyo wachambuzi wa mambo. Tatizo kubwa linaloikumba Serikali kwa sasa ni ya kibajeti. Taasisi nyingi zipo hoi kifedha. Ukifuatilia flow ya fedha kutoka Hazina kwenda kwny taasisi ndipo utagundua tatizo lipo wapi. Tulikuwa busy na kampeni hatukuwa tunafuatilia kinachoendelea. Hazina nao sijui walitudanganya kuhusu vyanzo vya mapato, sijui. Ila la msingi ni kwamba baada ya Bunge kumalizika Hazina waliziandikia Wizara zote kuwa bajeti iliyopitishwa haikuwa inatekelezeka hivyo wizara zitapewa 60%. Hivyo, kulikuwa na bajeti cut ya 40%. Hili wananchi wa kawaida hawalifahamu.

Binafsi naona watendaji wanaweza kuonewa sana huku tatizo la msingi likiwa halisemwi.

Umenena vyema kwa kweli kama taifa tunatakiwa kuacha kushabikia hizi mbwembwe za kisiasa na badala yake watu hususan waandishi wa habari watafute facts ktk haya yanayoendelea. Kwa mtazamo wangu matatizo ya watu wanyonge yametumiwa ili wale wale ambao walikuwa wanaacha kutimiza wajibu wao wa kutoa fedha za malipo ya wakandarasi kujijenga kisiasa.
Mathalani kutangaza kufuta bodi iliyo maliza muda wake ni kujitafuta umaarufu wa kisiasa (cheap popularity). Hata sasa kwa mujibu wa sheria zetu za manunuzi wakandarasi hao wasipolipwa mashine hizo hazitatengenezwa.
 
Nakuunga mkono mkuu. Wachangiaji wengi humu siyo wachambuzi wa mambo. Tatizo kubwa linaloikumba Serikali kwa sasa ni ya kibajeti. Taasisi nyingi zipo hoi kifedha. Ukifuatilia flow ya fedha kutoka Hazina kwenda kwny taasisi ndipo utagundua tatizo lipo wapi. Tulikuwa busy na kampeni hatukuwa tunafuatilia kinachoendelea. Hazina nao sijui walitudanganya kuhusu vyanzo vya mapato, sijui. Ila la msingi ni kwamba baada ya Bunge kumalizika Hazina waliziandikia Wizara zote kuwa bajeti iliyopitishwa haikuwa inatekelezeka hivyo wizara zitapewa 60%. Hivyo, kulikuwa na bajeti cut ya 40%. Hili wananchi wa kawaida hawalifahamu.

Binafsi naona watendaji wanaweza kuonewa sana huku tatizo la msingi likiwa halisemwi.

Tuache porojo, nichukulie mfano wa mama njelekela, alivyokuwa anapiga chaki alikuwa hodari wa kutuchangisha fedha za kukagua matiti, leo kawa boss wa muhimbili simsikii tena, inamaana huo upungufu wa budget hana? sasa huyu wa MOI hata kama alikosa budget aliitisha harambee tukashindwa kuchangia matengenezo ya hizo mashine, kwanza hata bei yake haifiki mil 60, isitoshe alikuwa anakaimu tu sasa si arudi kwenye kazi yake ya awali tatizo liko wapi?
 
umenikumbusha 2013 wakati nipo MNH hakuna diclofenac twaambia wagonjwa wakanunue nje.. hali ile mi ilinikera sababu wagonjwa wa idara yangu wanahitaji sana dawa za maumivu.. nkamuuliza intern pharmasist mmoja akanambia ... muhimbili inatakiwa ichukue dawa kwa supplier flani nimesahahu nadhani ni MSD na si kwengineko na kama hawana ndio imekula kwetu , na pia kulikuwa na Tatizo hospitali inadaiwa... supplier amesitisha zoezi la kuleta dawa...

hii mikataba huwa watu wanaingia huku wakipewa pesa ndio maana wanaingia mikataba mibovu!!,....

mwisho wa siku tunakuja kupata lawama madactari tunabania dawa,, tuna maduka nje ..... makatili mgonjwa ana maumivu hatuwapi dawa.... et cal

kwa utawala huu wa awamu ya 5 mambo yatabadilika i hope Insha Allah

Hivi wewe njiwa ule mgomo wa madaktari uliosbabisha vifov yya wananchi wasio na hatia ulikuwemo au hukuwemo?
 
