Ubaguzi CRDB

Ubaguzi CRDB

Joined
Jan 2, 2013
Posts
31
Reaction score
5
Wanajamvi kuna ubaguzi wa wazi CRDB kwenye suala la kukodisha nyumba za watu binafsi kwa ajili ya kufungua matawi mapya hususan huku Kanda ya Ziwa.

Ndio mana baadhi ya wilaya huku wanatumia Mobile ATM (yale magari yenye atm). Mameneja wao huku kanda ya ziwa wanajitahidi kutafuta nyumba kwa ajili ya matawi, wanaingia makubaliano ya mwanzo na taarifa zinatumwa makao makuu ili waridhie ufungwe mkataba rasmi. Chaajabu makao makuu wakiona jina la mmiliki wa nyumba hilielekei kuwa mcha......a(kabila moja maarufu la kaskazn linalomiliki hii nchi

Huo ni mkakati wa mkurugenzi mkuu wao kutaka kuneemesha watu wa kwao tu) unarudishiwa majibu kwamba haiwezekani kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.

Iligundulika dec 2012 sababu ya kukataa nyumba nyingi baada ya mpangishaji mmoja kuamua fuatilia ngazi ya mkoa na kupewa jibu la wazi na kweli na meneja.. wewe siyo mcha.............a kamwe hututapangisha kwako, tunasubiri mwenzetu ajenge ndo tupange, tutaendelea na mobile ATM.
huu ubaguzi unapunguza upanuzi wa Hii Bank (CRDB) huku kanda ya ziwa kwa sababu hao ndugu zake mkurugenzi mkuu hawana nyumba za kuwapangisha baadhi ya wilaya huku lake zone.

Nawasilisha wakuu, kama kawaida kunawatakao anza oh1 umejiunga leo, kwa taarifa yao mimi ni mzoefu humu jamvini,nimefanya hivi kwa sababu ya usalama wangu, nmanake hawa jamaa ndo kila kitu nchi hii.
 
Wewe unashangaa hilo nenda kijijini Marangu wamejenga branch kule wakati kuna mikoa hata hawajajenga.Ajira zenyewe waangalie ni wachaga kwa kwenda mbele.
 
CRDB kuna ubaguzi ktk upangishaji wa nyumba kanda ya ziwa ni tuhuma nzito na hazipaswi kupuuzwa,wengine wanadai hata ktk ajira,kupata ajira au kupata promotion ni lazima uwe wa huko,umeoa au kuolewa na mtu wa huko narudia tena hizi ni tuhuma ambazo wkt mwingine chanzo chake ni majungu na wivu ila wenye mamlaka wazichunguze maana lisemwalo.......Pili nchi inaongozwa na serikali ya CCM na sio hao uliosema wach....
 
Tuwekee mabua ya majibu uliyorudishiwa yenye majibu yasiyo na kichwa au mguu ili tuamini, kikubwa ukiweza ondoa jina lako! Pole kwa kupigwa chini ingawa bado nina mashaka mengi na utafiti wako wa kusikia ... kikubwa acha kulalamika kwa vitu ambavyo hauna ushahidi navyo wa kutosha kwani kama CRDB hawataki kupangisha nyumba yako et co we si m.....ga, then unaweza kuifanyia biashara nyingine!:A S angry:
 
Wewe unashangaa hilo nenda kijijini Marangu wamejenga branch kule wakati kuna mikoa hata hawajajenga.Ajira zenyewe waangalie ni wachaga kwa kwenda mbele.

Hela inafuata hela muzee. Sasa kama Wamarangu wana mihela wasiwekewe tawi wakawekewe Wanyarugusu na vijisenti vyao (Watanzania wengine wana wivu wa kike. source: B.W MKAPA)
 
Tuhuma nzito hizi, na inaonyesha umeandika ukiwa na jazba sana, ndiyo maana sentenso zimekaakaa kiajabuajabu.
Hata hivyo siamini kuwa mtu anaweza kujibiwa Live namna hiyo!...labda una matani naye!

