Sidhani kama wengi wanaelewa maana ya upendo, mapenzi ya ukweli kabisa ni machache sana, wengi tunasukumwa na ubinafsi, labda uishi tu na mwenza sababu ya upweke, labda watoa msaada, labda umeshinikwa, labda hutaki wanaume wengine wampate huyo mwanamke, labda wataka tu kuzaa naye (maana tunashabiana na wanyama kupenda kuacha mbegu) ila huna jinsi lazima uoe, labda wataka usaidiane na mwenzako kwenye haya maisha magumu..
Tumesoma na kushuhudia wenzetu wazungu wasivyo penda danganya kuhusu swala mapenzi, wanaanza kwa mapenzi moto moto mno, kama kumbikumbi, zile tamaa na hisia au kama msemavyo mapenzi yakipunguwa, kila mtu anashika muda wake, haijalishi wameona au wanamajukumu kimaisha..Naamini ndoa sio lazima mpendane ila ni kama mwaweza kuvumiliana na kuishi pamoja kujenga familia..
Mapenzi ya ukweli labda labda ndio yale wasikia mtu kajinyonga, kauwa, kachanganyikiwa...n.k. n.k. kazi kweli kweli..(ni maoni yangu, sio lazima uyakubali)