Ubabe wa Magufuli unavyozidi kumharibu kisiasa

Waziri Magufuli amempongeza Mbunge wa Kawe, Mheshimiwa Mdee kwa kukaa kando badala ya kuungana na wabunge wa DSM kuhusu suala la nauli ya kivuko kama alivyofanya Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Mnyika, huku kukiwa na matatizo lukuki jimboni kwake Ubungo kama vile ukosefu wa maji na mabweni UDSM.

Source: Clouds FM

Clouse ni kichwa cha mwenda wazimu
 
Tatizo la sisi watanzania ni watu wa kudeka sana kama watoto, uko kudekadeka ndio kumetufikisha hapa tulipo.Watu wanataka kiongozi kama JK ahadi nyingi uku akiwachekea wakati utekelezaji ni Ziro.Nchi kama Rwanda wamepata maendeleo ya chap chap kwa sababu wana mtu mkakavu kam Kagame.Watz tuache kulialia tumuache Magufuri afanye kazi yake.

watz mnachekesha na kuuzunisha.mmeshupaa kisa eti mnyika kapewa vyake na malock,pili mmezoea kudekezwa japo deko zenyewe mh!hata vitabu havipendi mazabazabina kama nyie coz ushoga hamtaki na wkt huohuo kukalipiwa hamtaki hah!
 
Magufuri hana maana yoyote. Matatizo ya maji si yupo kwa Mwandosya? Kama Prof mgonjwa si yupo Eng. Lwenge? Huko UDSM wakuu wa chuo wako wapi? Kero ya Kivuko Kigamboni ni sawasawa! kushughurikiwa kwa kutetewa na wabunge hawa. Magufuri arobaini yake inakaribia.

Inakaribia wapi ishafika alilewa na masifa hapo kabla ila sasa hakuna kitu anazaraulika kama soli ya kiatu au anatafuta wa kufa nae huyu kibabu si akafie mbela ya safari peke yake
 
hapo hapo mbunge wangu kandamiza, wamezoea kubebwa, we sh. 100! mbona sisi huku kivuko cha misungwi tunalipa tsh. 300 na kamanga tsh. 800, wamezoea umwinyi tu, kama vp waogelee au warudi vijijini kama sisi, wananikela kwa kulia kulia hao wa dsm!
 
na hayo mawazo kwenye hiyo rangi katoa Magufuli ama umeongeza wewe mwenyewe mtoa mada....! daah mwsho wa siku Mta,shauri Mnika akaweke Maji hata kule Lualo Jeshini kwaku yeye ni Mbunge....

Umeona hee watu wanadhani kuwa mbunge ndo kufanya imposible kuwa posible?
 
ngoja tusubiri reaction ya mtemvu and co.; vita bado mbichi kabisa hii - ushauri wangu 'ajionaye amesimama aangalie asianguke'
 
Waziri Magufuli amempongeza Mbunge wa Kawe, Mheshimiwa Mdee kwa kukaa kando badala ya kuungana na wabunge wa DSM kuhusu suala la nauli ya kivuko kama alivyofanya Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Mnyika, huku kukiwa na matatizo lukuki jimboni kwake Ubungo kama vile ukosefu wa maji na mabweni UDSM.

Source: Clouds FM

Hii ni fikra dhaifu sana hasa kutoka kwa Dr. ni mtazamo potofu kutaka kuwaaminisha watanzania na wana wa DSm kwa,ba tatizo la kivuko ni la jimbo la kigamboni pekee. Pia ni ujinga au mtindio wa akili kufikiria kwamba watu
Wanaotumia kivuko waliokashifiwa ni wakazi wa jimbo la kigamboni tu na kwamba manufaa ya kivuko yanaishia kifamboni tu. Ni uvivu mwingine wa kufikiri na udogo wa uwezo wa kupambanua multiplier ya vitu. Huyu bwana anazidi kuonyesha udhaifu kila siku kukicha. Sijui kwanini amehamua kushusha na kudhalilisha heshima yake mwenyewe.

Atambue ni ujinga kutaka kufunga mtu au watu mdomo kwa matatizo au hali ya mahali kwingine.
 
Magufuri hana maana yoyote. Matatizo ya maji si yupo kwa Mwandosya? Kama Prof mgonjwa si yupo Eng. Lwenge? Huko UDSM wakuu wa chuo wako wapi? Kero ya Kivuko Kigamboni ni sawasawa! kushughurikiwa kwa kutetewa na wabunge hawa. Magufuri arobaini yake inakaribia.