Mkuu mwambie aporomoshe mjengo afu auite "MASSAWE HOUSE" aone kama hatawakodishia. Au na mikataba wanaingia kwa kichagga ili wasiingie mkenge kukodisha kwa "chasaka"?
 
Nepotism ni kitu mbaya sana, hatuwezi endelea kwa kuendekeza ukabila rangi, dini, n.k.

Inawezekana kabisa tatizo hilo lipo kabisa. Lakini kwa upande mwingine hebu fanya analysis kidogo kwa kuangalia idadi ya wanafunzi kwa makabila katika vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu. Jaribu kuangalia wanaohitumu fani ya uhasibu kwa makabila. Sasa ajira automatic ni lazima itaenda kwa huo uwiano.
 
Sio upangishaji nyumba kwa ajili ya kufungua matawi hata kwenye AJIRA pia Wachaga ndio wanapewa kupaumbele kwanza.
Itafanya watu wajilaumu kutokuwa Wachagga sasa.
 
wanajamvi kuna ubaguzi wa wazi CRDB kwenye suala la kukodisha nyumba za watu binafsi kwa ajili ya kufungua matawi mapya hususani huku kanda ya ziwa. ndo mana baadhi ya wilaya huku wanatumia mobile atm (yale magari yenye atm). mameneja wao huku kanda ya ziwa wanajitahidi kutafuta nyumba kwa ajili ya matawi, wanaingia makubaliano ya mwanzo na taarifa zinatumwa makao makuu ili waridhie ufungwe mkataba rasmi. chaajabu makao makuu wakiona jina la mmiliki wa nyumba hilielekei kuwa mcha......a(kabila moja maarufu la kaskazn `linalomiliki` hii nchi (huo ni mkakati wa mkurugenzi mkuu wao kutaka kuneemesha watu wa kwao tu) unarudishiwa majibu kwamba haiwezekani kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.
iligundulika dec 2012 sababu ya kukataa nyumba nyingi baada ya mpangishaji mmoja kuamua fuatilia ngazi ya mkoa na kupewa jibu la wazi na kweli na meneja.. wewe siyo mcha.............a hkamwe hututapangisha kwako, tunasubiri mwenzetu ajenge ndo tupange,tutaendelea na mobile atm.
huu ubaguzi unapunguza upanuzi wa HII BANK (CRDB) huku kanda ya ziwa kwa sababu hao ndugu zake mkurugenzi mkuu hawana nyumba za kuwapangisha baadhi ya wilaya huku lake zone.
nawasilisha wakuu, kama kawaida kunawatakao anza oh1 umejiunga leo, kwa taarifa yao mimi ni mzoefu humu jamvini,nimefanya hivi kwa sababu ya usalama wangu, nmanake hawa jamaa ndo kila kitu nchi hii.

Kanda ya ziwa ni kubwa mno ina maana kuanzia Shinyanga, Mwanza, Musoma, Kagera na siku hizi kuna sijui Sia muyu na Geita zinazogawanya maeneo ya Kanda ya ZIwa na huko Ukanda wa Kusini. Sasa kote huku tatizo ni lile mpaka Wachagga wajenge nyumba ndipo CRDB wafungue matawi? Ni hitimisho lililokosa mantiki maana nanusa harufu ya ubaguzi na sababu za kutunga. Halafu kama lengo lingekuwa ni hilo si mkurugenzi angetoa mikopo ili majengo yajengwe na ndugu zake hao? Haiwezekani matawi yakashindwa funguliwa na hali wateja wapo wa kutosha wa kuhudumiwa na matawi hayo kwa sababu hakuna majengo ya Wachaga. Tupe research areas, size of population
interviewed na ikibidi aina ya watu hao in terms of their education level, profession gender na kabila japo sio muhimu maana contextuosly umekuwa influenced na hilo kwenye bandiko lako
 
