Ubaguzi kati ya CCM, CUF wahamia kisiwani Unguja

mazrui.jpg

Katibu mkuu wa CUF Zanzibar, Ali Ahmed Mazrui.
By Bakari Kiango, Mwananchi; bkiango@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani kwa maelezo kuwa sheria na kanuni zilikiukwa, jambo ambalo CUF ililipinga ikisema uchaguzi ulikuwa huru na haki na waangalizi wote walithibitisha hilo.
Zanzibar. Vitendo vya kibaguzi ambavyo vimetawala kisiwani Pemba tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio, sasa vimeanza kuonekana maeneo ya vijijini kisiwani Unguja.

Hali ya kubaguana imekuwa ikikua tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio ulioipa CCM ushindi kwenye visiwa vyote viwili baada ya CUF kuususia kutokana na kutokubaliana na kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika Machi 20, hali ya kutoelewana miongoni mwa wananchi imekuwa ikitawala kwenye kisiwa cha Pemba, ambako ni ngome ya CUF. Wananchi wamekuwa wakibaguana kwenye vyombo vya usafiri, elimu, misikitini na kwenye biashara.

Hivi karibuni Mwananchi, iliandika makala kuhusu hali ya ubaguzi kwenye kisiwa cha Pemba, ikizungumza na wananchi na viongozi ambao walithibitisha kuwa ubaguzi unazidi kukua na kuvitaka vyama vya siasa kuzungumza na wanachama wao ili kuondoa hali hiyo.

Mwananchi imebaini kuwa hali hiyo ya ubaguzi imeanza kusambaa pia maeneo ya vijijini kisiwani Unguja.

“Kile kinachotokea Pemba ni cha mtoto. Hapa Unguja, kuna fukuto linafukuta chini kwa chini,” alisema naibu katibu mkuu wa CUF Zanzibar, Ali Ahmed Mazrui.

“Ipo siku litaibuka baya maana ni kama bomu. Kwa sababu wananchi bado wana donge rohoni.”

Mwananchi iliyotembea maeneo ya Nungwi, Mkokotoni na Matemwe yaliyoko Kaskazini Unguja, takribani kilomita 30 kutoka mjini ilishuhudia vitendo hivyo.

Mwananchi ilitembelea Mkokotoni ambako kuna usafiri wa boti au mashua za kuvuka kwenda Tumbatu na kuongea na wananchi ambao walithibitisha kuwepo kwa vitendo vya kubaguana.

“Ukitaka kwenda upande wa pili (Tumbatu) kama wewe ni mgeni, utapanda chombo chochote kiwe cha CUF au CCM, lakini kama wewe ni CCM au CUF itakupasa upande chombo cha wafuasi wenzako,” alisema kada wa CCM, aliyejitambulisha kwa jina Said Shaali.

“Mbaya zaidi, watu hawa (CUF) wameingiza siasa za chuki hadi katika misiba, hatushirikiani. Kuna siku mwanangu alifukuzwa na CUF kama mbwa alipokwenda kushiriki msiba wa rafiki yake kisiwani Tumbatu,” alisema Shaali.

Alisema hali hiyo ilianza kujitokeza baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mwaka jana, akidai kuwa wafuasi wa CUF walianzisha chuki dhidi ya wenzao wa CCM.

Ally Khatibu Juma, ambaye alisema ni nahodha wa boti inayosafirisha abiria kati ya Tumbatu na Mkokotoni, alisema si lazima kila mtu apande boti yake.

“Kila boti ina bendera ya chama, mimi yangu inapeperusha bendera ya CUF. Kamwe sitakuja kubeba mtu wa CCM. Ni bora niende na abiria wawili,” alisema Juma.

Alisema hata viongozi wa Serikali wakienda Tumbatu kupeleka msaada, haupokelewi.

“Viongozi wa Serikali wasijisumbue kutuletea msaada,” alisema.

“Siku moja mwakilishi wa jimbo la Tumbatu (CCM), Haji Omar Kheir alimtuma mtu aje atuletea tende katika misikiti mitatu, tulimkatalia kwa sababu ni haramu kwetu.”

Kauli hiyo ya Shaali ilithibitishwa na katibu wa CCM wa Wilaya ya Unguja Mjini, Baraka Shamte ambaye alisema baadhi ya misikiti ilikataa tende zilizopelekwa na Kheir ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Vikosi vya SMZ na Idara Maalumu.

Alisema kitendo kinachofanywa na CUF si kizuri na kwamba anashangaa kwanini mamlaka husika haioni mambo hayo ili chama hicho kichukuliwe hatua za kisheria kwa uvunjifu wa haki za binadamu.

Nungwi

Hali ni tofauti kwenye eneo la Nungwi ingawa kuna dalili za ubaguzi kuanza kuingia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafuasi wa CUF wanaoishi Nungwi walisema kamwe hawawezi kumsamehe Jecha kwa kitendo chake cha kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

“Hatutamsamehe Jecha kwa kitendo chake cha kuzima ndoto ya chama chetu kupata kiongozi ambaye ni chaguo la watu (Maalim Seif),” alisema Sharif Ali Sharif.

Sharif alisema chama hicho, hakina mpango wa kufanya vurugu kama watu wanavyodhani, ila njia sahihi wanayoitumia ni kutoshirikiana na watu wa CCM kuanzia Serikali hadi wanachama wake.

Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ilimaliza matatizo ya Wazanzibari, lakini Jecha akishirikiana na Serikali wamefanya kila liwezekanalo kuhakikisha Maalim Seif anakwaa kisiki katika uchaguzi uliopita. “Wakitaka mkakati uishe ni haki kutendeka na haki yenyewe itendeke kwa Maalim Seif kuwapo madarakani na si vinginevyo,” alisema Sharif.

Lakini mjumbe mmoja katika uongozi wa Shehia ya Nungwi alisema wafuasi wa vyama hivyo viwili sasa wanashirikiana kwenye shughuli za kijamii.

Sheha huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Khatib Kombo Bakari, alisema ikitokea msiba au sherehe wafuasi wa CCM hujumuika pamoja na wenzao wa CUF bila tatizo lolote.

“Hapa hakuna suala kama hili,” alisema lakini akaonya: “Ila kuna watu wanataka kuiga mkakati huo ulioanza katika maeneo mengine.”

Alisema kuna baadhi ya watu wanataka kuiga mkakati huo, lakini bado hawaungwi mkono na wenzao na hadhani kama watafanikiwa.

Wakizungumzia kauli hizo, wanachama wa CUF walisema makada hao wanaogopa kusema ukweli kwa kuhofia kushughulikiwa na viongozi wa ngazi ya juu.

“Kwanza hii ni ngome ya CUF. Kwa hiyo mkakati huu upo na wasijisumbue hata kuja kuoa kwetu hatuwapi mke na waende wakawaoe CCM wenzao,” alisema Mwakahanzi Juma.

Aliongeza kuwa msiba ukitokea CCM wanakuwa mstari wa mbele kuhudhuria lakini wanachama wa CUF hawaridhiki badala yake wanaamua kuwatenga na mwisho wa siku wenyewe wanajisikia aibu na kuondoka eneo hilo.

Pemba ubaguzi balaa

Wakati hali ikianza kujitokeza kisiwani Unguja, ubaguzi unazidi kukua Pemba.

Shehia ya Kigomani, eneo la Matemwe, Hobe Juma Simai alisema CUF wanaendesha mpango huo wa kubaguana, lakini akasema hauna tija zaidi ya kurudisha nyuma maendeleo. “Dai lao kubwa ni kwamba wamedhulumiwa haki yao. Ndiyo maana wakifika msikitini wakimuona imamu anayeswalisha ni CCM wanagoma kuswali.

“Mimi nawasihi warudi ili tuwe kitu kimoja na tushirikiane kwa maendeleo ya Shehia ya Kigomani na sehemu nyingine,” alisema Simai.

Hata hivyo, baadhi ya wafuasi wa CUF wanaoishi Kigomani walipinga kauli ya Simai ya kuwataka kuwa kitu kimoja na badala yake walisema hawatarudi nyuma.

Wafuasi hao walisisitiza kuwa endapo wakishirikiana na CCM watakuwa wamewasaliti wenzao kwa kuwa dhuluma wanayodai ilifanyiwa na CCM ni kubwa.

“CCM wanajisumbua, CUF hatutarudi nyuma, ndiyo maana sasa sasa hivi tunaswali kivyetu vyetu katika misikiti na tumeshajipangia ratiba waanze wao au sisi kuswali,” alisema Ramadhan Tano.

