Ubinafsi ndio unaowafanya watu wanaoana

Ubinafsi ndio unaowafanya watu wanaoana

KikulachoChako
Umenena sahihi lakini kwa hawa binadamu wa sasa.
Wanawake wanapenda mali, wanaume twapenda uzuri wa mke, hapo kiasi fulani ni ngumu kujua upi upendo wa kweli, ila tukimhusisha Mungu hakika tutafika
 
Last edited by a moderator:
KikulachoChako
Umenena sahihi lakini kwa hawa binadamu wa sasa.
Wanawake wanapenda mali, wanaume twapenda uzuri wa mke, hapo kiasi fulani ni ngumu kujua upi upendo wa kweli, ila tukimhusisha Mungu hakika tutafika

Kweli mkuu....
 
Last edited by a moderator:
Word mkuuu,ilaaaaaa,kwa hyo ulitaka nioe chizi ili nisionekane mbinafsi kwa jinsi unavyofikiria???
 
sio ubinafsi unafanya watu waoane. Wengi wanapenda kutimiziana furaha, na ndio maana hata akimwona mpenzi wake anahuzuni au shida fulani naye lazima ajisikie vibaya. Hakuna ubinafsi hapo mkuu.

Unatimiza furaha yako ya kujisikia vizuri na sio furaha ya mwingine

Hata huyo anaejisikia vibaya ni kwasababu mtu anaemfanya ajisikie vizuri anahuzuni hivyo anajitahidi arudi kwenye mood ili apate kile anachokitarahia kwa mhusika

Ni sawa na wewe gari lako lipate hitilafu,unahuzunika sio kwasababu unalipenda sana bali kwasababu linakupeleka kila.unapotaka na kama litashindwa kufanya hivyo utaachana nalo

Ndio maana mpenzi au mkeo akianza kuwa na kisirani utamuacha kwasababu ile furaha aliyokuwa anakupa inakuwa haipo tena,yaani sababu iliyokufanya ukamuoa inakosekana na anakosa thamani

Ubinafsi huo...!!
 
Ndoa ni muunganiko wenye kuleta furaha katika kipindi cha maisha yao yote kwa wale ambao wameunganishwa na upendo wa dhati kutoka ndani ya nyoyo zao...upendo ambao unawafanya watu wawe mwili mmoja katika kila hali..hapa namaanisha kwenye shida na raha....siku zote ni raha kuwa na umpendae na ni jambo lenye kuzijaza nyoyo zetu furaha na raha wakati wote...machungu ya ndoa yanaanzia pale unafiki unaoingia ndani yake...ninasema unafiki kwa kuwa si kila mwanandoa huwa anaingia ndoani kwa sababu ya upendo bali wengine hufuata mali na vitu vingine vya kupendeza machoni lakini sio rohoni.....matokeo yake ndio huzaa majuto ndani ya ndoa na kuzaa falsafa kuwa ndoa ni gereza la mateso ilihali maana halisi ya ndoa haiko hivyo.....tunapochagua wenzi wa maisha tujitahidi kuzipa nafasi nyoyo zetu ziamue...kwani upendo wa kweli hutoka mioyoni mwetu na sio mifukoni mwa mwetu au mwa mtu....na kipimo cha upendo usiwe mali bali matendo ya yule anayedai anakupenda kwani MUNGU hajawahi kumficha mnafiki....
Umesoma nikichoandika?
 
Love nilishawahi ku define ni superiority complex of ones feelings over someone ,hapa definition yng nahisi inahusika
 
umefanya utafiti au umeandika! tu maana sioni mashiko kwa unayozungumza tafta maana ya ndoa then linganisha na huo ubinafsi wako tena uangalia katika angle tofauti nadhani utapata majibu la sivyo sio utagwaya sana

Ni Mtazamo tu
 
May be it's true, too philosophical for the simple mind to understand this.
 
Thread imekaa poa sana hii ila kuilewa inabidi utafakari kidogo
 
Najaribu kuhusisha mada yako Eiyer na mtazamo wa Sigmund Freud ktk saiko changanuzi, kuna kitu nakipata kuwa,, ubinafsi ni asili ya mwanadamu (we are born selfish) na ubinafsi huo huo ndio unatusukuma kuelekea matamanio yetu, sio ya kimapenzi tu, bali pia ya kimaendeleo n.k mf ukitazama kwa nini mfumo wa ubepari unazidi kunawiri na ule wa ujamaa unakufa, ni kwa kuwa asili ya ubinafsi ya ndani ya mtu inakubaliana na ile ya nje yake.
Your deadly right.
^^
 
Last edited by a moderator:
Najaribu kuhusisha mada yako Eiyer na mtazamo wa Sigmund Freud ktk saiko changanuzi, kuna kitu nakipata kuwa,, ubinafsi ni asili ya mwanadamu (we are born selfish) na ubinafsi huo huo ndio unatusukuma kuelekea matamanio yetu, sio ya kimapenzi tu, bali pia ya kimaendeleo n.k mf ukitazama kwa nini mfumo wa ubepari unazidi kunawiri na ule wa ujamaa unakufa, ni kwa kuwa asili ya ubinafsi ya ndani ya mtu inakubaliana na ile ya nje yake.
Your deadly right.
^^
Ni kweli kabisa mkuu kwasababu kanuninya utajiri ni ya kibinafsi zaidi na wale ambao sio wabinafsi hawawezi kuwa matajiri kamwe!
 
Last edited by a moderator:
hii kitu sikubaliani nayo kabisa. Kuna watu hasa wanaume ambao anaweza akamuoa msichana fulani kwa ajili yakumfanya huyo girl awe happy and peaceful, kuna mwingine anakuwa na hamu tu kumsaidia fulani katika hali aliyonayo labda ya msongo then katika harakati hizo na mapenzi yanajichanganya mwisho wanaoana.

Mkuu bila Shaka utakuwa hujauzwa mahal au mimi ndo nimechanganya madesa!

Naona huu ndo upendo ambao mkoa mada anaumanisha!! Na ndo upendo wa kweli! Kujitoa kwa ajili ya furaha ya mwingine
 
Back
Top Bottom