Ubalozi wa Marekani Dar wanusurika kulipuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubalozi wa Marekani Dar wanusurika kulipuliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RayB, May 18, 2010.

 1. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ubalozi Wa Marekani DSM Chupuchupu
  Ubalozo wa Marekani nchini umenusurika kulipuliwa na mwanafunzi wa shule ya msingi anayedaiwa kuhamasishwa na mafunzo aliyopewa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda.

  Taarifa kutoka ndani ya ubalozi huo, zimeeleza kuwa kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, hivi sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam.

  Habari zilisema mwanafunzi huyo mwenye umri wa kati ya miaka 15 na 17, alifanikiwa kuingia ndani ya ubalozi huo Jumapili iliyopita saa tatu usiku, akiwa na vifaa alivyotaka kutumia kufanyia ulipuaji huo.

  source: Father Kidevu
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  UBALOZI wa Marekani Dar es Salaam umenusurika kulipuliwa.

  Mwanafunzi wa shule ya msingi anayedaiwa kuhamasishwa na mafunzo aliyopewa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda amekiri kutaka kuulipua.

  Taarifa kutoka ndani ya ubalozi huo, zimeeleza kuwa kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake, amekamatwa, yupo katika kituo cha polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

  Habari zinadai kuwa,mwanafunzi huyo mwenye umri wa kati ya miaka 15 na 17 aliingia ndani ya ubalozi huo Jumapili iliyopita saa tatu usiku, akiwa na vifaa alivyotaka kutumia kufanyia ugaidi huo.

  Inadaiwa alikuwa na dumu la lita tano la mafuta ya taa, utambi na kiberiti cha gesi.

  Kwa mujibu wa chanzo cha habari, baada ya kuingia ndani ya ubalozi huo, alikwenda moja kwa moja kwenye tangi linalohifadhi zaidi ya lita 1,000 za dizeli kwa nia ya kulilipua.

  Habari zilidai kuwa, kijana huyo alipoingia ndani ya ubalozi huo akipitia geti namba tatu ubalozini hapo, walinzi walikuwa wamelala.

  Alipolifikia tangi hilo, kijana huyo anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Mtambani wilayani Kinondoni, alijaribu kufungua koki za tangi hilo kwa nguvu na kuwaamsha walinzi hao usingizini.

  Walinzi walimkamata na baada ya kumhoji, alikiri kuingia katika ubalozi huo kihalifu akitaka kuulipua, hatua ambayo ingesababisha mshituko mkubwa kama wa asubuhi ya Agosti 7, 1998, ubalozi huo ulipolipuliwa na kuua watu kadhaa wakiwamo Watanzania na Wamarekani.

  Kijana huyo alidai kuwa yeye na wenzake wapatao 15 walipatiwa mafunzo kwa njia ya video na mtandao huo, kwa ajili ya maandalizi ya kuulipua ubalozi huo Juni mwaka huu.

  Alidai baada ya kuhamasika na mafunzo hayo, yeye na mwenzake aliyekuwa amemwacha katika eneo linalotumika kuuzia maua karibu na ubalozi huo, walikwenda kujaribu kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo.

  Taarifa zilisema walinzi hao walimpeleka kijana huyo katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, ambako anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

  Ofisa Habari wa habari katika Ubalozi wa Marekani nchini, Halima Mbaruku, alithibitisha kuwapo kwa jaribio alilosema ni la kuuchoma moto ubalozi, lakini akasema kwa sasa hauko katika nafasi ya kulizungumzia, kwa kuwa polisi wanalifanyia uchunguzi.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa kuhusu tukio hilo, hakutaka kulizungumzia zaidi ya kusema yeye hayuko Kinondoni.

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtambani, Daudi Mwinyijuma, alipoulizwa kuhusu habari hiyo, alitaka atajiwe kwanza jina la mwanafunzi huyo, ili afuatilie, lakini hakuna mtu aliyekuwa tayari kumtaja mshukiwa huyo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, kwani simu yake ilikuwa haipatikani.

  Agosti saba mwaka 1998, balozi mbili za Marekani katika Afrika Mashariki; wa Tanzania na Kenya, zililipuliwa kwa kipindi cha muda mfupi ambapo jumla ya watu 258 waliuawa na wengine 5,000 walijeruhiwa.

  Kwa ubalozi wa Dar es Salaam, gari lenye milipuko lilifika asubuhi ulipokuwa ubalozi huo barabara ya Laibon na kutaka kuingia katika moja ya malango na kuzuiwa na lori la maji lililokuwa linamilikiwa na ubalozi huo.

