Ubepari: Suluhisho la Matatizo yetu!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Ndiyo Mchungaji kakulia kwenye Ujamaa, kalewa mvinyo wa Nyerere na Azimio la Arusha, anapenda haki sawa kwa wananchi.

Lakini leo Mchungaji anasema "Ubepari" ndio suluhisho la matatizo yetu.

Ubepari wa Mchungaji ni ule wa kumuwezesha mzawa awe bwanyenye, tajiri, kabaila na mwenye mali, alimradi kila kitu ni halali.

Ubepari wa Mchungaji ni ule ambao unasema Serikali kazi yake ni kutunga sheria, ,kusimamia sheria na udhibiti wa kanuni na kujenga misingi imara ya kuwezesha uzalishaji mali, misingi kama Barabara, Maji, Reli, Mtandao wa Umeme, Simu na kisha kuachia sekta binafsi iendeshe shughuli za kila siku na Serikali ikinge mikono kupata kodi na pato lake!

Ubepari wa Mchungaji ni ule wa kumtaka kila mtu aanze kuchangia huduma na kulipa kodi. Bure imefika tamati, ni buriani bin hayati, hatuwezi kuendelea kudai tu-masikini, maana tunalelea umasikini kwa kuendekeza jamii isiyotaka ondokana na umasikini!

Ubepari wa Mchungaji ni ule wa Mtanzania mbunifu na mchapa kazi ambaye atatumia njia na mifumo halali bila kupita njia fupi kujijenga kiuchumi na ni ruksa kuwa nyapara na kuajiri wenzake wasiotaka kujituma!

Tukisha anza kujijenga kama mabepari, kila mtu atachangia uzalishaji mali na tutaanza kupiga hatua za maendeleo tukiwa huru wa utegemezi wa Serikali na misaada kutoka nje.

Kwa upande wa pili wa Ubepari wa Soko Huria, Mchungaji anasema, nafasi ya kwanza ni kuhamasisha wazawa na uzalishaji wa mali wa ndani, iwe ni viwanda, kilimo, madini na huduma. Misingi imara ya uzalishaji iwekwe ili wazawa wapate fursa ya kushindana na wawekezaji kutoka nje.

Mwisho, kwenye Ubepari wa Mchungaji, Serikali inakuwa wabanifu wa matumizi na si Pedeje wa kuzimwaga hovyo hovyo!

Heri ya 2009!
 
Last edited:
Ubepari wa Mchungaji unasemaje kuhusu Elimu kwa wote? Wale wasio na uwezo wa kulipa ada zao wenyewe walipiwe na sisi sote au waachwe tu? Vyuo vikuu wasome watoto wa matajiri tu au tufanyeje?

Kijumla, Ubepari wa Mchungaji unasemaje kuhusu user-pay policy? Huduma za hospitali kwa wale wasio na uwezo (na ni wengi kweli kweli) ziweje?

Mchungaji ajibu hoja.
 
Mawazo yako mazuri, lakini i wish kungekuwa na fomula rahisi kama hiyo.

Sio ngumu kumpata mjamaa ambaye naye atasema ujamaa ndio suluhisho, na akatoa arguments nzuri tu. Wote mtakuwa sawa, lakini ukweli ni kwamba suluhisho ni complex kuliko tu kutumia ujamaa au kutumia ubepari.

Pengine si sawa kusema ubepari ni suluhisho kwa sababu tu umejaribu ujamaa ikashindikana. Na vile vile pengine si sawa mtu akisema ujamaa ni suluhisho kwa sababu kuna sehemu anaona umefanya kazi.

Kila tatizo linasuluhisho lake kuendana na aina ya tatizo na mazingira yake.

Kuna mazingira ambamo ubepari utafanya kazi vizuri, na mazingira ambamo utakuwa ni disaster. Kuna mazingira ujamaa utafanya kazi vizuri, na mazingira ambamo utakuwa ni disaster. Na mazingira haya yanajumuisha watu wenyewe waliopo na mtazamo wao wa dunia.

Hakuna magic formula ambayo ukiitumia tu basi mambo yote yanawanyookea.

Historia inatuonyesha kwamba sehemu ambapo capitalism inafanya kazi, kulikuwa na kitu kinaitwa feudalism kabla, ambacho kiliandaa mazingira mazuri kwa ajili ya capitalism kuanza na kukua. Capitalism haikutokea tu kwa sababu watu waliamua "kuanzia sasa kila mtu alipie huduma", ilikuwa kama natural evolution kwenye jamii husika, na kwa kuwa ilisaidia kukuza uzalishaji, na kwa ujumla kusaidia jamii husika kuendelea. And it worked. Na kabla ya feudalism kulikuwa na mazingira mengine ambayo yaliruhusu feudalism kukua kama natual replacement ya mode of production ya wakati huo.