CRDB miaka ya 90. Hakuna hata aliyekuwa akiijua kwanza, ilikuwa ni benki iliyodharaulika sana. Kaja Dk.Kimei kaibadilisha sana na kuifanya kuwa benki inayojiendesha kwa faida na kila mtu hapa ni shahidi. Inavyoelekea mtoa uzi ameandika lakini taarifa zake hajazifanyia utafiti. Kweli inawezekana Dk Kimei akawa mchaga lakini akaajiriwa mchaga kwa sifa zake kulingana na mahitaji watu wakaanza kuzusha. Wapo waliomzushia huyu mzee na kashfa kadha wa kadha za rushwa za ngono. Naona hizo zimekosa mashiko wanakuja na za ukabila. Mnyonge mnyongeni...Haki yake mpeni. Bila Dk Kimei CRDB ilikuwa imeshaonekana kimeo tu kwa watanzania enzi za Mwinyi.
 
There is no point of view here ni chuki binafsi tu.mtoa mada chekecha akili yako iendana na mfumo wa kiDIGITALI zaidi!!!
 
Na ndio kabila linaloongoza kwa wizi wa mitihani na upendeleo kuanzia secondary hadi vyuo vikuu. Hasa udaktari muhimbili. Ninao mfano hai
 
Hapana bana kuna watu wa makabila mengine huwa asilimia kubwa hawapo serious na issue za kazi ukiona kabila moja linapendelewa alafu hiyo taasisi inafanikiwa basi ujue jamaa wanamoyo wa kujituma.

Hakuna muujiza crdb wanapiga kazi na kila mtu anaona mengine ni matokeo tu ya kibinadamu na utashi wa mtu mmoja mmoja atakavyo elewa.

Tuache kulalamika.
 
wanajamvi kuna ubaguzi wa wazi CRDB kwenye suala la kukodisha nyumba za watu binafsi kwa ajili ya kufungua matawi mapya hususani huku kanda ya ziwa. ndo mana baadhi ya wilaya huku wanatumia mobile atm (yale magari yenye atm). mameneja wao huku kanda ya ziwa wanajitahidi kutafuta nyumba kwa ajili ya matawi, wanaingia makubaliano ya mwanzo na taarifa zinatumwa makao makuu ili waridhie ufungwe mkataba rasmi. chaajabu makao makuu wakiona jina la mmiliki wa nyumba hilielekei kuwa mcha......a(kabila moja maarufu la kaskazn `linalomiliki` hii nchi (huo ni mkakati wa mkurugenzi mkuu wao kutaka kuneemesha watu wa kwao tu) unarudishiwa majibu kwamba haiwezekani kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.
iligundulika dec 2012 sababu ya kukataa nyumba nyingi baada ya mpangishaji mmoja kuamua fuatilia ngazi ya mkoa na kupewa jibu la wazi na kweli na meneja.. wewe siyo mcha.............a hkamwe hututapangisha kwako, tunasubiri mwenzetu ajenge ndo tupange,tutaendelea na mobile atm.
huu ubaguzi unapunguza upanuzi wa HII BANK (CRDB) huku kanda ya ziwa kwa sababu hao ndugu zake mkurugenzi mkuu hawana nyumba za kuwapangisha baadhi ya wilaya huku lake zone.
nawasilisha wakuu, kama kawaida kunawatakao anza oh1 umejiunga leo, kwa taarifa yao mimi ni mzoefu humu jamvini,nimefanya hivi kwa sababu ya usalama wangu, nmanake hawa jamaa ndo kila kitu nchi hii.

Nijuavyo Mkurugenzi Mkuu wa CRDB ni MPARE....!!
 
Mkuu hata maeneo ya kusini baadhi ya maduka huwezi ajiliwa kama wewe si muslim,vinginevyo ubadili dini! Ubaguzi wa ukabila na dini upo tanzania!
 
Mimi huwa nakubari ukweli yaani kama mtu yoyote kafanya vizuri huwa namsifu yaani nkiangalia crdb, ipp,azzam, wizara ya nishati na magufuli ni watu wanaofanya vizuri sana I wish mtu kama Dr Kimei au Mengi angepewa nchi awe president kwa sababu zinazoonekana angefanya mambo makubwa mmno.
 
Back
Top Bottom