  Ilipofika saa 4.39 gari hilo lilifyatua mlipuko kutoka umbali wa meta zipatazo 35 nje ya ukuta wa ubalozi na kusababisha vifo na majeruhi.

  Watanzania waliopoteza maisha yao katika shambulizi hilo la kigaidi ni Abdulahaman Abdulah, Elisha Paulo, Elia Hassan, Siyad Harane, Ramadhani Mahundi, Mtendeje Rajabu na Mbegu Abdallah.

  Wengine ni Mohamed Abas, William Mwila, Almosaria Yussuf, Mzee Shamte, Yusuph Ndale Bakari, Yusuph Nyumbo na Dotto Seleman.

  Katika kujibu mashambulizi hayo, Serikali ya Rais Bill Clinton wakati huo, ilishambulia kituo cha mafunzo cha Afghanistani na kiwanda cha dawa cha Khartoum Sudan, ambacho kinadaiwa kutengeneza gesi inayotumika kulipulia mabomu.

  Mashambulizi hayo yalidaiwa kufadhiliwa na Osama bin Laden, ambaye anaaminika kuendesha mtandao wa ugaidi dhidi ya Marekani.

  HabariLeo | Ubalozi wa Marekani Dar wanusurika kulipuliwa
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mungu wangu tena!:painkiller::painkiller::painkiller:
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  walinzi wamelala?.............wafungwe hao kwanza :mad:
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,442
  Likes Received: 81,491
  Trophy Points: 280
  Lahaula! Bora hakufanikiwa maana kama angefanikiwa basi mlipuko huo ungezidi kuitia doa Tanzania yetu
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sounds fishy to me.
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Mlinzi anayelala si mlinzi. Hivi na security systems zote kama alarm, CCTV (ingawaje aliyekuwa kwenye CCTV alikuwa amelala) vilikuwa na vyenyewe vimelala? Hawa watoto wamehamasishwa na aidha wazazi, waalimu wao wa madrasa surati, na video show zinazooneshwa kwenye vibanda huko uswahilini; pia alQaida vile vile - kama huko kwao wanatumia watoto kwa nini isiwe huku. Pia itakuwa 'inside job' kwani huyu mtoto alijuwaje kama kuna hicho kisima cha mafuta?

  Hawa ndio wanaochoma nyumba nyingine za watu na mabweni ya mashule na tunajikuta tunahofia TANESCO na vifaa vya umeme vya kichina ukute kumbe sio! Wamarekani waweke walinzi wao pia. Ila huwa naona kuna FFU pia, ni wa mchana tu? Au usiku pia? Nao walikuwa wamelala?
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  duh! jamaa wanafundisha watoto kufanya ugaidi (wameshafundisha 15), na bado watu wanaunga mkono eti ni vita dhidi ya US upuuzi huu. Mashehe wafanyekazi ya makusudi kuwaelimisha vijana wao ubaya wa chuki na uzuri wa upendo. Biblia inasema mpende adui yako.
   
 9. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kaazi kwer kwer
   
 10. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Huyo mtoto alivunja geti? Yaani hata usiku halihitaji mtu akufungulie ndio uingie?
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  I thought Ubalozi wa USA una ulinzi kuzidi hata Ikulu? Kumbe hata mtoto wa below 17 years anaweza ku-break in bila walinzi kutambua? Looks like story ya kusadikika!
   
 12. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I dont buy this........
   
 13. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli! Hapo hakuna walinzi!:angry:
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Me either! Too sensational to be true! Mafuta ya taa? Utambi?
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi ninavyoijua Marekani huyo mtoto asingepelekwa kituo cha polisi badala yake wangemtait mule mule ndani ya ubalozi wao kwani mule ni zaidi ya kambi ya jeshi.
  Mmh! hii stori!!
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yaani saa hizi tayari angekuwa Guantanamno badala ya OB police station? Why didnt they do that/ kwani wameshawahi kuwapeleka kule vijana chini ya miaka 16!
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nisaidieni! Nimejaribu ku-browse the web for this piece of news nime-draw blank. Labda kuna mtu anaweza kusaidia?
   
 18. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  April Fools!
   
 19. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Mwanaume wa miaka 17 ni mkubwa sana kwenye ulimwengu wa kijeshi,akiwa well trained anaweza kuwa komandoo,na akafanya lolote.sema hata hiyo habari yenyewe haijitoshelezi
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  si tueambiwa source ni habari leo au?
   
Loading...