Ninaochosema hapo ni kwamba badala ya kutafuta magic forumula (na kujiuliza ni ubepari? au ni ujamaa?) inahitajika kuyaangalia matatizo na mazingira yake na kuyapatia ufumbuzi mahususi badala ya kutafuta suluhisho rahisi kwa sbabu tu ni la kibepari au la kijamaa.

Na kwa kadiri ninavyojua hakuna jamii yoyote ambayo ni pure ya kijamaa, au pure ya kibepari. Jamii zote zinamchanganyiko wa hizo mbili, na tofauti inakuwa ni kwa kiasi gani inalalia upande upi. Na jamii fulani inafanikiwa kuendeleza ustawi wa watu wake pale inapopata uwiano ulio sawia. Na uwiano ulio sawia unaweza kuwa si sawa katika jamii tofauti, la sivyo huo uwiano ndio ungekuwa magic forumla yetu.

Naomba nifafanue kwa kutumia uliyoyaandika.

Unaposema "Serikali kazi yake ni kutunga sheria, ,kusimamia sheria na udhibiti wa kanuni na kujenga misingi imara ya kuwezesha uzalishaji mali, misingi kama Barabara, Maji, Reli, Mtandao wa Umeme, Simu" mimi napata ujumbe mmoja kwamba unakubali kwamba kuna mambo ambayo jamii inabidi kuwajibika kwa pamoja kuyashughuliakia (some sort of ujamaa). Kwa hiyo unakubali kwamba Ubepari peke yake pengine hautaweza kuyafanyia kazi kiufanisi mambo haya. Na uko sawa kabisa.

Kwa hiyo kuchanganya ujamaa na ubepari ni ngumu kuepuka. Ila swali la msingi ni je, lipi liendeshwe kibepari na lipi kijamaa? Na hapa ndio msuguano kwenye jamii unaanza. Wewe umetaja maeneo yanayotakiwa kufanyiwa kazi na jamii nzima, mwingine atapingana na wewe kwenye hili au lile, either kwa sababu za msingi au maslahi binafsi. Na bahati mbayo anayeshinda hayo malumbano si lazima awe aliye sahihi. Na hicho ndio chanzo cha matatizo zaidi; hakuna mchawi.

Unaposema "Bure imefika tamati" unanipa utata kidogo. Kwa sababu ninavyojua hakunaga cha bure, hata kwenye ujamaa. Dhana kwamba kuna watu wanapewa vya bure inasababishwa na uelewa finyu wa mchango wa kila mmoja katika jamii husika.

Kwa mfano mkulima analima kahawa miaka nenda rudi. Asilimia kubwa ya mapato yanayotokana na mauzo kahawa yake inabaki huku mjini na nyie ndio mnatanulia. Kumbuka kahawa yake ndio inaleta fedha za kigeni nyie mnaenda kununulia mashangingi ili muweze "kumtembelea kwa urahisi". Kesho na kesho kutwa akitaka mumsaidie kumpeleka mtoto wake chuo kikuu mnamwambia mnampa bure? Mnaangalia mnachompa tu anachowapa nyinyi je?

Mtu miaka miwili tu tangu amalize chuo amekatwa kodi kiasi ambacho ni zaidi ya ile ambayo alikopeshwa. Achilia mbali mchango wake kwa ujumla katika pato la taifa. Kumbuka mchangu huu ungekuwa mdogo zaidi kama angeishia form 6. Halafu mnasema mmempa bure? Mbona hamuongelei mchango wake?

Mkulima kule kijijini anahenyeka na kuwazalishia chakula, mnampa hela ya mbuzi. Fedha nyingine yote wanachukua wachuuzi hapo katikati, na nyie huku mjini mnafurahia kula mboga saba. Na huku mnamkata kodi kwa kila anachokiuza na anachokinunua (VAT). Kesho na kesho kutwa ukame unatokea hawezi hata kununua chakula chake. Mnampelekea chakula cha msaada. Utathubutu kusema mnampa bure?

Watu ambao hawachangii chochote kwenye pato la taifa mmewaacha wajijue wenyewe (Wahadzabe, etc). Hamuwakati kodi, wala hamuwapelekei chochote. Kwa hiyo yeyote mnayechukua kodi kutoka kwake mna wajibu wakumsaidia anaposhindwa. Sio bure, ameshalipia, na anaendelea kilipia. Msipende kupata tu, kutoa mnaona tabu.

Labda nihitimishe tu kwamba iwe kwenye ujamaa au ubepari, maendeleo ya mtu mmoja mmoja ndio maendeleo ya jamii nzima. Ukisema maendeleo yawe kwa wanaotaka na ikawahivyo, basi usishangae pale wasiotaka wakiwarudisha nyuma hata wale wanaotaka. Na mabepari waliofanikiwa wanajua hilo, na wanajitahidi kadiri inavyowezekana kuhakikisha haachwi mtu nyuma kwa sababu kila anayeachwa nyuma ni mzigo uatakaokuwa unawavuta nyuma.

Mzee Augustine Moshi amegusia elimu. Unaweza ukadhani ubepari wako ni tosha kukupeleka mbele. Lakini kumbuka kila asiyeelimika katika jamii yako atakuwa mzigo kwako utake usitake, directly au indirectly. Kesho na keshokutwa utahitaji waajiriwa wako wawe na ufanisi wa hali ya juu ili huo uzalishaji wako uwe wa hali ya juu. Utashangaa pale utakapogundua kwamba wewe umejitahidi wao ndio wanaokuangusha kwa sababu ya uelewa mdogo na elimu duni. Utasema ngoja uwalipe mshahara mdogo maana uzalishaji wao ni mdogo, nao wanaanza kukuibia. Hehehe :) Ulidhani elimu kila mtu kivyake na sasa unashtukia inakula kwako.

Sasa bepari mwenye akili timamu atasema "kodi yangu mimi itumike kupeleka hawa shule", na hiyo ikitokea ustawi wa bepari na hao walioelimika unakuwa, na ndio jamii inakuwa.

Iangalie elimu kama investment na si matumizi. Pengine itakusaidia kuona kwa nini mabepari wengine wanawalizamisha watu waende shule "bure". Na nikuhakikishie kwamba investment hii inalipa.
 
Haya mambo ya aidiolojia kubwa yameshindwa tayari. Ukomunisti/Usoshalisti ulishindwa kuanzia Ulaya mpaka Afrika (na sasa umebaki unasimama kwa nguvu za madikteta tu huko Korea Kaskazini na Cuba) na Ubepari ndiyo huu tunauona unatetereka kutokana na uroho wa pesa.

Napenda jinsi mchungaji anavyosema "Ubepari wa Mchungaji" kwa maana ya kwamba hataki kutumia ubepari wa kitabuni.Ubepari wa kitabuni umejaa mikanganyo na mara nyingi hii imekuwa sababu ya kushindwa kutekelezeka.

Kwa mfano, wahafidhina wa Marekani (natumia mifano ya watu walioendeleza mifumo hii kwa miaka mingi ili tuone walivyofanya) unakataa kuwa na serikali kubwa, na ukienda katika upande wake wa watu wasiopenda kuingiliwa (conservative libertarians) wanaamini katika soko huria, lisilo na vikwazo, na lisiloingiliwa na serikali. Lakini katika nchi ambayo kuna matabaka, mengine yakiwa yamepatikana katika utumwa, kuwa na soko huria lisiloingiliwa na serikali ni pingamizi kwa wengine kuingia katika biashara. Huwezi kuwa na equal access bila serikali kuingilia, hata kama ni kidogo.

Naweza kusema vivyo hivyo kuhusu wengine kama social democrats na liberals wanaamini katika serikali kuingilia sana, lakini hapa nilitaka kuangalia wahafidhina na mabepari.

Binafsi naamini katika kutatua matatizo, hata kama itabidi kuchanganya aidiolojia au kutunga mpya.Zilizopo zimeshindwa.
 
Ubepari wa Mchungaji unasemaje kuhusu Elimu kwa wote? Wale wasio na uwezo wa kulipa ada zao wenyewe walipiwe na sisi sote au waachwe tu? Vyuo vikuu wasome watoto wa matajiri tu au tufanyeje?

Kijumla, Ubepari wa Mchungaji unasemaje kuhusu user-pay policy? Huduma za hospitali kwa wale wasio na uwezo (na ni wengi kweli kweli) ziweje?

Mchungaji ajibu hoja.


Mwalimu,

Kabla sijajibu swali lako, ngoja nikudunge swali, Ujamaa umetufikisha wapi kielimu na kiafya?

Kama Kenya na Uganda waliokimbilia Ubepari uchwara misingi na mfumo wa Elimu na Afya ni bora kuliko Tanzania, tulikosea nini na dhana ya elimu na afya kwa watu wote na kwa bure?
 
Rev:

Tunaweza kuwa mabepari wazawa. Lakini kuna uwezekano kuwa mabepari hao watakuwa ni asilimia 2 tu ya nchi na wenye kutumia zaidi ya asilimia 90 ya mapato ya nchi na kuwaacha wengine katika umasikini wa kutupwa. Sioni kama huo ubepari utakuwa ni suluhisho kwetu.
 
Mwalimu,

Kabla sijajibu swali lako, ngoja nikudunge swali, Ujamaa umetufikisha wapi kielimu na kiafya?

Kama Kenya na Uganda waliokimbilia Ubepari uchwara misingi na mfumo wa Elimu na Afya ni bora kuliko Tanzania, tulikosea nini na dhana ya elimu na afya kwa watu wote na kwa bure?

Ujamaa ulitufikisha mbali sana kielemu na kiafya. Tatizo lilianza baada ya kuupiga chini na kuvamia UNYANG'AU...Tunachokiona sasa ni matunda ya baada ya kupiga chini ujamaa na sio matokeo ya ujamaa.

Tunaweza kupima ujamaa kuanzia 1967 hadi 1977. Kilichotokea baada ya hapo haikuwa sababu ya ujamaa bali ushindi wa njama za maadui wa nje na wa ndani wa ujamaa pamoja na matukio ya kimataifa...

Tanzanianjema
 
Mwalimu,

Kabla sijajibu swali lako, ngoja nikudunge swali, Ujamaa umetufikisha wapi kielimu na kiafya?

Kama Kenya na Uganda waliokimbilia Ubepari uchwara misingi na mfumo wa Elimu na Afya ni bora kuliko Tanzania, tulikosea nini na dhana ya elimu na afya kwa watu wote na kwa bure?

Hata aikijibu kwamba "ujamaa haukuifikisha Tanzania kokote kielimu na kiafya" unadhani hiyo itakuwa tosha kuhitimisha kwamba "ujamaa haufai"?

Ni sawa sawa na mtu akakukumbusha kwamba uchumi wa dunia unayumba sasa hivi nakakuambia kwamba hiyo inaonyesha kwamba ubepari umeshindwa, kwa hiyo ubepari haufai.

Unatafuta majibu rahisi kwa mswali magumu. Naomba nisisitize tena hakuna magic formula. Kama huwezi kutatua matatizo yako, basi si ujamaa wala ubepari utakaokusaidia. Hakuna manual ya ujamaa au ubepari inayoelezea jinsi ya kutatua matatizo yote.

Na ukiangalia vizuri utakuta watu wanatofautiana sana kwenye definition zao za ujamaa na ubepari. Unaweza kuta mnabishana wee, kumbe kila mmoja ana uelewa wake.

Kwa mfano, muheshimiwa Mchungaji uko against kabisa na "bure" kwa sababu unaamini ni dhana ya kijamaa, na ujamaa haujaifikisha nchi yako popote, na pengine ujamaa ndio chanzo cha matatizo yako yote. Na nadhani unaamni kwamba USA, UK, Australia, e.t.c. ni nchi za kibepari. Sasa ushawahi kusikia "unemployment benefits"? ( Unemployment benefits - Wikipedia, the free encyclopedia ). Je, unafahamu kwamba USA na UK wapo watu wanalipwa fedha za "bure" kihivyo? Je, hiyo inafanya nchi hizo ziwe za kijamaa?

Lesson of the day: ukitaka kuzungumzia ideologies, jaribu kuzielewa kwanza; wengi huwa tunazikurupukia na kuzipachikia dhana ambazo si zake. Elewa kwamba Ujamaa ni nini na Ubepari ni nini.
Mkapa mwenyewe aliingia kichwa kichwa akidhani ubepari maana yake ni FDI, sasa hivi, kwa habari sisizo thibitika, tunasikia anajuta huko aliko :) Wasiwasi wangu ni kwamba wewe unadhani ujamaa ni kuwa na vitu bure, na ubepari ni kila mtu kujigharimia.

Ukiniuliza mimi ntakwambia ideologies zote zikitumiwa peke yake huwa zina-fail kwa sababu unakuwa unajaribu kutoa one simple solution to all complicated problems. People cling to ideologies when they run-out of ideas. Badala ya kufikiria ni jinsi gani ya kutatua matatizo ya elimu au afya, kwa mtu mwingine ni rahisi zaidi kudandia ujamaa au ubepari ukiamini kwamba hilo ndilo litakuletea suluhisho la matatizo yake yote au ndio chanzo cha matatizo yake yote. Mwingine atalaumu ujamaa au ubeprari mpaka pamoja na kushindwa kupata mke mwema au mume mwema. :)
 
Last edited:
Kwanza kabisa katika mijadala ya namna hii ambayo ina msingi wa matumizi na maana ya maneno ni vizuri kwanza kabisa tujue tunazungumzia nini. Yawezekana tunaposema Ubepari na Ujamaa tunazungumzia kitu kile kile isipokuwa kutoka katika mtazamo tofauti kama wale vipofu waliopelekwa kwenda kushuhudia tembo aliyeuliwa. Kila mmoja aliweza kusimulia jinsi alivyomuona tembo kwa kupapasapapasa. Matokeo wakawa wanabishana sana juu ya tembo yukoje.