Mkazi mwingine wa Kigomani, Mcha Abdulrahman Kundi alisema si katika ibada hata kwenye masoko wakiona anayenadi bidhaa ni mtu wa CCM, hawampi ushirikiano.

“Wenyewe wanapenda sana tushirikiane, lakini sisi hatutaki. Kwa sababu ya dhuluma waliyotufanyia mwaka jana kupitia kwa Jecha Salum,” alisema Kundi.

Chanzo Wananchi
 
Hiyo inaitwa mfa maji

Wanaotapatapa ni madikteta wa SMZ na mazombi yao! Maana fimbo wanayochapiwa sasa kwa muungwana lazima arudi nyuma.

Watu wameligomea meli lao sasa wanafikiria kulipaki kwenye nanga, watu wamesusa kuwauzia karafuu zao sasa soko liko Mombasa Kenya.

Mazombi hata yanapofikwa na msiba yanafukiana yenyewe, hayauziwi kitu au vya kwao kununuliwa.

Mazombi waliyapanda haya sasa waache wavune matunda yao maana muungwana Amani Karume alijitahidi kuyaondoa haya yote lakini watwana wameyarudisha kwa nguvu.
 
Eee Mungu muumba wa vyote tupe MOYO wa SUBIRA na UVUMILIVU tuvuke salama kipindi hiki cha MAPITO. we Mola ndiye upangaye na kuyamaliza yote busara na hekima zako zisizomithilika.

Ni upumbavu uliovuka viwango vya upumbavu kumhusisha Mungu katika majanga mliyoyatengeneza wenyewe.Tukiweka itikadi za kisiasa pembeni na kuyaangalia mambo haya kwa jicho la ukweli ni nani asiyejuwa kuwa ccm na serikali yake ndiyo chanzo cha misuguano hii ya kijamii inayoendelea Zanzibar?

Nani kati ya Mwanaccm awezaye kwenda mbele za Mungu na kushuhudia kuwa ccm haikufanya hila katika matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar?Ni kiongozi gani hasa huko ccm na serikalini awezaye kujishika kifuani huku mkono mmoja ukishika kitabu kitakatifu kisha aungame kwa dhati kabisa kuwa ccm ilishinda Zanzibar?

Msiwalazimishe watu waitwe wachochezi kwa uchu wenu wa nadaraka.Serikali yetu haina dini,lakini viongozi wakuu wa serikali wana dini na wanamuamini Mungu,Je Rais anaweza kwenda mbele ya "Madhabahu ya Bwana" na kuthibitisha pasi na shaka kuwa ccm ilishinda Zanzibar?Anaweza kukisogelea kiti cha hukumu na kukiri kuwa ccm ilishinda Zanzibar?

Mkome kumuhusisha Mungu katika uhalamia wenu wa kupora haki ya wananchi wanyonge walioamua kutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi wanaowataka,lakini kwa kiburi cha dola serikali ikaipora haki yao.

Leo hii tunashuhudia usanii wa kiimani wa viongozi wetu wakijifanya wanawafuturisha watu huku wakijuwa fika kuwa viti vyao walivyokalia ikulu vipo juu ya migongo ya wananchi wa Taifa hili waliowapora haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.Ni unafiki kuisogelea Nyumba ya ibada huku mikono yako ikimwagika damu ya haki za Watanzania uliowapora haki zao za kikatiba.

Mkome kumuhusisha Mungu wetu wa Haki,bila aibu wala soni kiongozi anasimama na kuomba tumuombee,tumuombee kwa nani wakati Mungu wetu tunayemuamini hafungamani na dhurma za wazi wazi zifanywazo na serikali katika kupora Demokrasia?Si wana midomo na vifua waombe wenyewe kwa mungu wanayeamini atawabariki huku miguu yao ikiendelea kukanyaga haki za msingi za Raia.Hatutaki kuhusishwa kwenye dhihaka ya kumdhihaki Mungu,wanaimani zao,wamsogelee wenyewe wamuombe huyo "mungu wao anayeruhusu udharimu kwa waja wake"

Msifikiri sote mlitukata vichwa na kututwisha maboga yasiyoweza kufikiri na kupambanua mambo,tulishiriki katika hatua zote za uchaguzi,tuliona kwa macho yetu namna uchaguzi ulivyoendeshwa kimizengwe na kushuhudia mambo mengi ambayo hata mkitulazimisha tuyaamini kwa nguvu za kidola hatuwezi kuyaamini badala yake tutabaki kimya tu kuulinda uhai wetu,sasa ukimya wetu usichukuliwe kuwa ni imani yetu kwa serikali,ukimya wetu unatokana na woga tu na si kwamba tunaiamini serikali.

Tena ukome kabisa,kama umevimbiwa na viwavijeshi wa Lumumba,endelea kuvifakamia kimya kimya bila kumuhusisha Mungu na udhalimu wenu.Usitulazimishe tuitwe wachochezi,hatutaweza kunyamanza huku Mungu wetu mpenda haki tunayemuamini Akiendelea kuhusishwa na udhalimu wa dola lililong'ang'ania madaraka.

Bora niitwe mchochezi kwa kuitetea imani,kuliko kukaa kimya na kuwasikiliza wadhalimu wakimkejeli Mungu kwa kuomba waombewe wakati miguu yao imesimama juu ya haki za msingi za kiraia,ishieni huko huko na ufedhuri wenu,pumbavu.
 
Bara huo upuuzi hauji tokea,watu wanawaza kutafuta rizki,habari ya siasa hatuhitaji,uchaguzi ushamalizika.Kama kuna aliyeshinda kihalali sawa,aliyedhulumiwa asubiri uchaguzi ujao.
Lakini umaskini uko kote bara na visiwani. Kinachotakiwa kufanya siasa safi kila mtu apate haki tupambane na umaskini
 
Bara huo upuuzi hauji tokea,watu wanawaza kutafuta rizki,habari ya siasa hatuhitaji,uchaguzi ushamalizika.Kama kuna aliyeshinda kihalali sawa,aliyedhulumiwa asubiri uchaguzi ujao.
kwani pemba na unguja walitegemea huu upuuzi utakuja kutokea? haya mambo mnaya'generate' wenyewe nyinyi LUMUMBA si suala la kuleta viroja hapa.
 
Eee Mungu muumba wa vyote tupe MOYO wa SUBIRA na UVUMILIVU tuvuke salama kipindi hiki cha MAPITO. we Mola ndiye upangaye na kuyamaliza yote busara na hekima zako zisizomithilika.
Mkuu maombi pekee kwenye keyboard hayasaidii pambana na kimatendo kukemea hili suala la hawa wakoloni weusi CCM.
 
Zanzibar. Vitendo vya kibaguzi ambavyo vimetawala kisiwani Pemba tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio, sasa vimeanza kuonekana maeneo ya vijijini kisiwani Unguja.

Hali ya kubaguana imekuwa ikikua tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio ulioipa CCM ushindi kwenye visiwa vyote viwili baada ya CUF kuususia kutokana na kutokubaliana na kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani kwa maelezo kuwa sheria na kanuni zilikiukwa, jambo ambalo CUF ililipinga ikisema uchaguzi ulikuwa huru na haki na waangalizi wote walithibitisha hilo.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika Machi 20, hali ya kutoelewana miongoni mwa wananchi imekuwa ikitawala kwenye kisiwa cha Pemba, ambako ni ngome ya CUF. Wananchi wamekuwa wakibaguana kwenye vyombo vya usafiri, elimu, misikitini na kwenye biashara.

Hivi karibuni Mwananchi, iliandika makala kuhusu hali ya ubaguzi kwenye kisiwa cha Pemba, ikizungumza na wananchi na viongozi ambao walithibitisha kuwa ubaguzi unazidi kukua na kuvitaka vyama vya siasa kuzungumza na wanachama wao ili kuondoa hali hiyo.

Mwananchi imebaini kuwa hali hiyo ya ubaguzi imeanza kusambaa pia maeneo ya vijijini kisiwani Unguja.

“Kile kinachotokea Pemba ni cha mtoto. Hapa Unguja, kuna fukuto linafukuta chini kwa chini,” alisema naibu katibu mkuu wa CUF Zanzibar, Ali Ahmed Mazrui.

“Ipo siku litaibuka baya maana ni kama bomu. Kwa sababu wananchi bado wana donge rohoni.”

Mwananchi iliyotembea maeneo ya Nungwi, Mkokotoni na Matemwe yaliyoko Kaskazini Unguja, takribani kilomita 30 kutoka mjini ilishuhudia vitendo hivyo.

