Ubabe wa Magufuli unavyozidi kumharibu kisiasa

Nlikukwa naona kama anafaa kuwa waziri (sio raisi) ila kwa siku zinavyosonga itafika mahali ntaona hafai kuwa hata balozi wa nyumba kumi kama ataendelea na mtindo wake huu. Ni hivi karibuni alihamisha wafanyakazi (baadhi ngazi ya mkoa) wa idara fulani kwa kukurupuka tu (sijui ishu imeishia wapi! yani mambo yake ni ya kukurupuka kinoma yeye anajiona ndo anachapa kazi kumbe hewa tu!

Ni bora subira utakachoamua kitakuwa na ulinganifu pande zote badala ya hulaka ya kukurupuka na uamuzi unaotolewa kuonekana unatofautiana kutoka kwa mtu ambaye hatukutemea kufanya hivyo, na kwa mantiki ya kujenga utetea sasa anaishia kutukana watu hadharani bila aibu.
 
Mramba alivyotukana kipindi kile watu wale nyasi watu tulilalamika lakini kwa nini sasa hivi wengi wana sympathise na magufuli ilhali wote walitumia lugha za kebehi/dharau?
 
WATANZANIA WATANZANIA!! Acheni maneno maneno yasiyo na tija ya kuijenga nchi, toka juzi magufuli >< 2, vyombo vya habari magufuri, ndiyo aliongea, si tushamjibu kitu kidogo kinakuzwaa mpaka basi hakuna kiongozi aliyeperfect mlitaka kila siku afanye mema? Asikosee?
Acheni kupoteza mda kwa hoja ndogo kama hizo! Sh.200 tatizo. Mbona hamzungumzi kupanda kwa bei za vyakula? Tsh200 ndo inawaathiri watz wote?
Tunakuwa ka vyombo vya habari vya uingereza.
TUJENGE TAIFA KWA KUFANYA KAZI KWA BIDII, SIO KUKAA KUZUNGUMZIA HOJA YA SIKU MOJA WIKI NZIMA.
 
Mramba alivyotukana kipindi kile watu wale nyasi watu tulilalamika lakini kwa nini sasa hivi wengi wana sympathise na magufuli ilhali wote walitumia lugha za kebehi/dharau?

Magufuli hakua na haja ya kutumia lugha ya kebehi/matusi. Alipaswa tu kuelezea kistaarabu kuwa nauli haitashushwa. Na si mambo ya pigeni mbiz etc. Kwa hilo Pro-Magufuli muadmit kakosea

...Sasa kama Nauli haitashushwa, watu ambao watagoma kulipa nauli mpya na wanataka kwenda mjini kutokea Kigamboni wataendaje?kwenye pantoni la temesa watazuiwa so option itakayobaki ni either wazunguke kongowe, wavuke bahari kwa kupiga mbizi, mtumbwi, maboti au pantoni binafsi, au wahame Kigamboni, ndio ukweli huo japo ni mchungu kumeza kwa watu wanaopenda kuendekeza vya bure na kucheza viduku kwenye mambo ya msingi...

...Tungekuwa na kiongozi mkuu wa namna ya Magufuli, nchi hii ingenyooka...
 
kiuhalisia, kosa la Magufuli ni kutokumung'unya maneno,sioni sababu ya malumbano, sukari,mafuta,mchele vinapanda bei kwa kasi ya ajabu, wanasiasa hawaoni hayo,anatakiwa apewe ushirikiano ili aijenge DSM iliyo Bora,ambalo ndio lengo la kupanda kwa nauli,la msingi ni kuzuia mianya ya walaji
 
I do support you Magufuli.
Watz 2shazoea sauti za kubembelezwa.
JK My president alishawahi kuongea kauli kali sana kwa wafanyakazi, mbona hamkumjadili kiivyo? Wangapi wameongea kauli nzito 2mechunia MAGUFULI MAGUFULI. Jengeni nchi kawa wenzetu china sio kujenga nchi kwa malumbano yasiyona maendeleo.
NAFUNGA RASMI POST HII.
 