Sasa tunaposema Ubepari au Ujamaa tunamaanisha nini?

a. Je tunamaanisha mifumo ya kiuchumi, utawala, kisiasa ya nchi hasa zenywe mwelekeo wa falsafa za Magharibi kama vile Marekani, Uingereza, Japan n.k kwamba ndiyo Ubepari na wakati huo huo tunaposema Ujamaa tunamaanisha mifumo ile ya kiuchumi iliyowahi kutumiwa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisoviet?

b. Tunaposema Ubepari tunazungumzia ile hali ya uzalishaji na ulaji kama maana ya kiasili kama inavyonyambuliwa na Adam Smith katika the "Wealth of Nations" na wenzake wa kipindi cha mageuzi ya Nchi za Magharibi?

c. Tunaposema Ujamaa tunazungumzia ile hatua mojawapo ya mwelekeo wa mwanadamu kama ilivyodokezwa na kina Karl Max katika "Das Capital" na maandishi ya baadaye ya watu kama kina Lenin, Kim Jong Ill (Juche Idea).

d. Tunaposema Ujamaa tunamaanisha jinsi ambavyo ulifafanuliwa na Mwalimu katika treaties yake ya "Ujamaa" jinsi ambavyo yeye aliuona unaweza kutumika Tanzania au ni ujamaa kama wa Muammar Qadaffi unaofafanuliwa katika The Green Book?

Hivyo kabla sijajitupa katika ulingo huu wa kuonesha ni kwanini Ujamaa bado ndiyo mkombozi wa kweli wa Tanzania naomba Mchungaji atupatie maana ya "Ubepari" na "Ujamaa". Na anaweza kufanya hivyo kwa kuweka dondoo tu na naamini watu watamuelewa.

Naomba atupe angalau sifa saba za Ubepari ukitofautisha na Sifa Saba za Ujamaa. Vinginevyo mimi naweza kuzungumzia sikio na mwingine akizungumzia Mguu wakati mwingine akaamua kuzungumzia ubavu!!!!
 
Badugu,

Sizungumziii Ubepari kama itikadi ya siasa, ingawa huwezi kuwa na mfumo wa Kibepari bila kuwa na itikadi inayoendana nayo.

Labda nifafanue bila kumpa Mwanakijiji tafsiri saba za kila mfumo.

Hivi leo tujiulize, yule Mchaga na Mpemba ambao walikuwa na maduka mitaani kwetu kwa nini tuliwachukia na kuwaita makabaila kisa ni wafanyabiashara?

Mkandara, wote tunajua ni mfanyabiashara, akirudi kwao Nansio kufanya biashara yake kwa uhalali kisha akaamua kugombea Udiwani au Ubunge kwa nini tumkatalie kwa sababu yeye ni mfanyabiashara?

Ubepari ninaozungumzia ni mfumo wa kiuchumi ambao utaruhusu watu kuweza kuwa wazalishaji mali stadi na kuzalisha kwa ziada bila kujisikia vibaya au kutomaswa vidole kisa wimbo wa kale unaosema Ubepari ni Unyama.

Taifa lolote ili liendelee, linabidi lijengwe kwa nguvu za raia wote na hasa tabaka la kati.

Sisi Tabaka la kati lilikuwa kwa muda mrefu ni waajiriwa wa Serikali na Mashirika ya umma ambao hutegemea mishahara na si wabunifu wa kuzalisha mali.

Ndiyo nazungumzia kupunguza chee na dezo kwa kuwa kwa mgongo wa kusema lazima tutoe huduma bure kwa raia wetu "masikini" tumeendeleza umasikini kwa nguvu za nyuklia na si kuondokana na umasikini.

Mwanadamu anapopata upenyo wa kupata kitu kwa bure, hufurahia na kuloea mpaka kujisahau na siku ukimuondolea dezo atachukia.

Lakini hatuwezi kuendelea kulialia kuwa sisi ni masikini tusaidiwe kwa kila kitu na tupatiwe huduma kwa bure bila sisi wenyewe kuchangia.

Mmezungumzia Wamarekani kuwa na shule na huduma za afya bure, je pesa za kuendesha shughuli hizi zinatoka wapi kama si kodi za mapato? iwe mapato ya mishahara au mauzo?

Sisi kodi tunamkimbizia Manji na Mengi, yule Bundala, Lyimo na Masauni ambao ni wakulima au wavuvi tunawapa "ruzuku" ya kuwasamehe kodi kisa tunadai wao ni masikini hawawezi kulipa kodi, huku tukiwanyonya kwa kuwalipa fidia ndogo ya uzalishaji mali wao.

Sasa kama dhana ni hiyo, kulimbikiza kodi kwa wachache na hata tunataka kodi kubwa kwa wawekezaji lakini siye wenyewe tunapiga chenga, iweje basi tutegemee vya bure?

