Uber Tanzania: Support thread

Oct 25, 2012
67
53
Kwa maswali, changamoto, habari na taarifa kuhusu huduma kwa wote wasafiri na madereva,
karibuni....JINSI YA KUTENGENEZA HELA UKIWA NA UBER KAMA DREVA AU UBER PARTNER

1. JISAJILI KUWA UBER PARTNER
2. UTAPATA REFERRAL CODE, TUMIA HIYO REFERRAL CODE KUSAJILI MADEREVA WENZIO NA UTAPATA KIASI CHA 100,000TZS [BADALA YA 50,000 YA HAPO MWANZO] KWA KILA DREVA ULIYEMSAJILI AKIMALIZA TRIP 5 BADALA YA 20 ZA HAPO MWANZO [NEW]UPDATES:
1. Tuna habari njema na kubwa kabisa kwako usiku wa leo!! Kuanzia usiku wa leo, tutaleta huduma itakayoruhusu kuongezeka kwa gharama maeneo yenye uhitaji mkubwa wa matumizi ya Uber.Haya maeneo yatakuwa yakionekana kwa rangi katika ramani ambapo rangi nyekundu itaashiria maeneo yenye uhitaji mkubwa wa matumizi ya Uber. Kama utapokea ombi la kutoka kwenye moja kati ya haya maeneo ya rangi, kifaa chako cha Uber kitaonesha namna ambavyo ongezeko la gharama litakavyokuwa. Kwa mfano, kama utapokea ombi kwenye eneo ambalo gharama inaongezeka kwa mara 1.5 ya gharama, basi gharama ya safari ya TSH 10,000 itakuwa TSH 15,000. Tunategemea kukuona barabarani.

2. Uber Imefungua garantii yenye nguvu zaidi! Kuanzia wiki hii, ili kufuzu na kupata kipato kutoka Uber kwa malipo ya wiki, basi unapaswa kuhakikisha una kamilisha japo trip 1 kila lisaa ambalo utakua online (hewani). Kwa kila lisaa ambalo utakua online (hewani) na kukamilisha angalau trip 1, utafuzu hakikisho letu au garantii ya kwamba utapata Tsh 6,500. Kama mfano, ukiendesha masaa 50 kwenye wiki na kukamilisha angalau trip 50 au zaidi, utapokea kiasi cha Tsh 325,000 za fedha za uhakika (garantii) kutoka kwa Uber baada ya makato yote ya Uber. Kama utatengeneza fedha pungufu na kiwango cha garantii, Uber wataongezea tofauti hiyo kwenye akaunti yako ya benki Alhamisi. Kumbuka kuzingatii masaa ya garantii ni Jumapili- Alhamisi saa KUMI NA MBILI ASUBUHI mpaka saa SITA USIKU na siku za wikendi ni IJumaa- Jumamosi kuanzia saa KUMI NA MBILI ASUBUBI mpaka SAA TISA ALFAJIRI. Tafadhali zingatia masaa haya na utengeneze kipato kizuri. Uber!!

Kama ni dreva na hujajiunga na Uber bofya link hii ujiunge
t.uber.com/get
 
Natumia sana Uber.. Huduma nzuri ila bado sana hamjatoa elimu ya kitosha ili madereva wengi wajiunge..
 
Kama mimi nahitaji kukodisha hizo gari,na niko kwangu nyumbani,nitaweza kuzipata kwa mawasiliano ya kivipi?
 
Ukitaka kutumia usafiri wa dreva au gari zilizojiunga na Uber unachohitaji ni
1. Kudownload app ya Uber kwny plasytore
2. Kujisajili kupitia app
3. Kuomba huduma kupitia app hapo nyumbani kwako na dreva aliye karib yako atapata ombi lako na kuja kukuhudumia
 
Hiyo app,ni ipi maana nimeandika ubber,zimekuja app,nyingi na nimedownload moja,hiyo inavyoonyesha ni kama ya mwenye gari sio ya mteja anayetaka gari.
 
Asante sana,nimesha download app.,ila sijafahamu jinsi ya kuifahamisha taxi niko wapi na Nina mhitaji aje anifuate nilipo
 
Ukilaunch app yako juu kabisa kuna kibox kimeandikwa pic up a location, hapo andika eneo ulilopo, Google map itakusaidia kutambua eneo lako wakati unaandika, then bofya chini button nyeusi imeandikwa REQUEST UBERX
 
Hongera wakubwa..labda baadae mnaweza mka expand services... Mkaanza kupiga routes ndefu mkikaa pale ubungo kuna wanaoachwa na ma basi, mnaweza mkachukua wajipange labda watatu au wanne muwapeleke mikoani...
Zingatieni usalama lakini....
 
UBER mna baadhi ya madereva ni vichaa, wanafoka foka njia nzima. Hao mnawafanyaje? kuna mmoja kidogo nimtwange makof jana analalama njia nzima.
Ikitokea hujaridhika na huduma dereva aliyokupa, unapokuwa una rate safari andika na maoni yako, aidha unaweza kuchagua safari katika sehem ya app yako inayoonesha safari zote ulizowahi kufanya na ukaandika maoni yako juu ya huyo dereva. Maoni yote yanachunguzwa kabla ya hatua stahiki kuchukuliwa
 
Achaneni na hayo mambo ya kukodi kwa kutumia App.Wekeni namba za simu kwa kila locations. Mfano nipo Tandale napiga simu gari ya uber iliyopo karibu na Tandale.Hayo ma App yenu ni wachache wenye smartphone.
 
Kwa maswali, changamoto, habari na taarifa kuhusu huduma kwa wote wasafiri na madereva,
karibuni....JINSI YA KUTENGENEZA HELA UKIWA NA UBER KAMA DREVA AU UBER PARTNER

1. JISAJILI KUWA UBER PARTNER
2. UTAPATA REFERRAL CODE, TUMIA HIYO REFERRAL CODE KUSAJILI MADEREVA WENZIO NA UTAPATA KIASI CHA 100,000TZS [BADALA YA 50,000 YA HAPO MWANZO] KWA KILA DREVA ULIYEMSAJILI AKIMALIZA TRIP 5 BADALA YA 20 ZA HAPO MWANZO [NEW]UPDATES:
1. Tuna habari njema na kubwa kabisa kwako usiku wa leo!! Kuanzia usiku wa leo, tutaleta huduma itakayoruhusu kuongezeka kwa gharama maeneo yenye uhitaji mkubwa wa matumizi ya Uber.Haya maeneo yatakuwa yakionekana kwa rangi katika ramani ambapo rangi nyekundu itaashiria maeneo yenye uhitaji mkubwa wa matumizi ya Uber. Kama utapokea ombi la kutoka kwenye moja kati ya haya maeneo ya rangi, kifaa chako cha Uber kitaonesha namna ambavyo ongezeko la gharama litakavyokuwa. Kwa mfano, kama utapokea ombi kwenye eneo ambalo gharama inaongezeka kwa mara 1.5 ya gharama, basi gharama ya safari ya TSH 10,000 itakuwa TSH 15,000. Tunategemea kukuona barabarani.

2. Uber Imefungua garantii yenye nguvu zaidi! Kuanzia wiki hii, ili kufuzu na kupata kipato kutoka Uber kwa malipo ya wiki, basi unapaswa kuhakikisha una kamilisha japo trip 1 kila lisaa ambalo utakua online (hewani). Kwa kila lisaa ambalo utakua online (hewani) na kukamilisha angalau trip 1, utafuzu hakikisho letu au garantii ya kwamba utapata Tsh 6,500. Kama mfano, ukiendesha masaa 50 kwenye wiki na kukamilisha angalau trip 50 au zaidi, utapokea kiasi cha Tsh 325,000 za fedha za uhakika (garantii) kutoka kwa Uber baada ya makato yote ya Uber. Kama utatengeneza fedha pungufu na kiwango cha garantii, Uber wataongezea tofauti hiyo kwenye akaunti yako ya benki Alhamisi. Kumbuka kuzingatii masaa ya garantii ni Jumapili- Alhamisi saa KUMI NA MBILI ASUBUHI mpaka saa SITA USIKU na siku za wikendi ni IJumaa- Jumamosi kuanzia saa KUMI NA MBILI ASUBUBI mpaka SAA TISA ALFAJIRI. Tafadhali zingatia masaa haya na utengeneze kipato kizuri. Uber!!

Kama ni dreva na hujajiunga na Uber bofya link hii ujiunge
t.uber.com/get
Mkuu habari za muda
unaweza nipatia mawasiliano yenu kwa hapa Tanzania, maana 0759842044 haipatikani...., thanks.
 
Majuzi tu nimelipa 6,000 zaidi sababu Ya uzembe wa dereva wenu
Nimetuma several emails kucomplain so far no response
....uswahili ushawaingia nyie Uber
Mnakera
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom