Ubepari: Suluhisho la Matatizo yetu!

Susuviri na Mkandara,

Shukranio waungwana kwa kuchungulia humu ndani na kudondosha japo yule mbuni au thumuni!

Leo hii, nimesoma kuwa Serikali inatafuta wawekezaji wa zile Ranchi za Taifa, ili wajenge viwanda vya kusindika nyama, nikajiuliza, kwa nini serikali yetu bado inaburuzana na uzalishaji mali na si kukinga mikono kuvuna kodina ushuru, huku ikihakikisha sheria na kanuni zinafuatwa kulinda usawa na ustawi wa uchumi na jamii?

Jibu linakuja kwenye mfano wangu wa kusema siasa ya ujamaa na dhumuni la Serikali kuendesha shughuli za uzalishaji mali.

Tuliyoyafanya miaka 20 ya kwanza ya Uhuru yalikuwa na ulazima pamoja na kasoro zake.

Kasoro zilizokuwa katika zoezi zima la Azimio la Arusha na Ujamaa na hasa kutaifisha mali ni kuondoa nguvu za watubinafsi kuwa wazalishaji mali mahiri, wenye ubunifu na ufanisi wa hali yajuu.

Kilichoharibu ni kuingiliwakwa Uzalishaji mali katika kila skta na Siasa. Ndio siasa kama hamasisho lilifaa, lakini kama muongozo na injini ya uzalishaji hapo tulikosea ndio maana nauliza yule Mpemba na Mchaga kwa nini tuliwaona si wenzetu na kuwanyooshea vidole kuwa ni wanyonyaji?

TUlichokifanya vyema kwa Ujama ni kujenga umoja wa kitaifa na kukomaa kisiasa. Lakini madhara yetu kukomaa kisiasa ni kuewa mvinyo wa Umwinyi wa madaraka ya Kisiasa na hivyo kujenga jamii tegemezi inayotegemea Serikali ifanye kila kitu na zaidi watendaji kutumia fursa hii kujineemesha kutokana na ukosefu wa Ubunifu na Ajira imara katika sekta binafsi.

Leo hii, kia mtu anasema kufanya kazi Serikalini ni mali, maana uhakika wa maisha upo, na huu uhakika si wa ustawi kupitia mishahara pekee, bali ni ubunifu wa kinyonyaji ambao tunaupigi vita humu ndani kwa jina la ubadhirifu, uhujumu na ufisadi.

Leo hii kama wakati wa Azimio la Zanzibar tungebainisha wazi ni vipi Azimio hili lingetuletea maendeleo ya Uchumi na kuoanisha na mwelekeo wetu katika Soko Huria na Uwekezaji, tusingefikai mahali tulipo ambapo Serikali inashindwa kujiongezea mapato na hivyo kuanza kutafuta njia za panya kuongeza pato na kuanza kuuza mashirika hovyo au kuingia mikataba hovyo.

Hili linatokana na kukosekana kwa ushindani wa ndani wa kibiashara ambao ungechochewa na mfumo bora wa Kibepari ambapo Serikali kazi yake ni kukusanya kodi na kuratibu shughuli huku ikilinda na kujenga sheria imara na kudhibiti mapato yake kwa kuwa na utaratibu mzuri wa ukusanyaji mapato.

Jiulizeni, kama leo Precision Air na ATCL zingeanza kazi siku moja na kila moja ikawa huru bila mkon owa Serikali, je ATCL ingkuwa inabangaiza na kulitia Taifa hasara?

Je leo kukoanza kampuni mpya ya kusambaza Umeme na Maji ambazo hazitegemei ruzuku ya Serikali au kusubiri muongozo wa Serikali katika kila kitu je tungekuwa na shida tunazozipata kila siku?

Ufisadi ni ufisadi, hata katika mfump wa Kibepari, ufisadi upo. Tatizo katika mfumo wetu wa kijamaa, Ufisadi unatokana na tamaa inayotokana na kukosekana kwa namna au mbinu nyingine za watu kuwa wazalishaji mali na kujipatia kipato halali.

