Ubalozi wa Marekani kuwaondoa raia wake Tanzania kwasababu ya Corona na kuwarudisha kwao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa wito kwa raia wake kurejea Marekani, kufuatia uwepo wa maambukizi ya virusi vya #COVID19

Ubalozi umewataka raia wake wote wanaotaka kuondoka kufanya hivyo mapema kutokana na mashirika mengi ya ndege kusitisha safari. Umesema, hadi kufikia Machi 29, 2020 Shirika la Ndege pekee litakalokuwa na ndege za kutoka nje ya Tanzania ni Shirika la Ethiopia

Ubalozi huo umesema kwa sasa haushughuliki na kuwatoa raia hao nje ya Tanzania kuwarudisha Marekani, ila kama hatua hiyo itafikiwa umewataka wale wote watakaotaka kutafutwa na Ubalozi huo kutuma taarifa zao muhimu za utambulisho

Hadi sasa Marekani ambayo ndio nchi yenye maambukizi mengi zaidi, ina jumla ya maambukizi 85,594 yaliyorekodiwa na vifo 1,300

IMG_20200327_092642.jpg
 
huu ni uthibitisho tosha kuwa corona marekani haipo, au uenda kuendelea kubaki tanzania ni hatari zaidi ya kuwa na ugonjwa huu ukiwa united state of american
Corona haipo Marekani?? Are serious mkuu? Mpaka sasa wameipiku China kwa visa vingi.

Na kuna vifo zaidi ya 1000 wewe unasema corona haipo Marekani, au ndo wazee wa conspiracy theories.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamesisitiza Kabisa kuwa Must return to US now. Na hii wameitangaza leo ila walishaanza kuwalazimisha raia wake waondoke Tanzania. Huu ugonjwa ni hatari halafu imagine uupate ukiwa Tanzania where our medical system is very poor. Hata kama ni mimi nina option ya kuondoka I will surely do so.

Something is not right somewhere.... Only great thinkers can understand.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwani kwetu huwezi kupata maji ya moto ukaweka kipande cha limau ukanywa au ukala machungwa kwa wingi,sema wenzetu ni wavivu wa kula matunda!!!!
 
huu ni uthibitisho tosha kuwa corona marekani haipo, au uenda kuendelea kubaki tanzania ni hatari zaidi ya kuwa na ugonjwa huu ukiwa united state of american

Yaani WHO, dunia inatangaza kila siku halafu anatokea mtu mmoja kutoka Tanzania anakubali Corona haipo Marekani, acheni kusujudia watu kila saa kwenye kila kitu mzee, tuliza akili.

Au taarifa zinazotolewa na Trump mwenyewe kuhusu hali ya Corona nchini mwake huwa hauzisikii, basi tufanye ile siyo Corona bali ni homa ya Dengue
 
huu ni uthibitisho tosha kuwa corona marekani haipo, au uenda kuendelea kubaki tanzania ni hatari zaidi ya kuwa na ugonjwa huu ukiwa united state of american
Hivi upstair kwako kuko vizuri kweli?
Marekani ndio inaongoza kwa kuwa na case nyingi sasa hivi.

Nikupe ukweli:
Marekani anaona Serikali yetu haipo serious.
Inadanganya data na hakuna step yoyote inayochukuliwa.
Kwa hio wameshaona kuwa hili dude litakuja kuua watu hapa hadi kila mtu atashangaa
 
Back
Top Bottom