Watz tunashangaza. Oh kauli mbaya..kwanini tunapenda vilivyorembwa? Kama serikali imesema kuvuka lazima ulipe 200, option ya kuvuka bila kulipa si ndio upige mbizi au uzunguke kongowe! Jamani tunahitaji viongozi wasiogopa kuchubua hisia za mtu kwenye maamuzi.
 
Haiwezekani baada ya miaka 50 tangu tupate uhuru ishindikane kujenga daraja pale ili wananchi watumie bure kama zinavyotumika barabara nyingine. Kama kungekuwa na daraja basi watu wengi ambao wana kipato cha chini wangetembea kwa miguu na hivyo kuwa na haki ya kutumia miguu yao kwa usafiri kama vile watanzania wengine wengi wanavyofanya kwenye maeneo yasiyohitaji vivuko.
 
Magufulii(8).jpg

KWA WANANCHI KIGAMBONI ALIONGEA HIVI:

Kauli inayodaiwa kuwaudhi wananchi hao ni ile iliyotolewa na Waziri Magufuli Januari Mosi, mwaka huu, alipozungumza na wananchi wa Kigamboni kuhusu nauli hiyo mpya na kuwaambia kuwa

asiyetaka kulipa nauli hiyo
  • apige mbizi baharini
  • kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au
  • arudi kijijini akalime.

KWA WAANDISHI WA HABARI ALIONGEA HIVI
Pia baadaye siku hiyo hiyo, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo, alisema

yeyote asiyetaka nauli hiyo mpya kutozwa,

anunue kivuko chake na akitaka akipe jina la chama chake cha siasa kisha atoe huduma hiyo kwa Sh. 100 au bure ilimradi aende kwake (waziri) kupata kibali cha kutoa huduma hiyo.

Mtazamo wangu juu ya Magufuli
Nilivyokuwa namfikiria Magufuli kwa sasa nimeanza kubadili msimamo, maana mambo ya uongozi si shauri ya kufanya utakavyo na kutojali wananchi unaowatumikia. Na mtazamo wake kila kinachopingwa anasukumia vyama vya siasa kama alivyoongea na waandishi wa habari. Huu ni upeo wa kidikteta, Magufuli ni mwanaharakati wa mfumo wa kidikteta.

Hakuna wananchi hapa wewe,hivi watu kulipa mia mbili ndo mnaona wanaonewa,acheni unafiki na majungu,Lazima tufanye maamuzi magumu alitoshauri lowasa ili kulioka taifa,tusitake kujifanya tunahuruma kwa wananchi wakati tunawadumaza,acheni kabisa unafiki
 
Kwa vyovyote vile rekodi ya utendaji ya mtu huyu ni ya kipekee sana, kwangu mimi sioni mtu wa kumlinganisha naye kwa sasa ndani na nje ya chama chake.
 
Mtazamo wangu juu ya Magufuli
Nilivyokuwa namfikiria Magufuli kwa sasa nimeanza kubadili msimamo, maana mambo ya uongozi si shauri ya kufanya utakavyo na kutojali wananchi unaowatumikia. Na mtazamo wake kila kinachopingwa anasukumia vyama vya siasa kama alivyoongea na waandishi wa habari. Huu ni upeo wa kidikteta, Magufuli ni mwanaharakati wa mfumo wa kidikteta.
He was a teacher..cant help it
 
Wote wanaoshupalia ongezeko la shilingi mia wakiwemo wabunge wa Dar naamini wana ajenda ya siri na siyo ongezeko la nauli na kama hawana ajenda ya siri basi ni mataahira wenye mtindio wa ubongo. haiwezekani mtu mwenye title ya mbunge ahamasishe wananchi na kuita vyombo vya habari kujadili shilingi mia huo muda na gharama za kuandaa huo mkutano zingetosha kuwafanya hao wanaowahadaa kwamba wanawatetea kupata pesa nyingine zaidi ya elfu kumi kuliko kuwapotezea muda wao eti wanawatetea. Mtu kama Mnyika nilikuamini sana kwa umakini wako sijui nani kakutapeli ukaingia kwenye jambo hili la kitaahira!!!!!!!!!! Nasikitika sana mdogo wangu mbona wewe siyo mnafiki? Hayo ni vita ya wana ccm kaa pembeni usiitie doa Chadema yetu . Mimi nasema Magufuli usiombe radhi kamwe hakuna ulichokosea na Mungu atakupigania. Kuhusu kupiga mbizi ni sahihi kwa kuwa huwezi ukatembea kwa miguu baharini ukitaka kuvuka. Hilo ni jibu la kisayansi na ukiwa nchi kavu utatembea kwa miguu angesema watembee baharini kwa miguu hiyo ndiyo ingekuwa kejeli.

Hii ndiyo design ya viongozi tunaotaka kwa sasa kila sehemu. Waziri wa fedha naye angetoka na single yake ya walipa kodi/tax! wasiotaka kulipa ushuru wa bidhaa wafunge biashara zao. Mbona tutasonga mbele, na hiyo 200 ya magufuli itakubalika mbona. Tatizo hapa ni hizo wizara zingine kutofanya kazi zao vizuri ndiyo maana mnamuona Dr kama mnaa hivi.
 
inawezekana hata rc wa wakati huo (iringa) dr.kleruu umauti ulimkuta kwa lugha za kuchefua kama hizi.
sioni sababu za magufuli kuwa na lugha chafu kiasi hii.kama waziri sisi watanzania/wana kigamboni ni walipa kodi na hivyo huduma ya pantoni inaweza kutolewa bure maana kodi inayolipwa inaweza kuendesha/kulipia gharama ya uendeshaji.

Viongozi wa jamii ya magufuli hawafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji sembuse waziri ndiyo maana serikali hii inaitwa serikali legelege.
yeyote anaye pinga nauli kuongezwa kwa mia ni taahira na hana kazi ya kufanya baba mama na watoto wako mna muda wa kujadili shilingi mia eti sisi wakazi wa kigamboni !! Kigamboni ni tanzania lazima mfuate sheria hakuna umwinyi hapo fanyeni kazi na siyo uvivu wa kupiga domo tu nauli lazima mlipe . Magufuli anajua kazi hivi angekuambia upinge mbizi nchi kavu ungemwelewaje? Unapiga mbizi kwenye nchi kavu mmezoea kudanganywa kwa maneno mazuri mkiambiwa ukweli mnaandamana eti kwa mia watu wa kigamboni hovyoo kabisa mnadanganywa na ndugulile aendelee kuchukua posho kwa mgongo wenu mnamuona mkombozi mna akili kweli nyie wa kigamboni. Magufuli baba usiombe radhi hakuna ulichokosea msema kweli hapendwi bali wanafiki wanaungwa mkono kama wabunge wa dar.
 
Magufulii(8).jpg

KWA WANANCHI KIGAMBONI ALIONGEA HIVI:

Kauli inayodaiwa kuwaudhi wananchi hao ni ile iliyotolewa na Waziri Magufuli Januari Mosi, mwaka huu, alipozungumza na wananchi wa Kigamboni kuhusu nauli hiyo mpya na kuwaambia kuwa

asiyetaka kulipa nauli hiyo
  • apige mbizi baharini
  • kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au
  • arudi kijijini akalime.

KWA WAANDISHI WA HABARI ALIONGEA HIVI
Pia baadaye siku hiyo hiyo, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo, alisema

yeyote asiyetaka nauli hiyo mpya kutozwa,

anunue kivuko chake na akitaka akipe jina la chama chake cha siasa kisha atoe huduma hiyo kwa Sh. 100 au bure ilimradi aende kwake (waziri) kupata kibali cha kutoa huduma hiyo.

