Ubabe wa Magufuli unavyozidi kumharibu kisiasa

Msilete siasa jamani kwenye mambo ya msingi hapa,, Hivi kama maisha yanapanda na ghalama za kutoa huduma nazo zinapanda, kuna ubaya gani nauli kupanda kutoka sh 100
mpaka sh 200? hivi hz siasa kuna mahara inabidi ziwe na staha ili serikali ifanye kazi yake,, huku kujikomba kwa wapiga kura kunarudisha sana maendeleo ya nchi na tatizo kubwa wanasiasa wetu kuwa maskini wa mawazo wamekuwa wanafikiria chaguzi2 hata kama kuna kutumikia wananchi badala ya uchaguzi. Unapochaguliwa mbunge ama uongozi cyo kutetea maana yake ni kutaka kila ki2 kiwe nafuu hata kama haikubaliki. hv hicho kivuko kikiharibika hela ya matengenezo itatoka wapi kama cy kujiendesha chenyewe?,,msijinufaishe ki siasa kwa kutetea ujinga. mh, magufuli upo sawa fanya kazi kwa kuangalia mbele usiwaze mambo ya uchaguzi kama hawa wabunge wa dar, hamna shukurani wananchi hata mgepunguziwa sh, 25 mgelalamika kudadi sh 50 . Mmeshapandikizwa ujinga, lakini hawa wanaowashawishi kutaka nafuu kika ki2 cjwi cku watakapopata madaraka wao watawaongoza vp.
 
Tatizo la sisi watanzania ni watu wa kudeka sana kama watoto, uko kudekadeka ndio kumetufikisha hapa tulipo.Watu wanataka kiongozi kama JK ahadi nyingi uku akiwachekea wakati utekelezaji ni Ziro.Nchi kama Rwanda wamepata maendeleo ya chap chap kwa sababu wana mtu mkakavu kam Kagame.Watz tuache kulialia tumuache Magufuri afanye kazi yake.
 
na hayo mawazo kwenye hiyo rangi katoa Magufuli ama umeongeza wewe mwenyewe mtoa mada....! daah mwsho wa siku Mta,shauri Mnika akaweke Maji hata kule Lualo Jeshini kwaku yeye ni Mbunge....

Mkuu hayo yote kayatamka, pia amesema anamheshimu sana Mheshimiwa Mnyika hatahivyo anashangaa kushupalia ongezeko la nauli ya kivuko wakati hasemi lolote kuhusu sh. 200 wanazolipa watu wanaoingia Ubungo stendi kuu ya mabasi
 
Makufuli anatapatapa. Anataka kutuletea siasa za divide and rule. Wenye akili zetu tumemshtukia. Leo hii Makufuli anampongeza Mbunge wa CDM! Mboni mambo! Kweli anatafuta huruma
 
simtetei waziri magufuri kwa kauli yake,nachelea kusema kuwa watanzania tumezoezwa kubembelezwa kama vile,rais anasema tokeni na msirudi mabondeni,wananchi wanarudi,wakipatwa mafuriko oh serikali haijali watu wake,leteni helikopta tuokoe watu.jamani tuwe makini,hili jambo linakuzwa bila sababu. tuangalie na kujadili mambo muhimu kwa maendeleo ya wengi. tukuze uchumi watu waweze kulipa nauli hata wakipanga 500! kwa nini tuwe maskini hata tukose sh.100? TUJIULIZE.
 
Magufuli hakupaswa kumkandia Mnyika kama jinsi alivyotaja matatizo ya jimbo la ubungo. Naamini kabisa mh. Mnyika alishayapeleka hayo matatizo katika wizara husika so wakulaumiwa ni serikali na mawaziri husika wa CCM wanaotakiwa washughurikie hayo matatizo maana Mnyika ni mtoaji na mwelekezaji utatuzi wa tatizo jimboni kwake but wahusika ni nyinyi mawaziri na wizara zenu. So nathubutu kusema mh. Magufuli umekosea sana kumponda Mnyika na kwa waelewaji umaarufu wako ndivyo unavyoshuka.
 
Hebu ngoja kidogo jamani, Dr Maghufuli kaleta hoja nzito sana hapa.

