Ubarikio wa Mtoto: Bajeti Milioni 25!

Ubarikio wa Mtoto: Bajeti Milioni 25!

Kuna mambo ni kama tunaya-complicate sana miaka hii

Zamani hizo ubarikio sijui ubatizo, kumaliza darasa za 7, kidato cha nne, wala hakukuwa na sherehe

Lakini miaka ya karibuni, hadi arobaini ya mtoto, wanaweka sherehe, hela zinatolewa kwa michango

Kwahiyo kuanzia January, hadi inafika December unakutana na kadi 25 hadi 30 za michango

Ukikaa upige hesabu ya hiyo michango, unagundua ungeweza kununua bond UTT ama ukanunua hisa hata za milioni 3 TCC ama TBL 🙌
 
Kwanza miaka sisi tunakuwa ilikuwa mafundisho ya kipaimara yanalenga kutujenga zaidi Kiimani,upendo na ushirikiano na siku ya Kipaimara(Ubarikio)ikifika watoto wote waliobarikiwa pamoja na wazazi wao tunashiriki Sherehe happ happ kanisani,mtakula pilau nyama soda kibao baada ya hapo wazazi na watoto mnarudi nyumbani

Hii ya sasa hivi naona sio ubarikio tenaa ni mambo mengine
Wala sio mambo mengine, ni vile wazazi wako (wetu)
1. Hawakulipa uzito kiivyo hilo swala
2. Hawakuwa na uwezo wa kwenda mbali zaidi kama sasa wafanyavyo.

Usijikune usipofika
 
Ila wabongo, Hapo kwenye kamati mlikubaliana vizuri sana hadi huyo jamaa mwenye mtoto moyoni kasema "hawa ndio watu sasa"... ila mmekaa pembeni ndipo mnakosoa bajeti ambayo mlipotisha wenyewe...

Wabongo tukiacha unafiki tutafika mbali sana, tukianza kuambiana ukweli tutafika mbali...

Yanayotokea huko serikalini yanaanzia huku, mngekuwa serikalini ina maana mngepitisha bajeti ya hovyo kisa tu mnaogopa kusema ukweli...

Hivi wabongo mnaelewa maana ya kamati kweli? Inapaswa palepale mnamuambia au kumshauri kwa uwazi kwamba hio 25M ni nyingi...
Sio mmekubaliana kwenye kamati halafu mnatoka hapo mmefadhaika na hamjapendezwa...

Bongo noma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom