Ubabe wa Clouds FM uangaliwe

yani wakiona mtu kang'aa tu lazma wamchukue inshort wanataka wawe juu daily
 
Sasa hapo wa kulaumiwa nani? Clouds au Watangazaji wenyewe

Hata mimi nimejiuliza, utafikiri wanapigwa bakora waende Clouds... huyu mmmmh ana lake na ni kauchochezi ambako hakana miguu wala kichwa.
 
Kwa avatar yako duh unaonyesha upo kwenye mambo ya muziki, si uende uongee nao na wewe upate maarifa au!? Inaonyesha umekaa ukaona uje uwaharibie humu kumbe ndio umesaidia kuwapa promo haswaaa ya kuwa keanini hao wote eapende kujiunga na Clouds na wala hawakubebwa au kutekwa kwenda kuwafanyia kazi

Lengo lako limepiga chini, uko ulipo jiongezeni tu muendelee kushindana huku mkituburudisha sisi wananchi.
 
umemsahau Fred wa alokuwa redio ya mwanza ile
 
Sasa tatizo ni nn ? Kwani wamelazimishwa kuendelea kufanya kazi ? Ujui kuwa ni soko huria ? Maelezo mengi lakini hamna kitu
 
Watu wengine bhana wanafurahisha
Wanasikitisha
Wanahuzunisha na kushangaza pia,
Hivi mkuu kiuhalisia kutokana na Thread yako ubaya wa Clouds uko wapi? Hao watangazaji walishikiwa viboko na bastola hili waje wasain kufanya kazi clouds? Unawazidi akili hao wahusika wenyewe walioamua kufanyapo kazi? Halafu badala ya kuwa na hoja nzuri unashabikia na kuhamasisha Watu wasikilize EAradio na Efm what for? Komaa na radio zako unazozipenda na sisi tunaoielewa clouds tutaendelea nayo, nani hajui mchango wa clouds katika kuinua na kuwafaidisha wasanii na kupata ajira mbali mbali kwa vijana? Japo wana mapungufu yao make clouds inaendeshwa na binadamu isitoshe wanadamu hatujakamilika, ebu wanapofanya mazuri wape credit zao na wanapokosea waambie pia, sisi ngoja tuendelee kupasua mawingu.
TUNAKUFUNGULIA DUNIA KUWA UNACHOTAKA
KAMATA FURSA TWENDE ZETU
HII NDO THE PEOPLE'S STATION.
 
Mtoa mada subil nikwambie hakuna mtangazaji Tz atakayekataa kwenda clouds!. Pamoj na mapungufu yao ila ndo media inayoongoza kuwalipa vizuri wafanyakazi wao na inawapa nafasi bila kuwabanabana wafanyakazi wao hasa kwenye shughuli zao binafsi mfano mirad ayo anauwezo wakuitangaza brog yake kupitia kipindi chake na hakuna tatizo lakini kitu hichohicho huwezi kukifanya kwenye radio nyingine Tanzania hii..
 
yah ni kweli..ila ndo naona umuhimu wa mikataba..kama wangekua namikataba wasingezungushwa zungushwa
Unajua watangazaji na madjs wanapenda kwenda clouds kwakuwa inawapa fursa za kufanya mambo mengine huku wakiwapa support.
Yani mtangazaji au dj anakuwa na uwezo wa kuja na idea yake na akaifanyia kazi.
Mfano soudy brown na mwenzake idea yao ya ubuyu, umekuwa mashuhuri kwasababu wanautangaza bure kupitia clouds na watakuwa wanapiga ela kweli kweli maana wana mawakala almost kila mkoa.
Bado tour wanazofanya hawabanwi kitu kinacho wafanya hata wengine watamani kujiunga clouds.
Yani watangazaji wa kila kipindi utakuta wanajitahidi waandae kitu ambacho kitawawezesha wapige tour na kuandaa show za nje waingize mkwanja.
Mwisho wa siku kila mtu anaangalia maslahi yake dogo janja anakwambia kwa sasa anapambana kutetea maisha sio hip hop hivyo hivyo kwa kila mtu anapambana apate maslahi sio jina tu.
 
yani wakiona mtu kang'aa tu lazma wamchukue inshort wanataka wawe juu daily
Sasa kwani hilo ni kosa? Ni sawa na mpira tu mwenye kisu kikari anabeba wachezaji wazuri.
Mbona efm waliwachukua akina hando japo waliweza mrudisha mmoja lakini hakuna aliyesema lilikuwa kosa.
Na ukifuatilia utakuta watangazaji wengi na.madjs waliotoka redio nyingine wao ndiyo walikuwa wa kwanza kumuomba ruge kuja clouds.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…