MWENDAKULIMA
JF-Expert Member
- Jul 17, 2009
- 952
- 354
Bwana Mwendakulima, nina mashaka juu ya uwezo wako wa analysis. Sijui hata kama unaelewa maana ya rapid transformation from IDM to Mzumbe University na pia inaonekana umesikia ju ju kuhusu transformation lakini hujui transformation process ya IDM ilianza lini. Unaongelea suala la MA na PhDs ambalo unaonekana kuwa less informed. Kwanza unaonekana umekariri, Mzumbe University hakuna MA programme yoyote hadi leo hii. Kama una maana ya masters programmes basi hebu tukusaidie. Masters programmes zinazotolewa Mzumbe ni MPA, MBA, na MSc. Probably MA is in the pipeline to be offered in the future but currently not offered. Lakini unaonekana hujui historia ya Mzumbe katika kutoa programmes za masters ilianza lini. Ni kama vile unadhani masters programmes zimeanza kutolewa na Mzumbe University mwaka 2002. Ukweli ni kwamba masters programmes zilianza kutolewa tangu mwaka 1989 by defunct IDM. Naamini huu ni wakati ambao hata ulikuwa hujui kinachoendela katika masuala ya elimu Tanzania. PhD zimeanza kutolewa mwaka 2005/2006. Mwanafunzi wa kwanza kutunukiwa PhD ni Dr. Eleuter Mushi (2009) ambaye sasa ni Mhadhiri Mzumbe, wa pili ni Dr. Modesta Opiyo na orodha imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Mwaka 2011, Chuo kiliwatunuku PhD wahitimu 7 akiwemo Dr. Emmanuel Nchimbi, wengine ni wahadhiri kutoka hapa nchini na moja toka Nigeria. Swali langu ni je, Mwanasiasa John Pombe Magufuli na John Ndunguru wakitunukiwa PhD na UDSM hakuna shida, ila Emmanuel Nchimbi akitunukikwa PhD Mzumbe basi kuna shida na kelele nyingi. (You seem to have prejudice in this matter). Do you want to force everyone to go to UDSM?, people must have choice and for them Mzumbe is their choice and above all external examiners wa Mzumbe University ni hao hao Professors wa UDSM na kwenye Viva Voce Examinations wanaalikwa na kutoa comments sasa hizo quality assurance zenye shida ni zipi? Je hao wanasiasa ambao leo hii wameshaonekana ni wengi ni akina nani zaidi ya Nchimbi na Kamala? Kwa nini hakuna aliyeenda mahakamani kuomba mahakama itengue uhalali wa PhD zao?
Ni haki kuwa na wasiwasi mkuu, naomba nikutoe wasiwasi kuhusu uelewa wangu na uwezo wangu wa analysis. Nimeandika maneno machache sana (ukilinganisha na huo mkeka wako) tena very shallow kuonesha wasiwasi wangu kuhusu hicho kinachoitwa Mzumbe University,ni wajibu wako wewe mtaalam kunitoa huo wasiwasi kwa maelezo mujarab siyo kuanza kunishambulia. ukisoma kwa umakini sikuandika popote kuhusu kuwashawishi watu waende UDSM,ukisoma vizuri utagundua hata hiyo UDSM nimeonesha ina tatizo (changamoto?) sugu ya human resource pamoja na kuwa ndiyo University kongwe zaidi ya umma hapa nchini. Mkuu ule mjadala wa mafisadi wa elimu ulikupita kando?maana usingediriki kuwatetea hao wanasiasa wako uliowataja. Nahitaji ufafanuzi wako hapo kwenye red tafadhali