Wale jamaa wa Gerezani, Sido na hata Veta, ni watu ambao tunapaswa kuwajenga wawe makabaila fulani, wenye kutumisa ustadi, ubunifu na uchapakazi kuzalisha na kuleta maendeleo. Wanachokivuna kwa halali tukipigie vigelegele na si kuwabeza au kuwatisha.

Kwa Tanzania kuendelea, ndiyo tunahitaji mfumo mpya wa kiuchumi ambao unalenga kujenga nguvu za uzalishaji kwa kila tabaka, na zaidi tunahitaji tubadili nadharia zetu na tabia zetu ili tuweze kuwa washindani na wazalishaji bora.

Ni ajabu Machinga wa Kichina anapeta na kuwa tajiri au mgeni aliye selule anakuja na Pasipoti akikaa mwaka mmoja tunafurahia yeye kuwa Bepari kutumia jasho na hazina yetu.
 
Last edited:
.......................Samahani sana, mie sijui kuchangia lakini najua kuwa ubepari na ukabaila hautufikishi popote.Heri yetu ni pale tutakapotambua haki zetu a kuzidai na kupewa basi !!!!...........................
 
Mchungaji kwa kweli kwa maana yako inawezekana hatuzungumzi Ubepari wala Ujamaa, tunazungumzia Maendeleo!
 
Ujamaa kama mfumo wa kisiasa ulileta matunda ya umoja, lakini kama mfumo wa kiuchumi, tulitoka kapa!

Tumeshajenga jamii iliyokomaa, hivyo kujenga uchumi shurti tuende kwenye Ubepari kama mfumo wa kiuchumi, huku tukiishi kijamaa.
 
Ujamaa kama mfumo wa kisiasa ulileta matunda ya umoja, lakini kama mfumo wa kiuchumi, tulitoka kapa!
Mimi nionavyo ni kwamba mlitoka kapa kwa sababu ya matatizo yenu mengine na jinsi mlivyo. Na haya matatizo yenu mengine na jinsi mlivyo vinaweza vikawafanya mtoke kapa hata kwenye huo ubepari. Tatizo sio ujamaa wala ubepari, tatizo ni nyinyi.
Tumeshajenga jamii iliyokomaa, hivyo kujenga uchumi shurti tuende kwenye Ubepari kama mfumo wa kiuchumi, huku tukiishi kijamaa.

Unajua ujamaa na ubepari ni concepts ambazo ni vague kidogo. Ingekuwa rahisi ungezungumzia nini hasa ungependa kibadilike, au kifanywe tofauti (kibepari). Maana kama ni kubinafsisha mmebinafsisha, na aliyewaongoza kwenye hilo (Mkapa) anajuta nasikia huko alipo. Elimu mmebinafsisha, na kiwango cha kufaulu kinashuka, na kama kiwango cha kufaulu kinashuka, utalia tukizungumzia kiwango cha kuelimika.

Hebu niambie, ile TICS inaendeshwa kijamaa? Hivi huo uozo utaondokaje matakapoamua kuanza kujiita mabepari? Je, mnahitaji kuendesha BOT kibepari ili msiibiane hivyo? Na mnaendeshaje BOT kibepari? Kwani sasa hivi inaendeshwa kijamaa?

Ujamaa umewasainisha vipi mikata mibovu? Wataalamu ambao pengine ungesema wamekulia kwenye huo ujamaa wanawashauri vizuri msiingie kichwa-kichwa, mnawapuuza, mnang'atwa. Sasa ubepari utawasaidiaje kwa hilo?

Naomba niseme kwamba sijaribu kukueleza jinsi ujamaa ulivyo mzuri, au ubepari ulivyo mbaya.

Najaribu kukuambia kwamba tatizo sio ubepari au ujamaa tatizo ni nyinyi na jinsi mlivyo.
 
Unajua ujamaa na ubepari ni concepts ambazo ni vague kidogo. Ingekuwa rahisi ungezungumzia nini hasa ungependa kibadilike, au kifanywe tofauti (kibepari). Maana kama ni kubinafsisha mmebinafsisha, na aliyewaongoza kwenye hilo (Mkapa) anajuta nasikia huko alipo. Elimu mmebinafsisha, na kiwango cha kufaulu kinashuka, na kama kiwango cha kufaulu kinashuka, utalia tukizungumzia kiwango cha kuelimika.

Hebu niambie, ile TICS inaendeshwa kijamaa? Hivi huo uozo utaondokaje matakapoamua kuanza kujiita mabepari? Je, mnahitaji kuendesha BOT kibepari ili msiibiane hivyo? Na mnaendeshaje BOT kibepari? Kwani sasa hivi inaendeshwa kijamaa?