Ndio maana wakati wa Azimio la Zanzibar, tulisikia kauli za kuruhusu Wanasiasa wawe na mashamba, nyumba za kupanga, ng'ombe na kuku wa biashara!

Kwenye Ubepari, pamoja na ushindani wa watu binafsi kuzalisha na kuuza, kuna udhalimu wake ambapo Seriikali ndipo iuna uwezo wa kuingilia kati na kusawazisha kasoro kwa kuwa na sheria na kanuni ambazo ni madhubuti na zaweza kufuatwa na kila mtu.

Katika Ujamaa wa Tanzania na mfumo wetu wa Uzalishaji mali, maafa yake ni Serikali kuwa baba na mama wa kila kitu. Serikali ni mtunga Sheria, mratibu wa Kanuni na ni mzalishajji mali!

Hivi leo, tumesikia Idrisa Rashidi, David Matakka, na wengine ambao ni wakurugenzi wa Mashirika ya Serikali wakituhumiwa, lakini kila siku wanaednelea na shughuli, je haitoshi kuhoji ni vipi Serikali inakuwa na ugugumizi wa kutatua kasoro za kiutendaji na ufanisi? Jibu ni kuwa Serikali ndio tatizo!

Nakubaliana nawe Mkandara kuwa tuna makovu fulani ambayo inabidi tuachane nayo tuyasugue kwa dodoki kama si jiwe lamtoni ili tuweze kuwa na ngozi mpya.

Leo kama tukiilazimisha sekta binafsi ikashikilia uzalishaji mali na Serikaili ibakie kuratibu mambo, utaona tofauti yetu na Kenywa kwa haraka sana.

Nina imani kubwa sana na Watanzania kwa umoja wao, wanachohitaji sasa ni hamasa ya kuwa wazalishaji mali na kuondokana na fikra potofu kuwa kuwa na mali nyingi (za halali) ni dhambi haa kama Msahafu unasema ni rahsi kwa Ngamia kupenyeza tundu la Sindano kuliko Tajiri!
 
Amani iwe nawe!

Rev. Kishoka,

Ni lazima tutoe fasihi ya Ubepari na ni lazima tuyachambue matatizo yetu!

Tukubaliane, Ubepari haukutokea Nchi za magharibi kama wengi wanavyojua.

Ubepari ulitokea baada Wakiristo kugawanyika, wasomi wengi wameweza kuona hili, wameteta kuwa maadili ya waprotestanti kufanya kazi kwa nguvu zote na ulimbikizaji wa mali, yaani, na uwekevu. Hii imechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa ubepari. Hawa 'waprotestanti' ni wanajamii.

Hakika wananchi wengi wanafikiri "Mabepari" ni watu si salama, na hivyo basi kuonekana kama wadanganyifu, wevi, na, ni weupe tu. Hii sio kweli kama tunavyoona-ni wenye kufuata maadili ya kazi, ni wadini, ni jamii iliyojitenga na hukumu zao wenyewe.

Hapa naona ni lazima tuone mila na desturi zetu kijamii-zinavyochangia kisiasa na kiuchumi(kama haya ndio matatizo yapo hapa), na hatuwezi kuyaongelea hayo hapo juu kama hatutaongelea elimu na historia yetu kwa ujumla.


Hapo juu tunaweza kupata majibu mengi tu kuhusu huu 'Ubepari' na jinsi gani unachangia kuleta na kuondoa matatizo yetu.


Rev,

Matatizo yetu yako very vast! Tutafika!

Umeweka point nzuri huko juu, naamini ubepari tulikuwa nao(soma historia yetu) bado tunao na unaendelea kukua.

I will differ from your perspective though, nonetheless i can concur, but- Ubepari siyo suluhisho la matatizo yetu!

Amani ibakie nawe,

SYK
 
Back
Top Bottom