Hakuna asiyejua kuwa wakati kuna mchakato wa (akina Zitto na wenzao) kuandaa misingi ya tume huru ya uchaguzi, wahudumu wa tume hiyo wameendelea kuteuliwa bila hata ya mashauriano.
Ni wazi kuwa kwenye jambo hili nyeti kuna wenye maslahi yao binafsi ndani ya mchakato unaoendelea.
Wananchi kupitia tume huru ya uchaguzi wanahitaji mgombea aliyebora na aliyeshinda tu, ndiye atangazwe kuwa mshindi.
Hilo haliwezi kuamriwa na washindani. Wala suluhisho muafaka haliwezi kupatikana bila ya kuwa na katiba madhubuti ya wananchi.
Kupata katiba ya wananchi ndiyo ulio ukombozi kamili wa kuyaweka mamlaka ya nchi mikononi mwao. Ukweli mchungu, hilo haliwezi kuridhiwa na walio madarakani.
Katika hali isiyokuwa na uhuru kamili wa mihimili, hakuna lolote la maana linaloweza kutegemewa kwa mujibu wa sheria.
Hatupaswi kuogopa kulipa gharama zinazohitajika, kama nia yetu kweli ni kupata katiba ya wananchi. Mkono mtupu haulambwi.
Harakati zozote zinahitaji uongozi.
Chadema inayo nafasi ya kuendelea kutoa uongozi unaohitajika (ambao kwa bahati mbaya) umekosekana tangia Mh. Mbowe kukamatwa.
Ni muhimu kujipanga upya. Tena kukiwa na plan B mkononi katika kila ilipo lazima:
1. Pana haja ya kufanya mabadiliko ya msingi kiuongozi Chadema ili kukiwezesha chama hiki kuendelea kutoa uongozi unaohitajika kwenye harakati hizi.
2. Pana haja ya kuweka wazi mpango mkakati wa mapambano wa kuipata katiba hiyo mpya kwa maslahi ya taifa.
Hakipo cha kuficha kwa maana kinachotakiwa ni kupatikana kwa katiba mpya kwa njia za amani.
Waliweza kina Desmond Tutu wakauondoa ubaguzi wa rangi.
Kwanini isiwe sisi na katiba mpya?
--------------
Angalizo:
1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
3. Agenda yetu ni ya kudumu si marafiki.