Mwananchi ilitembelea Mkokotoni ambako kuna usafiri wa boti au mashua za kuvuka kwenda Tumbatu na kuongea na wananchi ambao walithibitisha kuwepo kwa vitendo vya kubaguana.

“Ukitaka kwenda upande wa pili (Tumbatu) kama wewe ni mgeni, utapanda chombo chochote kiwe cha CUF au CCM, lakini kama wewe ni CCM au CUF itakupasa upande chombo cha wafuasi wenzako,” alisema kada wa CCM, aliyejitambulisha kwa jina Said Shaali.

“Mbaya zaidi, watu hawa (CUF) wameingiza siasa za chuki hadi katika misiba, hatushirikiani. Kuna siku mwanangu alifukuzwa na CUF kama mbwa alipokwenda kushiriki msiba wa rafiki yake kisiwani Tumbatu,” alisema Shaali.

Alisema hali hiyo ilianza kujitokeza baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mwaka jana, akidai kuwa wafuasi wa CUF walianzisha chuki dhidi ya wenzao wa CCM.

Ally Khatibu Juma, ambaye alisema ni nahodha wa boti inayosafirisha abiria kati ya Tumbatu na Mkokotoni, alisema si lazima kila mtu apande boti yake.

“Kila boti ina bendera ya chama, mimi yangu inapeperusha bendera ya CUF. Kamwe sitakuja kubeba mtu wa CCM. Ni bora niende na abiria wawili,” alisema Juma.

Alisema hata viongozi wa Serikali wakienda Tumbatu kupeleka msaada, haupokelewi.

“Viongozi wa Serikali wasijisumbue kutuletea msaada,” alisema.

“Siku moja mwakilishi wa jimbo la Tumbatu (CCM), Haji Omar Kheir alimtuma mtu aje atuletea tende katika misikiti mitatu, tulimkatalia kwa sababu ni haramu kwetu.”

Kauli hiyo ya Shaali ilithibitishwa na katibu wa CCM wa Wilaya ya Unguja Mjini, Baraka Shamte ambaye alisema baadhi ya misikiti ilikataa tende zilizopelekwa na Kheir ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Vikosi vya SMZ na Idara Maalumu.

Alisema kitendo kinachofanywa na CUF si kizuri na kwamba anashangaa kwanini mamlaka husika haioni mambo hayo ili chama hicho kichukuliwe hatua za kisheria kwa uvunjifu wa haki za binadamu.

Nungwi

Hali ni tofauti kwenye eneo la Nungwi ingawa kuna dalili za ubaguzi kuanza kuingia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafuasi wa CUF wanaoishi Nungwi walisema kamwe hawawezi kumsamehe Jecha kwa kitendo chake cha kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

“Hatutamsamehe Jecha kwa kitendo chake cha kuzima ndoto ya chama chetu kupata kiongozi ambaye ni chaguo la watu (Maalim Seif),” alisema Sharif Ali Sharif.

Sharif alisema chama hicho, hakina mpango wa kufanya vurugu kama watu wanavyodhani, ila njia sahihi wanayoitumia ni kutoshirikiana na watu wa CCM kuanzia Serikali hadi wanachama wake.

Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ilimaliza matatizo ya Wazanzibari, lakini Jecha akishirikiana na Serikali wamefanya kila liwezekanalo kuhakikisha Maalim Seif anakwaa kisiki katika uchaguzi uliopita. “Wakitaka mkakati uishe ni haki kutendeka na haki yenyewe itendeke kwa Maalim Seif kuwapo madarakani na si vinginevyo,” alisema Sharif.

Lakini mjumbe mmoja katika uongozi wa Shehia ya Nungwi alisema wafuasi wa vyama hivyo viwili sasa wanashirikiana kwenye shughuli za kijamii.

Sheha huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Khatib Kombo Bakari, alisema ikitokea msiba au sherehe wafuasi wa CCM hujumuika pamoja na wenzao wa CUF bila tatizo lolote.

“Hapa hakuna suala kama hili,” alisema lakini akaonya: “Ila kuna watu wanataka kuiga mkakati huo ulioanza katika maeneo mengine.”

Alisema kuna baadhi ya watu wanataka kuiga mkakati huo, lakini bado hawaungwi mkono na wenzao na hadhani kama watafanikiwa.

Wakizungumzia kauli hizo, wanachama wa CUF walisema makada hao wanaogopa kusema ukweli kwa kuhofia kushughulikiwa na viongozi wa ngazi ya juu.

