Uandishi wetu Katika kingereza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uandishi wetu Katika kingereza.

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kichuguu, Jul 2, 2011.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Picha hii na maelezo yake nimevitoa kwenye Blogu ya Michuzi

  [​IMG]
  Jambo ninaloongelea hapo ni jinsi gani uandishi wetu katika kiingereza ulivyokwenda mrama kwa sababu ya kutaka kumjenga rais wetu.

  Ni kupindisha lugha ya Kiingereza kumtaja mtu kwa kutumia titles zaidi ya moja. Kwa mfano huwezi kusema General Dr. David Patreas, au Secretary Dr. Condoleeza Rice, au Secretary Professor Condoleeza Rice President Professor Dr. Obama. Kwa kawaida utawaadress watu wa aina hiyo kwa kutumia title moja tu ambayo ni more relevant katika madaraka yake, kwa mfano General David Patreas, Secretary Condoleeza Rice, President Obama. Hata hivyo unaweza kuwaadress kwa titles hizo nyingine iwapo utazitenganisha na titles za madaraka yao ila ukataja madaraka yake, kwa mfano: the army general, Dr David Patreas, au the US Secretary of State Dr. Condoleeza Rice au the US president, Dr Obama.

  Sasa ukiangalia maelezo ya kwenye picha hapo juu utaona mapungufu hayo ya kiuandishi hasa pale inapokuwa inamhusu Kikwete, na hili ni jambo linajitokeza sana katika waandishi wa Tanzania.

  Katika kumtaja Kikwete, waandishi wetu hutumia titles mbili: President Dr. Kikwete!!. Hilo ni kosa!! Kama ni lazima title ya Dr iwepo basi itenganishwe na title ya President; andika the Tanzanian president, Dr. Kikwete. Ni kama ilivyoaninishwa kwenye kumtaja the UN Deputy Secretary General, Dr. Asha-Rose Migiro. Kiuandishi amekuja tena kuboronga kwa kumtaja huyo rais wa Ivory Coast alipotaja the new Ivorian President Allasane Ouattara. Kwa vile alishaona umuhimu wa kuwataja wahusika kwa academic titles badala ya political titles, basi ni lazima angesema the new Ivorian president Dr. Allasane Ouattara, kwa vile jamaa ana Ph.D ya kikweli katika economics, siyo udaktari wa kupandikizwa wa Kikwete. Hilo ni swala la consistency!

  Kikawaida kwa vile marais ni wanasiasa, hawatakiwi kutumia titles za kiacademia, kwa hiyo ilitakiwa iwe ni straight forward kuwa Tanzanian president, Mr. Kikwete na Ivorian president Mr. Allasane Ouattara, kama ambavyo marekani wa wanasema the US President, Mr Obama
   

  Attached Files:

 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Umenena mkuu. Ni tuisheni kubwa. Shida waandishi wetu wanapoandika wanakuwa wanafikiria kwa Kiswahili na kutafsiri ki-sisisi lugha za watu.
   
 3. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Shida kubwa ni kwamba wanaandika wakiwa na fikra za kunfurahisha muheshimiwa bila kujali kuwa wanapoteza uweledi wao.
  This is so threatening
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Asante sana kwa ufafanuzi mzuri
   
 5. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutujuza!
   
 6. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  umesahau ......Engineer prof Mwandosya
   
 7. r

  rununu Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sahihi mkuu tatizo ni kutumia lugha ambazo hatuziwezi, kwa nini asingetumia kiswahili? Fikra sahihi huja kwa lugha sahihi!!!
   
Loading...