#COVID19 Ubelgiji kuipatia Tanzania dozi 115,200 za Johnson & Johnson

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Serikali leo inatarajia kupokea chanjo aina ya Johnson & Johnson dozi 115,200 kutoka Ubelgiji ili kuchangia kuongeza kasi ya kampeni ya kuchanja.

chanjo.jpg


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Ubelgiji na kuthibitishwa na serikali ya Tanzania, chanjo hizo zitachangia kuongeza kasi ya kampeni ya chanjo nchi nzima ili kulinda maisha na afya za Watanzania.

“Usambazaji wa chanjo hufanyika kupitia msambazaji wa kimataifa COVAX, na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF).

“Mchango huu ni sehemu ya ahadi ya awali ya Serikali ya Ubelgiji ya kusambaza angalau chanjo milioni nne kwa nchi za kipato cha kati na chini kufikia mwisho wa mwaka huu.”

Taarifa hiyo ilisema Ubelgiji imetekeleza ahadi hiyo na hadi kufikia sasa imetoa chanjo milioni tisa kupitia COVAX, pamoja na mchango wake wa kifedha wa EURO milioni 12.

Ilisema chanjo ya UVIKO-19 hupunguza hatari ya maambukizi pamoja na matatizo yake yanayoweza kuwa makubwa.

“Iwapo watu wengi iwezekanavyo Tanzania watapewa chanjo, kuenea kwa virusi hivyo kutazuilika. Tunaipongeza serikali kwa kuzidisha kampeni za kuongeza uelewa ili kuwafahamisha wananchi kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kupata chanjo na kuwezesha kupatikana nchi nzima,” ilisema.

Taarifa hiyo ilisema upatikanaji wa chanjo ya UVIKO-19 Tanzania bado ni mdogo na ni chini ya wastani wa Afrika. “Kwa ombi la Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo, Meryame Kitir, mlengo wa nchi yetu wa kutoa michango baina ya nchi mbili utakuwa Afrika na hasa zaidi kwa nchi washirika wa Afrika, ambapo upatikanaji wa chanjo unakosekana sana,” ilifafanua.

Ilisema wakati Ubelgiji na nchi nyingi za Magharibi sasa zina viwango vya kuridhisha vya chanjo, kwa wastani barani Afrika karibu asilimia tano ya watu wamechanjwa.

Kaimu Mkuu wa Mawasiliano Idara ya Afya wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Catherine Sungura, alilithibitishia Nipashe kuwa serikali leo inatarajia kupokea msaada huo wa chanjo kutoka Ubelgiji.

NIPASHE
 
Kibaya zaidi Hili WIMBI JIPYA la omicron halisikii chanjo ya aina yoyote.

Sasa sijui tunachanja tena ili iweje sasa
 
Naona salamu za shukrani kwa Wabelgiji, na neno beberu halitosomeka.
Tuna Kinga za asili japo kuongeza Chanjo ni hatua bora na muhimu.
 
Vipi kuhusu hili toleo jipya la Omicron ambalo wanasema halisikii chanjo yoyote na lina dili na vijana?
 
Wataalamu wetu ambao wanatusaidia kutambua chanjo hizi zinazoletwa kuwa hazina madhara wamefikia hatua gani katika kutengeneza chanjo yetu wenyewe ili tuache kuwasumbua wenzetu wa ng'ambo na kuangaika kututafutia chanjo?
 
Back
Top Bottom