Ujamaa umewasainisha vipi mikata mibovu? Wataalamu ambao pengine ungesema wamekulia kwenye huo ujamaa wanawashauri vizuri msiingie kichwa-kichwa, mnawapuuza, mnang'atwa. Sasa ubepari utawasaidiaje kwa hilo?

Naomba niseme kwamba sijaribu kukueleza jinsi ujamaa ulivyo mzuri, au ubepari ulivyo mbaya.

Najaribu kukuambia kwamba tatizo sio ubepari au ujamaa tatizo ni nyinyi na jinsi mlivyo.


Ewe Mkanada,

Uendeshaji wa Mashirika Tanzania ni kwa mfumo wa kijamaa ambao Serikali ina mikono yake ndani na kuingiza siasa.

Kama vyobo hivi vingeendeshwa kibiashara na huru ya Serikali na Wanasiasa kama vile TBL na TCC, basi tusingehangaika na Umeme, Maji au Chakula!
 
Nikiweza kupata majibu haya, nafikiri ubepari utakuwa sio suluhisho.

Ubepari na Masoko Huria yanaenda sambamba?

Je Ujamaa, hauwezi kwenda sambamba na Mfumo wa soko huru?
 
Rev Kishoka, mkuu ulipotea lakini umerudi na nadhani umenikuta niko fuming baada ya kuona kuwa hoja nyingi katika JF, inajaribu kuturudisha nyuma, eti serikali hivi serikali hivi.... oh mafisadi....terrible!
You have expressed my sentiments and sign me on anytime for your political party and for your political campaign, nitakuundia mfumo kabambe wa kisiasa kama wa Obama! Na utashinda kwa kishindo! Yaani kwa msimamo wako, I know that the best and the brightest of Tanzania will support you kwa sababu tumechoka kunyooshewa kidole kila siku! This is the tyranny of the mediocre! If you excel, they cut you down!
Mi naomba nisichangie as I see that you have the debate firmly under control, lakini hapa katikati nimechangia weee, nikaitwa fisadi! Hahaaa!
 
Rev. Kishoka,
Huwezi kupata yote mkuu, itikadi siku zote ndizo huzaa matokeo kiutendaji.. Ni kama daktari ile elimu yake ya shule ndiyo inayotumika kufanyia matibabu... na pinzani na Udaktari ni Uchawi akichanganya mambo haya tumeua mgonjwa..
Kifupi ndio maana Nyerere aliita Ujamaa kuwa ni mfumo wa kiafrika ambao haufungamani na upande wowote..In fact tulifungamana toka kisiasa hadi kiutendaji na ndio maana tuliboronga ktk uchum kwa sababu huwezi kufundisha hili kisha ukategemea fikra na matendo vizifungamane..

Historia yetu inatuambia kabisa kwamba kijamii tulikuwa wamoja (kwa mafungu) hata kabla ya Uhuru na ndio maana hata ktk harakati za Uhuru Nyerere aliweza kwenda mikoa yote akapokelewa akizungumza kiswahili kuomba kura za wananchi..
Hofu yetu kubwa ilikuwa ni ktk siasa... huu mfumo mpya wa kiutawala ambao ulianzishwa na nchi za Ulaya kuwa na vyama kuongoza na sio Machief kuwa ati ndio mfumo bora wa kiutawala, hivyo kulikuwepo na kazi mpya ya Nyerere kuweza kuvunja tawala zilizokuwepo kuunda serikali inayoweza kukubalika na wananchi..Na ndio maana tunampa sifa mwalimu kuweza kuondoa Ukabila kwani haikuwa kazi ndogo kuua utawala wa majimbo ambao ulitokana na tawala za makabila (chiefs)..Kwa hiyo mipaka yetu ya kimajimbo kama ya Ulaya ilikuwepo toka zamani, isipokuwa tu sisi majimbo hayo yalikuwa ni tawala kamili zenye majeshi na wizara zake chini ya Mtemi kama ilivyo Zanzibar ktk muungano huu..
Tatizo letu kiuchumi limeanza pia toka zamanai ingawa sote hatupendi kurudi nyuma kutazama tulikotoka..Lakini ukweli utabakia kwamba Utumwa ni moja ya athari kubwa za urithi wa mkoloni.
Sina maana nawalaumu wazungu isipokuwa nawalaumu wazee wetu, viongozi wetu ambao kama waliweza kuondoa dosari za Ukabila walishiundwa vipi kuondoa dosari zilizotokana na utumwa kwa sababu huo ulikuwa utamaduni wa kuagiza..

