Uboreshaji wa makazi bora Mijini na Vijijini

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
Kabla sijafika miji mikongwe kama Bagamoyo nilijua ni miji ya kuvutia kwa makazi yaliyoboreshwa kumbe nilikuwa najidaganya.

Tuongelee mji wa Bagamoyo na makazi yake, yaani wingi wa nyumba za udongo na kuridhika kwa wakazi wazawa wa hapo kwenye huo mji.

Mji wa Bagamoyo una jina kubwa lakini makazi yake yatakushangaza, nyumba za udongo katikati ya mji. Athali za kuacha makazi duni ya namna hii mijini na kwenye majiji tegemea miji hiyo kukumbwa na;

  1. Ongezeko la vijana wabakaji na walawiti
  2. Ongezeko la wezi na vibaka na ndio maana nyumba nyingi huku madirisha yamechanwa na wezi
  3. Kupanda kwa bei za bidhaa kwa maana nyumba hizo duni zinabeba idadi kubwa ya watu ambao kama normal human wanaitaji ku consume
  4. Ongezeko la vingoma vya vigodoro na baikoko ambavyo vinaharibu maadili kwa kasi ya 5G
  5. Vijana kutopenda kufanya kazi za uzalishaji, wameridhika kwamba wanasehemu za kulala, nyumba hizo duni wanahisi ndio tumaini lao kubaki mjini hivyo ikitokea mtu anataka kununua nyumba hizo duni ili kuweka makazi bora atapigea bei ya kushangaza kama ananunua ghorofa mbezi.
Serikali ikiendelea kuuacha makazi duni kushamili mjini jua madhara hayo hapo juu yanaikumba nchi kwa kasi sana. Tatizo kubwa litakuwa Kutokushuka kwa bei ya bidhaa: INFLATION, INFLATION, INFLATION.
Serikali haijaweka jitihada ya kupambana na inflation kwa sababu nadhani bado hawajajua msingi wa inflation kwa nchi hizi zinazoendelea uko wapi.

Mfumuko wa bei unawaathili sana watanzania kwa maana Pesa haikai, ukishachenji shs 10000 tu sekunde sifuri huna tena hiyo pesa.

Watu tunasahau kwamba msingi wa Inflation Kwa Tanzania upo kwenye kipengele cha MAITAJI (AGGREGATE DEMAND) kuwa makubwa kuliko uwezo wetu wa UZALISHAJI (AGGREGATE SUPPLY) kwa sababu nchi yetu ilishaachana na sera ya KILIMO KWANZA KWA UFANISI. Nchi zote duniani zilizoendelea zilianzia kitu kinaitwa MAPINDUZI YA KIJANI AU KILIMO ( AGRARIAN REVOLUTION).

Utoshelevu wa chakula ndicho kitu cha kwanza kuonesha muelekeo wa nchi katika kudhibiti mfumko wa bei.

Nataka kusema nini, Serikali kwa sababu now imejitaidi kuboresha mazingira ya vijiji vingi Tanzania kwa maana now ni rahisi kukuta vituo vya afya vijijini, upatikanaji wa maji vijijini, uwepo wa barabara na shule vijijini.

sasa kinachotakiwa kufanywa na serikali yetu ni kuanza na sera ya KILIMO KWANZA kwa kuondoa NGUVU KAZI INAYODHULULA HUKU MIJINI na JIJINI kwenye makazi duni wauze nyumba zao hizo duni hapo mjini KWA LAZIMA na warudi vijijini kuwahi mashamba na nyumba za kuishi kwa levo yao.

Hii sio kwa lengo baya wala kudhalilisha utu wa mtu, ifikie wakati kama familia zetu haziwezi kuwa na makazi bora mijini tuondoke turudi vijijini kuongeza thamani ya kilimo chetu.

Sasa kitakocho fanyika ni Serikali kutangaza mara moja hadi kufikia kwa mfano tarehe 30/05/2024 NYUMBA YOYOTE YA UDONGO ISIWEPO MJINI KWENYE HALIMASHAURI YOYOTE ILE TANZANIA.

KWENYE MANISIPAHA NA MAJIJI KUSIWEPO NA CHUMBA AMBAYO BATI LINA KUTU Wala haijapigwa rangi, wewe ukitaka ubaki mjini piga nyumba yako rangi na bati lipige rangi.

Hii itasaidia watu kuboresha makazi yao mjini na vijijini huku kwa kiasi kikubwa tukiweza kudhibiti mfumuko wa bei, ushoga unaokithiri mijini, wezi na vibaka wote wataondoka mjini na mengine mengi mazuri kote kote mjini na vijijini.
 
Wazo lako liko kinadharia zaidi kuliko uhalisia. Unadhani kila mwenye nyumba iliyochakaa mjini ana makazi na huko vijijini? Huko vijijini watu wataenda wenyewe iwapo kilimo au shughuli yoyote ya uzalishaji italipa. Mfano hapa mjini watu walikuja wenyewe bila kulazimishwa. Maeneo ya migodi watu hufurika wenyewe bila kulazimishwa.

Ushauri serikali ipeleke miradi ya uzalishaji huko vijijini, watu wataenda wenyewe bila shuruti na sio kwa haya matamanio yako. Au kama vipi ww binafsi kafungue shughuli ya uzalishaji huko vijijini kama hujaona watu wamekuja wenyewe.
 
Wazo lako liko kinadharia zaidi kuliko uhalisia. Unadhani kila mwenye nyumba iliyochakaa mjini ana makazi na huko vijijini? Huko vijijini watu wataenda wenyewe iwapo kilimo au shughuli yoyote ya uzalishaji italipa. Mfano hapa mjini watu walikuja wenyewe bila kulazimishwa. Maeneo ya migodi watu hufurika wenyewe bila kulazimishwa.

Ushauri serikali ipeleke miradi ya uzalishaji huko vijijini, watu wataenda wenyewe bila shuruti na sio kwa haya matamanio yako. Au kama vipi ww binafsi kafungue shughuli ya uzalishaji huko vijijini kama hujaona watu wamekuja wenyewe.
Wazo zuri
 
Umeandika vizuri lakini ulipoanza sera za kulazimishana kuuza nyumba au kubomoa nyumba za watu kwa sababu ni za udongo au hazina bati, nimekuona huna akili na unaonekana unaweza kuchafua hali ya hewa kwa ukosefu wako wa akili
 
Back
Top Bottom