Haikaribii,imefika tayari
 
Magufuli hakupaswa kumkandia Mnyika kama jinsi alivyotaja matatizo ya jimbo la ubungo. Naamini kabisa mh. Mnyika alishayapeleka hayo matatizo katika wizara husika so wakulaumiwa ni serikali na mawaziri husika wa CCM wanaotakiwa washughurikie hayo matatizo maana Mnyika ni mtoaji na mwelekezaji utatuzi wa tatizo jimboni kwake but wahusika ni nyinyi mawaziri na wizara zenu. So nathubutu kusema mh. Magufuli umekosea sana kumponda Mnyika na kwa waelewaji umaarufu wako ndivyo unavyoshuka.

Alijifanya mjuaji sana na kiherehere chake chakujifanya anaga wenzake kuropoka ndicho kilichomponza akidhani ni umaarufu
 
Binafsi naonga mkono kuongezeka nauli za abiria kwa kiwango hicho. Mizigo na magari tunaweza kujadili. Wanasiasa wasitafute cheap popularity. Waache Magufuli afenye kazi. Mara nyingine Kiongozi unatakiwa uwe tayari kutoa kauli ambazo watu hawazipendi lamsingi unachokitetea kiwe na maslahi kwao na kwa taifa.
 
Waziri Magufuli amempongeza Mbunge wa Kawe, Mheshimiwa Mdee kwa kukaa kando badala ya kuungana na wabunge wa DSM kuhusu suala la nauli ya kivuko kama alivyofanya Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Mnyika, huku kukiwa na matatizo lukuki jimboni kwake Ubungo kama vile ukosefu wa maji na mabweni UDSM.

Source: Clouds FM

kwa mara nyingine huyu mh dr magufuli amekurupuka kutoa maelezo hayo hapo juu,kwanza labda kwasababu anatumia vx hajaenda ubungo bus terminal kupanda basi anaepaswa kulipia shs 200 ni aidha msindikizaji,mpokeaji au wafanyabiashara wa hapo ubungo terminal,msafiri wa mikoani halipi kitu,pili kituo cha mabasi ubungo ni cha wasafiri wa mikoani kutoka kwenye kila pembe ya nchi na siyo jimbo la ubungo tu, tatu matatizo ya maji na mabweni udsm yanachangiwa utendaji mbovu wa wizara husika kwenye serikali ya ccm ambayo yeye ni member wa cabinet.kumbuka issue ya colective responsibilities.
 
Siku zote Magufuli hajawa mstaarabu kwa kauli zake. Uongozi unahitaji kujua kuheshimu wenzako hasa kwa kauli unazozitoa mbele ya unaowaongoza. Ili kuweza kuongoza kwa staha ni lazima uheshimike na wale unaowaongoza. Hii itakuja pale utakapo waheshimu watu wako kwanza. Kwa hili kakosea kwa kutoa kauli chafu. Yako mengi ya kuweza ku justify upandaji wa nauli lakini si kauli kebehi.

Kiubinadamu, kisiasa na kijamii kakosea. Sina la kumsaidia. Ki u kweli siku nyingi niliona akipewa nafasi kubwa -- say -- uwaziri mkuu tuu atakuwa dikteta ambae hajawahi kutokea bongo hii


Kauli za Magufuli zinapingana na taaluma yake ya Dr. vinginevyo hiyo PHD ni ya heshima hakusotea darasani. Wenye kiwango cha taaluma aliyo nayo watakubaliana na hoja yangu kwa kuwa anaonekana katika kauli yake hana ujuzi wa elimu ya usemaji (ritoriks) kiwango ambacho ndio masomo yanayoampandisha chati mwenye PHD. Mwenye taaluma hiyo anaweza kukusema mtu hapa usijue na ukajisikia tu kama amekusifia, ila ukifanya uchambuzi ndio unaweza kugundua alivyokukokotoa.

Idadi kubwa ya watu aliokuwa anaongea nao hakupaswa kutumia lugha ile hata kidogo, maana lugha hiyo angemwambia mtoto wake anayemlea kwa kuwa anamfunza adabu. Au angewaambia wapiga kura wake wa huko Ziwa Magharibi labda wamezoea ubabe na lugha za aina hiyo, lakini kwa watanzania wengi tu wastaarabu na tunajali utu na kutunza heshima ya kila mmoja hapo ndipo hekima ilipolala.
 