Tunatakiwa tusikumbwe na upepo wa matukio. Mtakumbuka kumekuwa na mijadala kwa nyakati tofauti hususani wakati wa bajeti ya wizara ya afya kuhusu hali ya huduma za afya ktk hospitali za serikali.

Hakuna jipya kuhusu kutokuwa na madawa hospitalini, ubovu wa vifaa na kubwa zaidi deni la serikali kwa MSD. Hoja ya kuwa kwanini huduma, madawa na vifaa ni bora kwenye hospitali binafsi naona halina mashiko sana kwani hospitali binafsi. Hospitali za serikali nyingi hazijiendeshi kibiashara ndio maana zinategemea ruzuku ya serikali. Kwa maana hiyo serikali ikishindwa kupeleka ruzuku ama kwa wakati ama kidogo au isipeleke kabisa unategemea huduma zitakuwa na hali gani?

Pia, sote tunakumbuka kuhusu madai ya madaktari walipogoma (kumbuka akina Dr. Ulimboka) pamoja na mambo mengine madai yao yalikuwa kuitaka serikali kuboresha mazingira yao ya kazi vikiwemo vitendea kazi kama vifaa tiba (vifaa tiba ni pamoja na mashine kama CT Scan, MRI, nk). Tuliwabeza, tuliwalaumu na kuwadhihaki. Na walikuwa wanasema hawajisikii vizuri wanapokutana na mgonjwa na kutakiwa kumwelekeza kwenda hospitali binafsi kutokana na ama vifaa vyao kuwa vibovu ama kutokuwepo kabisa. Tuyatazame haya kwa mapana yake. Bahati mbaya wanaofukuzwa huwa hawana nafasi ya kujitetea.

Tushishangae kuona Mganga Mkuu wa Hospitali akifukuzwa kwa wagonjwa kulala chini ama kutokuwa na dawa. Hili litakuwa ni kosa la hospitali husika ama serikali hususan Wizara ya Afya na Hazina? Binafsi nayaona matatizo haya kwa mtizamo huo.

Katika jambo hili tuangalie mfumo mzima kuanzia utendaji kazi na uwezeshwaji wa MSD, bureaucracy za wizara ya Afya na Hazina kabla ya kuwasuta watendaji wa chini.
 
Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL] basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL]

Naungana na wewe mkuu, Watendaji wakuu wa Taasisina mashirika wanapaswa kupiga kerere kwenye critical issues kama hizi na si kuishia kusema, hata wizarani wanajua!
 
mkuu na mganga mkuu pia!! huyu aliyepo ni mpole sana alafu pia sidhani kama ni MD ... nadhani ni "AMO"

Nafikiri ni 'system' nzima kuanzia huko juu mpaka kumfikia huyo mganga. Mganga nae aamshwe, 'upole' wake usituharibie utaratibu.
 
Nakubaliana na uchambuzi wako, na kwa kuwa mkurugenzi naye ni sehemu ya tatizo, basi acha atangulie. Na kama malengo ni kufika mwisho, basi 'kundi' lote nalo liangaliwe kwa darubini, na wenye shida wapishe pia.

Na kama hili litawezekana kwa wizara zote, duuh....miaka 10 ijayo labda tutakuwa mahali. Manake hizi wizara Mungu atusaidie tu, yaani kitu ambacho kingeweza kufanyiwa kazi kwa siku moja kinaburuuuuzwa miezi...zinabaki kalenda tu...njoo kesho...keshokutwa....
 
Hivi wewe njiwa ule mgomo wa madaktari uliosbabisha vifov yya wananchi wasio na hatia ulikuwemo au hukuwemo?

sikuwa tanzania kipindi hicho... nilikuja MNH 2013 nkafanya kazi mwaka nkaona mazingira hayanirihusu na ni magumu vitendea kazi hakuna , mgonjwa anakufa sababu dawa ambayo ina 3000 nje.... nkaona isiwe shida nkaondoka bongo tena ..

magufuli akirekebisha tunaweza kurudi
 
Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL] basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=HAPAKAZITU]#HAPAKAZITU [/URL]

Safi sana bro. well written. Itamsaidia rais awashughulikie na hao wengine waliojificha.
 
Nakubaliana na uchambuzi wako, na kwa kuwa mkurugenzi naye ni sehemu ya tatizo, basi acha atangulie. Na kama malengo ni kufika mwisho, basi 'kundi' lote nalo liangaliwe kwa darubini, na wenye shida wapishe pia.