“Kwanza hii ni ngome ya CUF. Kwa hiyo mkakati huu upo na wasijisumbue hata kuja kuoa kwetu hatuwapi mke na waende wakawaoe CCM wenzao,” alisema Mwakahanzi Juma.

Aliongeza kuwa msiba ukitokea CCM wanakuwa mstari wa mbele kuhudhuria lakini wanachama wa CUF hawaridhiki badala yake wanaamua kuwatenga na mwisho wa siku wenyewe wanajisikia aibu na kuondoka eneo hilo.

Pemba ubaguzi balaa

Wakati hali ikianza kujitokeza kisiwani Unguja, ubaguzi unazidi kukua Pemba.

Shehia ya Kigomani, eneo la Matemwe, Hobe Juma Simai alisema CUF wanaendesha mpango huo wa kubaguana, lakini akasema hauna tija zaidi ya kurudisha nyuma maendeleo. “Dai lao kubwa ni kwamba wamedhulumiwa haki yao. Ndiyo maana wakifika msikitini wakimuona imamu anayeswalisha ni CCM wanagoma kuswali.

“Mimi nawasihi warudi ili tuwe kitu kimoja na tushirikiane kwa maendeleo ya Shehia ya Kigomani na sehemu nyingine,” alisema Simai.

Hata hivyo, baadhi ya wafuasi wa CUF wanaoishi Kigomani walipinga kauli ya Simai ya kuwataka kuwa kitu kimoja na badala yake walisema hawatarudi nyuma.

Wafuasi hao walisisitiza kuwa endapo wakishirikiana na CCM watakuwa wamewasaliti wenzao kwa kuwa dhuluma wanayodai ilifanyiwa na CCM ni kubwa.

“CCM wanajisumbua, CUF hatutarudi nyuma, ndiyo maana sasa sasa hivi tunaswali kivyetu vyetu katika misikiti na tumeshajipangia ratiba waanze wao au sisi kuswali,” alisema Ramadhan Tano.

Mkazi mwingine wa Kigomani, Mcha Abdulrahman Kundi alisema si katika ibada hata kwenye masoko wakiona anayenadi bidhaa ni mtu wa CCM, hawampi ushirikiano.

“Wenyewe wanapenda sana tushirikiane, lakini sisi hatutaki. Kwa sababu ya dhuluma waliyotufanyia mwaka jana kupitia kwa Jecha Salum,” alisema Kundi
Siyo huko tu hata huku bara hali hiyo tayari imepiga hodi
 
Pamoja na kwamba nina laani sana tukio alilolifanya Jecha but inapofikia suala la IMANI nasita sana kusema sitasali IBADA itakayo salishwa na mwana chama pinzani wa chama changu. Sijui labda kwa vile siijui sana IMANI ya kiislamu; kwenye UKRISTO suala la kumchukia tu mtu linatosha kabisa kukupeleka motoni so is either uachane na mambo ya kusali ili uendeleze chuki au uachane na kanisa la huyo mchungaji/padre na kuhamia kanisa linguine linalo fanana mlengo na wewe au la USAMEHE ili maisha yaendelee mbele. Hili la kusamemhe nadhani ndio pia ambalo ccm wanalipenda zaidi, wanawakosea watu cause wanajaua watasamehewa. All in All, viongozi wa nchi, fanyieni kazi hotuba ya Lema kwenye bunge la mwezi February; huyu mtu bado nitaendelea sana kumuheshimu kwa kauri zake thabiti kabisa.
 
kwa mambo yaliyofanyika mwaka jana uchaguzi wa zanzibar ubaguzi ni lazima..
 
Huo ubaguzi haukuanza leo tatizo la waarabu ndio waliolianza wao wanarudia tu hakuna cha ajabu!
 
Binapsi sioni sababu ya msingi wananchi kubaguwana,Dini zote hazikubali waumini wao kubaguwana achilia mbali vyama vya siasa,huu ni zaidi ya unyama,nadhani iko uaja viongozi wa kisiasa wanaohamasisha wanachi kubaguana ni lazima wachukuliwe hatua kali kwani sio jambo zuri na kwanini iwe cuf tu iwabaguwe wenzao?sidhani km chama hiki kinastahiki kupewa nchi kuongoza naamini kitayafanya makubwa kuliko hayo
 
Back
Top Bottom