Haaahaaa mpango mzimaaa!
Halafu Marvel's Luke Cage mbona imetoka hadi episode ya 11.
Hujaiona tu mkuu?
Hebu itafute.
Haya turudi kwenye mada yetu.
Denzel Washinton alitakiwa aigize filamu inaitwa Hannibal kama Hannibal mwenyewe.
Wazungu wakapinga hadi leo imewekwa kapuni, kisa Hannibal hakuwa mweusi.
Sasa Mwafrika wa Carthage alikuwaje mweupe hawataki kujibu hadi leo.
Miaka ya 80 na 90 weusi walishika sana soko la muziki la Marekani.
Ikafika hadi kipindi wazungu wakawa wanaongea kama weusi, wanavaa kama weusi na kutamani sana kuwa weusi.
Hata ukiangalia matamasha ya Marvin Gaye, Billy Ocean, Michael Jackson, Nina Simone na wengine,
Wazungu walikuwa wanajaa sana, ubaguzi ulianza kuyeyuka. America was at its peak thanks to Ronald Reagan.
Lakini hili jambo kuna watu halikuwafurahisha kabisa hivyo mweusi akaanza kuminywa kidogo kidogo hadi wakapoteana.