Na kama hili litawezekana kwa wizara zote, duuh....miaka 10 ijayo labda tutakuwa mahali. Manake hizi wizara Mungu atusaidie tu, yaani kitu ambacho kingeweza kufanyiwa kazi kwa siku moja kinaburuuuuzwa miezi...zinabaki kalenda tu...njoo kesho...keshokutwa....

Dina, kuna kipindi maji dar yalikatika mji mzima, waziri alivyoenda wizarani akaambiwa mfumo mzima umeoza hivyo yanatakiwa mabomba mapya, alivyotoka hapo akaenda ruvu kwenye pampu akamkuta mhudumu alivyomuuliza akaambiwa switch ya kuwashia pampu mbovu wameagiza dar, akamchukua yule mhudumu hadi dukani yule waziri akanunua kwa pesa yake wakaja wakafunga maji yakaanza kutoka mji mzima.

Alichofanya magufuli ni poa tu, tena alivyokaribia getini alivua tai akakunja na shati nadhani lengo lake lilikuwa kupigana na huyo jamaa, basi tu hakumkuta na inawezekana alijua kimenuka akasepa mapema.
 
sikuwa tanzania kipindi hicho... nilikuja MNH 2013 nkafanya kazi mwaka nkaona mazingira hayanirihusu na ni magumu vitendea kazi hakuna , mgonjwa anakufa sababu dawa ambayo ina 3000 nje.... nkaona isiwe shida nkaondoka bongo tena ..

magufuli akirekebisha tunaweza kurudi
usirudi bado rama hajastaafu.
 
Dina, kuna kipindi maji dar yalikatika mji mzima, waziri alivyoenda wizarani akaambiwa mfumo mzima umeoza hivyo yanatakiwa mabomba mapya, alivyotoka hapo akaenda ruvu kwenye pampu akamkuta mhudumu alivyomuuliza akaambiwa switch ya kuwashia pampu mbovu wameagiza dar, akamchukua yule mhudumu hadi dukani yule waziri akanunua kwa pesa yake wakaja wakafunga maji yakaanza kutoka mji mzima.

Alichofanya magufuli ni poa tu, tena alivyokaribia getini alivua tai akakunja na shati nadhani lengo lake lilikuwa kupigana na huyo jamaa, basi tu hakumkuta na inawezekana alijua kimenuka akasepa mapema.

Unaona sasa...Na wa hivi wako wengi mno....
 
Ila jamani vitu vingine tuviangalie kwa jicho la kawaida tu. Haya wewe mkuu wa MNH, unajua kabisa mashine zako hazifanyi kazi, inatosha tu kusema nimeshatoa taarifa wizarani wanashughulikia? Haya kama ni wa wizarani, kitu kiko mezani kwako, miezi miwili una taarifa mashine imekufa, halafu? Kwa hiyo basi? What is the point ya kutupita barabarani mbio tena wakati mwingine tunawapisha ili muwahi kazini...hasa huwa mnawahi wapi?
 
I can see your point.Kwa hili la Muhimbili alitakiwa kufumua mfumo wote wa uwajibikaji na nadhani ile ilikuwa hatua ya awali.I believe wote waliohusika watachukuliwa hatua.
Badilisha mfumo, badilisha timu inayoendesha huo mfumo kama haifanyi kazi vizuri - siyo mtu mmoja mmoja. Hiki ndicho Magufuli anapaswa kufanya. Hii kuibukia shirika moja moja, then kutimua bosi mmoja/wawili wa shrika wakati sote tunafahamu kuwa maamuzi ya serikali yamekuwa yanaenda kwa ngazi huku yakihusisha wengi na teuzi nyingi za hao 'wabovu' zikianzia hukohuko ikulu, is a political stunt to say the least and won't get us very far. Naunga mkono nia ya Magufuli lakini naona kama strategy bado ni tatizo.
 
Tatizo ni pale kiongozi unapokosa maono. Naomba kukuuliza maswali yafuatayo:-

1. Muhimbili inakusanya shs ngapi kwa mwaka??
2. Muhimbili inategemea rukuzu kiasi gani kutoka serikalini?
3. Muhimbili ina vitegauchumi vingapi nje ya malipo ya wagonjwa na vipimo?
4. Udhibiti wa kukusanya mapato ya Muhimbili ukoje? Je mianya ya wizi na upotevu wa fedha imezibwa vizuri?
5. Mtiririko wa matumizi ukoje?
6. Weka hapa taarifa ya fedha ya Muhimbili (mapato na matumizi) wadau waijadili hasa vipaumbele Kama hospital ya Taifa
7. Je umeridhika na huduma inayotolewa Muhimbili (customer service)
8. Kwanini hospital Kama regency ambayo haina ruzuku inapanuka kila siku
9. Tatizo ni mfumo hilo halina ubishi. Ila lazima kuwe na pa kuanzia. Je huoni viongozi wengine wameamka baada ya kuona mambo yako serious na uwajibikaji unarudi serikalini.

Tusidharau hatua hii hata Kama hatumpendi muhusika. Ili mfumo upitiwe lazima watu na positions ziguswe.

Queen Esther

Nakuunga mkono mkuu. Wachangiaji wengi humu siyo wachambuzi wa mambo. Tatizo kubwa linaloikumba Serikali kwa sasa ni ya kibajeti. Taasisi nyingi zipo hoi kifedha. Ukifuatilia flow ya fedha kutoka Hazina kwenda kwny taasisi ndipo utagundua tatizo lipo wapi. Tulikuwa busy na kampeni hatukuwa tunafuatilia kinachoendelea. Hazina nao sijui walitudanganya kuhusu vyanzo vya mapato, sijui. Ila la msingi ni kwamba baada ya Bunge kumalizika Hazina waliziandikia Wizara zote kuwa bajeti iliyopitishwa haikuwa inatekelezeka hivyo wizara zitapewa 60%. Hivyo, kulikuwa na bajeti cut ya 40%. Hili wananchi wa kawaida hawalifahamu.

Binafsi naona watendaji wanaweza kuonewa sana huku tatizo la msingi likiwa halisemwi.
 
Ushauri tunauchukua yote yako mbioni kwisha lazima watu watolewe kafara ili yaibuke Mengi ambayo nayo ni uozo!
 
umenikumbusha 2013 wakati nipo MNH hakuna diclofenac twaambia wagonjwa wakanunue nje.. hali ile mi ilinikera sababu wagonjwa wa idara yangu wanahitaji sana dawa za maumivu.. nkamuuliza intern pharmasist mmoja akanambia ... muhimbili inatakiwa ichukue dawa kwa supplier flani nimesahahu nadhani ni MSD na si kwengineko na kama hawana ndio imekula kwetu , na pia kulikuwa na Tatizo hospitali inadaiwa... supplier amesitisha zoezi la kuleta dawa...

hii mikataba huwa watu wanaingia huku wakipewa pesa ndio maana wanaingia mikataba mibovu!!,....

mwisho wa siku tunakuja kupata lawama madactari tunabania dawa,, tuna maduka nje ..... makatili mgonjwa ana maumivu hatuwapi dawa.... et cal

kwa utawala huu wa awamu ya 5 mambo yatabadilika i hope Insha Allah

Wewe nawe ni Dr ?!?!?!!?!?!?!!!!!
Maajabu ya Ulimwengu haya
 
Mkurugenzi wa MNH angewezaje kwenda IKULU tena ya Kikwete kuishtaki Wizara yake? Kesho yake angepata uhamisho Lindi. Naamini alipeleka taarifa kwenye Bodi ambao nfio wangelifikisha kwanza Wizarani, kama halikutatuliwa wangepeleka IKULU. Dr Magufuli hawezi kutatua matatizo yaliyolimbikizwa na mtangulizi wake, tayari kuna tafiti ya kero zote, aunde Baraza Lake la Mawaziri, aingie nao mkataba na utendaji kazi uanzie chini kuja juu, apate weekly report. Atuzungukia taasisi ngapi nchi nzima?
 
Hii mada ni habari njema sana kwetu Watanzania. For a change, naona mjadala ukiainisha matatizo lukuki ya sekta ya afya. Enzi zile akina Ulimboka na wanaharakati wengine wakipigania matatizo hayo yashughulikiwe waligeuzwa kuwa "mashetani" wasioitakia mema nchi yetu na serikali "inayofanya vizuri" kuimarisha huduma za afya!

This is a turn for the best. Shukran mleta mada. Tuendelee, positively ...
 
Back
Top Bottom