Chanjo za corona zimepotelea wapi? Na uviko hali ikoje?

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
4,696
10,225
Yale machanjo yetu tuliyopewa zawadi na mabeberu bado yapo?

Siyasikii kabisa siku hizi kama hapo awali kwa jinsi yalivyokuwa yanapigiwa chapuo la mwendokasi.

Nasikia kulikuwa na mafurushi kadhaa ya chanjo. Sijui ni mafurushi ama makapu, lakini naamini hayo machanjo yalijazwa kwenye kapu fulani kubwa kubwa.

Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa na ugwadu wa chanjo basi akaenda kuyafakamia kwa pupa akatushawishi na sie tukadungwe. Nilimuahidi nitaenda.

Nimekaa nikafakari nikaona huu ni muda muafaka wa kwenda kubugia chanjo ya uviko. Sijui wanabugia au wanadungwa kwenye wowowo hata sielewi. Lakini nataka nikapate lile dude. Nikipata la JOHNSON JOHNSON itapendeza.

Sijui hata yanapatakani wapi? Nyie wataalamu wa machanjo huwa mnadungwa wapi?
 
Vita vya Ukraina na Russia vilivyoanza na Corona ijapotea hapohapo.Internationak media zikaachana na Corona
 
Back
Top Bottom