Sifa moja kuu ya kuwa kiongozi ni kusimamia yale unayosema. Tanzania inanuka viongozi vigeu vigeu, wanasema hili leo kesho wanakwenda kinyume. Magufuli kaza buti, kama vibosile watataka kurudia ile movie ya kukukashifu na kukuita mbabe ili waonekane 'watu wa watu' basi wafanye hivyo. Lakini watambue nchi hii imekwenda mrama kwa sababu ya kuwa biashara ya kinyonga!
 
Ukiwa na busara nyamaza. Maana kama mtu mzima alijua nini kaongea na kwa nini. Kwa nini mmsingemuuliza je zile foleni za weekend zitakuwa mwisho na utasimamia vipi mapato. Pole Mnyika ungeaga humu jamvini kabla ya kwenda. Other day pima maji kwa fimbo kwanza.
 
kwa mara nyingine huyu mh dr magufuli amekurupuka kutoa maelezo hayo hapo juu,kwanza labda kwasababu anatumia vx hajaenda ubungo bus terminal kupanda basi anaepaswa kulipia shs 200 ni aidha msindikizaji,mpokeaji au wafanyabiashara wa hapo ubungo terminal,msafiri wa mikoani halipi kitu,pili kituo cha mabasi ubungo ni cha wasafiri wa mikoani kutoka kwenye kila pembe ya nchi na siyo jimbo la ubungo tu, tatu matatizo ya maji na mabweni udsm yanachangiwa utendaji mbovu wa wizara husika kwenye serikali ya ccm ambayo yeye ni member wa cabinet.kumbuka issue ya colective responsibilities.


.....Mosi, Ubungo basi terminal ipo kwenye jimbo la Ubungo, so kama Mnyika yupo tayari kuongoza maandamano ya wananchi wa jimbo lingine kupinga bei ya Panton si zaidi sana aongoze maandamano ya kupinga kiingilio stend ya Ubungo?....Mnyika amekurupuka..

...Pili, Magufuli hajasema kuwa Mnyika atatue mwenyewe matatizo ya Hostel za wanafunzi Mlimani, alichosema NMnyika anawajibika kuhakikisha wananchi wake hawa wanapata malazi mazuri, na yeye alitegemea Mnyika angeleta hoja/mawazo wizarani mwake kupitia TBA namna wanavyoweza kulitatua tatizo hilo, lakini kwa masikitiko ya Magufuli, Mnyika hana muda wa kuleta hoja hizo za msingi kwa wananchi wake, yupo busy kwenye mambo ya majimbo mengine...

...Tatu, hajamsifia Mdee kwa kukaa kimya kwenye suala la Ubungo bali ni kwa kuwa busy kufutilia(wizarani na kwenye taasisi husika) utatuzi wa matatizo ya wananchi wake wa Kawe, amemshauri Mnyika kuwa ni vyema awe busy kwenye matatizo ya wapiga kura wake kabla ya kudandia mambo yasiyo na mashiko kwa wananchi wa ubungo waliomchagua....

...Big up Magufuli, one more time anaonyesha namna alivyo kiongozi Mtendaji,asiyeyupishwa na siasa za wanasiasa magoigoi wanaotafuta umaarufu kwenye mambo ya kipuuzi, go Dr.Magufuli go....
 
Magufuli hakua na haja ya kutumia lugha ya kebehi/matusi. Alipaswa tu kuelezea kistaarabu kuwa nauli haitashushwa. Na si mambo ya pigeni mbiz etc. Kwa hilo Pro-Magufuli muadmit kakosea
 
Sometimes, udikteta unahitajika hapa Tz, kwa jinsi watz tulivyo, tunahitaji amri. Go go Magufuli, wewe ni jembe vivuko lazima vijiendeshe.
 
Mramba alivyotukana kipindi kile watu wale nyasi watu tulilalamika lakini kwa nini sasa hivi wengi wana sympathise na magufuli ilhali wote walitumia lugha za kebehi/dharau?
 
Nlikukwa naona kama anafaa kuwa waziri (sio raisi) ila kwa siku zinavyosonga itafika mahali ntaona hafai kuwa hata balozi wa nyumba kumi kama ataendelea na mtindo wake huu. Ni hivi karibuni alihamisha wafanyakazi (baadhi ngazi ya mkoa) wa idara fulani kwa kukurupuka tu (sijui ishu imeishia wapi! yani mambo yake ni ya kukurupuka kinoma yeye anajiona ndo anachapa kazi kumbe hewa tu!
 
Back
Top Bottom