Hivi kweli 200/- watu tunapoingia tu ndani ya stendi kuu Ubungo huwa tunakua tumenufaika usafiri gani pale? Kwa nini nilipe kwa kumsindikiza mtoto wangu kwenda shule mikoani wakati na nauli pia namlipia mimi?

Kuna haki gani kulipia kupita tu getini wakati hakuna huduma yoyote ninayopata pale?
 
hilo nalo neno huyu jamaa kweli kichwa hiyo ni challenge kwako mnyika unapokosoa kubali pia kukosolewa
 
Dr Magufuli kwa kipindi cha karibuni amekuwa akifanya kazi kwa kutafuta sifa na kujikuta anatamka maneno yasiyo na busara.Inawezekana hakutegemea kuona wananchi wakimzomea kwa kujua kuwa anapendwa sn na watu hivyo akajikuta anapandwa na jazba na kujibu kwa jeuri ajirekebishe.Kuhusu nauli kupanda kwa mtu kuwa sh 200 naunga mkono kabisa ila napinga ongezeko la nauli ya maguta,gari nk ambavyo vimepanda kwa asilimia kubwa bila kuzingatia vigezo ushauri na kibali toka kwa Sumatra hapa ndio wabunge wangepigania sio kutaka Dr Magufuli aombe msamaha tu.hv sio hawa wabunge wa Dar miongoni mwao wanatuhumiwa na kashfa mbalimbali ikiwemo za Uda na nk au ndo tayari wameshatamani na kivuko siwaamini? Mnyika ulikurupuka wenzio kuna kitu wanatafuta ikiwemo umaarufu kama afanyavyo Dr Magufuli.
 
Kuna jambo linanipa shida pengine uongozi wa jiji wangetoa ufafanuzi. Wanakataza Bajaj na Bodaboda mjini lakini wanaruhusu Guta? Maendeleo in reverse? Tukumbuke Bajaj na Bodaboda wanalipia leceni na makato mengine, gutta wanalipa nini? Kama serikali haiko makini kuhusu mapato wana haki gani ya kulalamika wakati mtoa cheque kama Cameroon anapotoa masharti?
Umkatae mlipa kodi lakini wa bure sawa? Wabunge wa Dar wanasemaje kweli hili?
 
Dr Magufuli kwa kipindi cha karibuni amekuwa akifanya kazi kwa kutafuta sifa na kujikuta anatamka maneno yasiyo na busara.Inawezekana hakutegemea kuona wananchi wakimzomea kwa kujua kuwa anapendwa sn na watu hivyo akajikuta anapandwa na jazba na kujibu kwa jeuri ajirekebishe.Kuhusu nauli kupanda kwa mtu kuwa sh 200 naunga mkono kabisa ila napinga ongezeko la nauli ya maguta,gari nk ambavyo vimepanda kwa asilimia kubwa bila kuzingatia vigezo ushauri na kibali toka kwa Sumatra hapa ndio wabunge wangepigania sio kutaka Dr Magufuli aombe msamaha tu.hv sio hawa wabunge wa Dar miongoni mwao wanatuhumiwa na kashfa mbalimbali ikiwemo za Uda na nk au ndo tayari wameshatamani na kivuko siwaamini? Mnyika ulikurupuka wenzio kuna kitu wanatafuta ikiwemo umaarufu kama afanyavyo Dr Magufuli.

Magufuli ana mambo ya enzi za chama kimoja. Hivi si alikuwa mwalimu huyu? ana tabia za walimu wa chemistry au agriculture wa sekondari
 
Zungukeni kote ila Dr. Awatake radhi kwanza kama aliwashauri watu kmboni wapige mbizi, kauli za kiungwana ndio zinazotakiwa kauli za ktk blog zibaki huku huku
 
halima mdee hebu mjibu magufuli, je ni kweli ulikuwa pembeni au ulitingwa na majukumu mengine?
 
amesema kila mtu inabidi aheshimu katiba. Na yupo tayari kuwapa wanaotaka kukiendesha kile kivuko hata kesho lakini aje na mainjinia wake, mafuta yake na wafanyakazi wake. kasema katika siku mbili kipato cha kivuko kimeongezeka kutoka million 9 hadi million 18. kwa hiyo wanao tegemea Magufuli atapunguza nauli ya kivuko wasahau hicho kitu.
source Mlimani Tv. Mia
 
Back
Top Bottom