Mtazamo wangu juu ya Magufuli
Nilivyokuwa namfikiria Magufuli kwa sasa nimeanza kubadili msimamo, maana mambo ya uongozi si shauri ya kufanya utakavyo na kutojali wananchi unaowatumikia. Na mtazamo wake kila kinachopingwa anasukumia vyama vya siasa kama alivyoongea na waandishi wa habari. Huu ni upeo wa kidikteta, Magufuli ni mwanaharakati wa mfumo wa kidikteta.

ndio zenu watanzania mmezoea lugha za kisanii kama rais wenu, mmekalia uvivu tu na siasa kila jambo, hivi kwa akili zako unafikiri kile kivuko kinatumia maji?

tanzania bila rais dikiteta haiendi! well done magufuli ni wakati watanzania tuwe na upeo wa kufikiri hivi kupiga mbizi ni tusi na ku...mayo nini nini?

keep it up magufuli, tanzania imejaa mijitu kila jitu juaji na hayafati sheria hayo majitu ya tanzania, anzia tu kwenye daladala, njoo makazini, nenda mahospitalini nk. kila sector hakuna jitu linalofuata sheria.
 
Huyu ni mropokaji tu,nilishamtoaga maanani muda sana! Na kwa matusi yake ya juzi,nimekuja kugundua uwaziri ni nafasi ya juu sana kwake,anafaa kuwa mkuu wa wilaya au meya wa jiji tu! Nothing more
 
yeyote anaye pinga nauli kuongezwa kwa mia ni taahira na hana kazi ya kufanya baba mama na watoto wako mna muda wa kujadili shilingi mia eti sisi wakazi wa kigamboni !! Kigamboni ni tanzania lazima mfuate sheria hakuna umwinyi hapo fanyeni kazi na siyo uvivu wa kupiga domo tu nauli lazima mlipe . Magufuli anajua kazi hivi angekuambia upinge mbizi nchi kavu ungemwelewaje? Unapiga mbizi kwenye nchi kavu mmezoea kudanganywa kwa maneno mazuri mkiambiwa ukweli mnaandamana eti kwa mia watu wa kigamboni hovyoo kabisa mnadanganywa na ndugulile aendelee kuchukua posho kwa mgongo wenu mnamuona mkombozi mna akili kweli nyie wa kigamboni. Magufuli baba usiombe radhi hakuna ulichokosea msema kweli hapendwi bali wanafiki wanaungwa mkono kama wabunge wa dar.

Tukianza na wewe na makufuli wako wote mataahira tu,na kama mna akili timamu hamuwezi kutegemea kila mtu atawaunga mkono kwa kuongeza nauli.

Hivi kuna mtu mwenye data za ukweli kuhusu mapato ya pale kivukoni? Natafuta taarifa halisi,na sio ya kuchakachuliwa.

Hivi mtu wa sinza akijengewa lami lazima hela ipatikane sinza?? Au lami ya tegeta itoke kwa watu wa tegeta??
 
..Magufuli angejenga hoja zake kwa heshima bila matusi na kejeli angepungukiwa nini?

..imekuwa jambo la kawaida kwa Magufuli kuzusha na kutoa matusi dhidi ya yeyote yule anayepingana naye.

..mtakumbuka matamshi aliyoyatoa majuzi dhidi ya mheshimiwa mbunge wa Ukerewe.

..halafu vituko na vitimbi vyote hivi anavifanya akiwa na madaraka ya Uwaziri.

..Je, angekuwa Waziri Mkuu au Raisi ingekuwaje?

..huyu akiwa Raisi anaweza kutoa hata matamshi yatakayoharibu mahusiano na mataifa mengine, au hata kusababisha vita.
 
Back
Top Bottom