Hesabu kubwa ya watanzania wanategemnea ajira yaani maisha yao tunasoma ili tupate ajira na hatujiamini kabisa kama tunaweza kuanzisha kitu bila kuwa na mtaji mkubwa..Tumeshindwa kuelewa kwamba asilimia kubwa ya matajiri duniani wamerithi utajiri huo na nusu yake wametokana na elimu.. chanzo cha utajiri ni innovation na wachache sana waliweka msingi mkubwa zaidi ya akiba zao hivyo utajiri umetokana na idea wala sio ukubwa wa mtaji..ni kundi dogo sana la matajiri walioweza kutumia fedha kutajirika na kama ingekuwa rahisi hivyo basi uwekeshaji wa mpango wa Obama hizo Usd Billioni 800 usingekuwa na mazungumzo..Utajiri hutokana na kile unachoweza kuuza baada ya kuzalisha, hivyo kupanuka kwa maendeleo kunategemea soko la mauzo ya mali yako unapozungusha na sio fedha uloanza..

Mkuu, hili ndilo tatizo kubwa la urithi wa utumwa tulioachiwa na mkoloni na sio kubaguliwa au unyonge wa mateso kwani hata Wayahudi na Waigereza wenyewe walipitia taabu tena zaidi yetu sisi kupitia kutawaliwa..Lakini wenyeztu waliweza kuondokana na akili ya kitumwa, wakajifunza elimu ya sayansi na teknologia ktk vipaji walivyopewa na mwenyezi Mungu kujenga msingi bora wa maendeleo yao wenyewe kulingana na mazingira yao..Sasa ukija kwetu sisi tumeshindwa hata kutambua nini vipaji vya mwafrika zaidi ya kuiga, kuwa watumwa wa mawazo na hata viongozi wetu kina Mkapa wanaamini kabisa kuwa sisi ni wajinga hatuna lolote isipokuwa wivu, chuki, majungu na kadhalika..
Haya ni matusi makubwa lakini yana ukweli ndani yake kwa sababu ni mtumwa tu wa akili huwa na wivu, majungu, chuki binafsi kwa sababu kuna Upendeleo fulani..Na yule mwenye kusema ni mtumwa vile vile kwa sababu anahisi kuonewa wivu, chuki na majungu kwa sababu amepata kitu ambacho wengine wameshindwa kupewa/kukipata..Hivyo Mkapa sio tu alitutukana sisi bali hata yeyey mwneywe alionyesha ufinyu wa kufikiri kwake.. He is our reflection kwani tunaujua wazi alitoka wapi hadi kufikia urais.. he was nobody na hisia hiyo ilimkwaza kufikiri nje ya sanduku la utumwa.
Kwa hiyo utaona kwamba hata Ubepari wetu ni kama race ya kushindana kula ktk sinia la pilau, hakuna ustaarabu wala feelings kwa mwenye njaa au yule aliyeweza kushiba... maisha ambayo hata wanyama wenye asili moja hawaishi hivyo isipokuwa binadamu watumwa na wanyama wale waliofungiwa ktk cage..
Ni vigumu sana kuweza kusema Ubepari ndio suluhisho la matatizo yetu kwani hatufahamu nini ubepari ukiwa na akili ya kitumwa!..Ni sawa na watoto wanaokula ktk sinia moja kila siku wanaomba Mungu wakue wafikie Umri wa join meza kubwa nao wapate kula na wakubwa kila mtu na sahani yake..Kwa hiyo maendeleo yetu tunayategemea kwa kufikiria Umri na sio nguvu zetu, jitihada zetu na pengine kufikiria kwamba yule mtoto wa mzungu mwenye ustaarabu wa kula kwa vijiko alianza kula amekaa mezani akiwa na umri mdogo sana!..

Well, sijui kama umenielewa maanake hii mifano yangu kuna wakati huwa nashindwa kuiweka ktk lugha ambayo kila mtu atanielewa vizuri!...
 
Last edited:
Mkandara, even though what you have written is complicated but I do understand what you say and i didn't want to sound glibe in my previous post. I agree na ule msemo wako kuhusu mawazo ya kitumwa na unaweza kulaumiwa kuwa umewadharau watanzania wenzako but ni lazima tujifunze kusema ukweli.
Lakini umegusia intrepretation ya ubepari kwetu na ninakubali kwamba unfortunately watanzania wengi wanauona ubepari as a negative thing na hata wale ambao wanasema ni advocates za itikadi hii pia wanaamini ni ubabe... I really appreciate this comment of yours....
Ubepari wetu ni kama race ya kushindana kula ktk sinia la pilau, hakuna ustaarabu wala feelings kwa mwenye njaa au yule aliyeweza kushiba... maisha mabyo hata wanyama wenye asili moja hawaishi hivyo!..
Ni vigumu sana kuweza kusema Ubepari ndio suluhisho la matatizo yetu kwani hatufahamu nini ubepari ukiwa na akili ya kitumwa!..
Lakini hii haina maana kuwa ubepari si suluhisho, ungesema ubepari tuujuavyo sisi si suluhisho! Heshima zote mkuu, umetoa point moja nzito!
 
Back
Top Bottom