Uamuzi wa NEC pigo kwa UKAWA

Uamuzi wa NEC pigo kwa UKAWA

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imepigilia msumari wa mwisho katika kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) bada ya kutangaza kuwa kura za urais, ubunge na madiwani zitahesabiwa kwenye vituo vya kupigia kur kwa uwazi.

Uamuzi huo ni pigo kwa Ukawa ambao tayari wameanza kuchungulia mgombea wao wa urais Edward Lowassa kushindwa na mgombea wa Ccm Dk. John Magufuli kuanza kutumia ujanja wa kulalamika kwmba wataibiwa kura wakati wa kusafiriisha masanduku ya kura wakati wa uchaguzi ili wafanye fujo.

Jumanne wiki hii Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damiani Lubuva, alisema kura zote za urais, wabunge na madiwani zitahesabiwa katika vituo vya kupiga kura na matokeo yote kutangazwa hapo hapo na marufuku kusafirisha masanduku ya kupigia kura kama ilivyokuwa zamani.

Alisema ktika uchaguzi w mwka huu marufuku kuhamisha masanduku ya kura kwa sababu vituo vya kupigia kura vitbdilika na kuwa vituo vy kuhesabia kura baada ya upigaji kura kumalizika.

" kura zote za urais, ubunge na udiwani zitahesabiwa katika kila kituo na matokeo yatabandikwa vituoni hapo hivyo sijui wanaosema kura zitaibiwa zitaibiwaje", alisema Jaji Lubuva na kuongeza " baada ya matokeo kubandikwa katika kila kituo yatapoelekwa katika kata husika kujumlishwa na hapo pia yatabandikwa,

"Mshindi wa udiwani atatangazwa hapo na Yule wa ubunge na urais yatapelekwa jimboni ambako yatajumlishwa na mshindi wa ubunge kutangazwa na kukabidhiwa cheti huku uris yakipelekwa makao makuu ya tume.

Alisema njia hiyo itasaidia matokeo kufika haraka kama inavyotakiwa na baada ya tume ya uchaguzi kupokea matokeo hayo yatatangazwa moja kwa moja kupitia luninga na redioni.

Kutokana na hali hiyo alivishauri vyama vya siasa viache kauli za kuwataka wafuasi waowasiondoke kwenye vituo vya kupiga kura kwa vile hakuna kura zitakazoibiwa.

Kauli ya Lubuva ni mwiba kwa Chadema na Ukawa kwa sababu tayari walishawamoinisha wafuasi wao wataibiwa kura hivyo wafanye fujo, wakati wakijua wazi kuwa mgombea wao atashindwa kihalali ktika uchaguzi huo.

Habari za zilizopatiakana kutoka ndani ya chadema zinaeleza kuwa mwenendo wa mgombea wao, Lowassa katika kampeni zmeanza kuwatia wasiwasi na kwamba sasa wameanza kushawishi wafuasi wao wafanye fujo ili kuvuruga uchaguzi.

Habari hizo zinaeleza kuwa tayari chama hicho kimetoa mafunzo mafunzo ya kwa vijana 3,000 nchini ambao watasambazwa katika vituo vya kupig kura ili wanzishe fujo baada ya matokeo kusambazwa.

Mtoa habari wetu aliye karibu na chama hicho anasema kuwa lengo kuwa la kufanya hizo ni kutaka kuiweka serikali ya rais Kikwete katika matatizo ya mahakama kimataifa ya uhalifu.

Wanasema urais wanajua hawatapata, lakini mgombea wao Lowassa na wafuasi wake hususani waliotoka ccm hivi karibuni wanataka kuona rais Kikwete naye anaishi katika matatizo mazito ya kupelekwa ICC.



Chanzo: Dira
 
ikungi

Nina shaka na uraia wako!
 
Last edited by a moderator:
siyo Lowasa, Dovutwa, Magufuli, wala Mgwira aliye na uhakika wa kushinda. Wananchi watanzania ndio waamuzi. Sasa huo uhakika wa ushindi wa upande mmoja unaouongelea umeupata wapi? kura yako moja ndo inakuonyesha maamuzi ya watanzania wote? Usifanye watu waamini kuwa ushindi ni mezani na wala si katika sanduku la kura.
 
MTU kajipinda kuandika makala ndefu akiinuka ukisoma unakuta ni kama alikuwa anajisaidia tuu maana hakuna kitu zaidi ya uchafu. Mmelogwa?
 
Ukisikia kuna habari toka kwa waliochanganyikiwa wakiwa "news room" kwenda kwa mixed audience ndo kama hii... Spin doctoring!!

Bila tume kubanwa vizuri kila angle maelezo hayo ya Lubuva tungeyajuaje..??.
Ni hivi tutajumlisha matokeo ya vituo vyote mapemaa kabla ya tume... Sasa waje wajumlishe tofauti waone moto wake..!!
 
Rais Kikwete kafanya kila analoliweza katika awamu yake na anakaribia kumalizia kwa heri. Haya mabandiko ni ya nini?
 
Pigo kwa ccm na si vinginevyo
Acha kutupumbaza ccm ndo wamekata kauli kuskia kura kwenye vituo
 
Ukimjibu mpumbavu utafanana nae asiyejua kuwa CCM imeshafutwa shauri yake.
 
Huna akl ndugu muandishi
Nakushaul endelea na kilimo au shughuli nyingne utatoka sio uandishi.
 
Ukimjibu mpumbavu utafanana nae asiyejua kuwa CCM imeshafutwa shauri yake.

Jamaa zangu bado hawaamini kinachoenda kutokea. Wana jaribu kugusa kila mahali lakini wapi. Fikra za watanzania za mwaka 2005 sio fikra za sasa. CCM out ..!!!
 
Back
Top Bottom