Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,709
Siku za hivi karibuni kumekua na migomo ya sekta nyeti sana inayohusu uhai wa bindamu,Udaktri.Wapo waliounga mkono wapo waliopinga migomo hiyo iliyotokea kwa nyakati tofauti.Lakini pia wapo waliounga mkono msimamo wa serikali na wapo waliokosoa,pia wapo waliowaunga mkono madaktari na wapo waliowakosoa. Ni jambo la hatari sana kwa sekta hizi nyeti kusagishana na kushindwa kuiona thamani ya Ubinadamu,wala hili sio jambo la ushabiki.lawama zimetolewa kwa pande zote mbili na wamejitahidi kwa nyakati tofauti kutafuta suluhu na imeshindikana au imepatikana ya muda tu.Kwa nini?ni kwa sababu wanadam au watanzania wote tuna matatizo ya kufanana na hayo yanasababisha yote haya. Juzi kati hapa nilileta thread hapa inayohusu namna watu wanavyochagua wenza wa maisha kwa misingi ya elimu,fedha na muonekano wa nje(sura).Michango mnaijua wenyewe,kuna watu hapa walisema hawawezi kuolewa au kuoa darasa la 7 au asie na hela au muonekano fulani.Hii ina maana kwamba,asiekua na vitu hivyo sio binadamu yuko nusu na hatakiwi kuoa au kuolewa,ili akamilike au awe binadam anatakiwa awe na vitu hivyo.kwa sababu huyu anakua hana sifa za binadamu,ndo maana hata akitoa mawazo yake hayasikilizwi,huyu hana akili wala busara,utamsikilizajaje mtu hajaenda shule?Naam imezuka sintofaham baada ya wenye akili(Madaktari na serkali) kushindwa kuutambua utu na ubinadamu na kusigishana kuhusu pesa.Ubinadamu ukikosa nafasi.watu midomo wazi wenye akili wanashindwa kuliona jambo kama hili. Watu wanajiuluza yanatoka wapi haya?Ukweli ni kwamba mfumo wetu wa malezi umeleta haya.Mfano mdogo ni kwamba mtu unapochagua mwenza kwa kutumia vigezo vya nje kama pesa,elimu,mtu kama huyu lazima mwanae atalelewa kwa misingi hiyo ya kuvithamini vitu hivyo.Familia kama hii haiwezi kuitambua thamani ya ubinadamu.Watoto hawa watawathaminisha binadamu wenzao kwa namna ya wazazi wao,yaani kama huna hela na elimu kwao wewe sio binadamu. Serikali yetu na madaktari ni matokeo ya familia za namna hii.Ni jambo gumu sana kuacha watu wafe kwa sababu haulipwi vyema,pia ni jambo gumu zaidi kuacha kutambua thamani ya mdaktari ukaacha kuwalipa vyeme na ukajilipa wewe vizuri,haya yote mawili ni unyama na malezi yako lazima yatakua na matatizo.Tunatakiwa tutambue kuwa ubinadamu ni zaida ya fedha,lakini hili haliji hivihivi tu linatoka kwenye malezi yete.Naam ubinadam haupo na umetushinda.Mtoto akifeli mtihani au akitoka familia maskini anaonekana thamani yake haina tofauti na kondoo.