Hakuna pigo kubwa walilopata CCM kwenye uchaguzi wa mwaka huu kama hilo tamko la NEC kuwa matokeo yote ya udiwani, ubunge na Urais yatabandikwa kwenye vituo vya kupigia kura mara tu ya kukamilika zoezi la kuhesabu kura hzo.
Nikukumbushe tu kidogo ya kuwa tokea mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi urejeshwe nchini mwaka 1995, chaguzi zote zilizopita matokeo yaliyokuwa yakibandikwa kwenye vituo vya kupigia kura yalikuwa ya udiwani na ubunge pekee.
Mabox ya kura za Urais yalikuwa yakipelekwa Wilayani kwenda kuhesabiwa upya na hapo ndipo maccm walipokuwa wakifunga magoli yao ya mikono.
Bahati nzuri sana safari hii Jaji Lubuva 'chale' zimemcheza na kuamua kuvaa ujasiri kwa kufanya uamuzi huo mgumu na mchungu sana kwa Sisiem.
Cha maana hapo ijulikane wazi idadi halisi ya wapiga kura kila kituo na idadi halisi ya vituo. Ndiyo mje sasa na hizi nyimbo zenu za fulani ndiyo Raisi. Wwnu wa mezani. Kama mlimjua tangu mwanzo yanini kutusumbua kupiga kura. Mtangazeni mum apishe.
Sasa kwa taarifa yako ccm ealikuwa na mkakati wa kuweka pingamizi kwa huo utaritibi mpya ila wamedhindwa maana matokeo tutakuwa nayo yote kabla ya tume kuyapata sasa walete tofauti ndio ujue watu wanavyo taka mabadiliko kwa garama yoyote.
hizo ndo propaganda hakuna kitu Kama hicho hakuna vurugu hao wana nia ya kutafanya wananchi tufadhaike ila mwaka wa mwisho ccm tumemabadilika tuna jambo letu
Mimi nimekuelewa sn gamba, umeongea kinyume chake, maana wew ni mzee wa kinyume nyume, ushapiga buku saba yako umetulia. Lowasa ndo atakuwa rais wako wala usihangaike sn
kwa maoni yangu ni pigo kwa ukawa kwa upande tofauti ya ulivo eleza, ni nafasi ya chama tawala chenye nguvu kubwa ya kifedha(japo uhalali wake u mashakani) kurubuni mawakala wa ukawa vituoni, au kuhonga wasimamizi wa vituo ambavyo ukawa watashindwa kuweka mawakala
Hii ndio furaha UKAWA tena furaha kubwa wala si pigo kama mnavyotaka kupotosha umma. Kura zipo nyingi tu mitaani na vijijini, kinachotakiwa sasa ni kupata mawakala wazuri na waaminifu.
Ndugu zetu kwa kugeuza maneno tu mnastahili pongezi, nimewavulia kofia.
huu uandishi hauna tija zaidi ya ushabiki tu wa kisiasa. kwa sasa vyombo vya habari vingi vimeamua kuweka weledi pembeni kisa kuhongwa na wagombea pamoja na vyama vya siasa..
Inasikitisha sana! Kuwa kuna mtu mzima kabisaaa anaandika maneno ya uchochezi bila woga huku alikua ni uzushi.kesho la polisi wako wapi kumuachia mtu kama huyu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.