Nilinunua simu ya Tecno H7, ipo ndani ya kipindi cha warranty, imeharibika, inazima bila mpangilio. Siku niliyoipeleka pale ofisini kwao Samora, NHC 2ND FLOOR, DAR walii-flash bila kujua tatizo ni lipi, simu ikaendelea kuwa na lile tatizo, wakasema niwaachie tatizo ni hardware sio software.
Baada ya kuwafuatilia walisema wameagiza spea toka China, nisubiri wiki mbili, wiki mbili zimefika wanadai bado, walichukua spea toka Kariakoo, haijafaa, hivyo nisubiri wiki mbili zaidi waagize toka China!
Nawasihi Watanzania wenzangu kujiepusha na Wachina na hizi simu za Tecno, customer care zao ni mbovu, pia uwezo wa ufundi wao na ufanisi wa simu zao ni wa mashaka.
Nawasilisha wakuu..