Uagizaji/Biashara ya Magari

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Wana JF kwa wale ambao wanafuatilia habari za kiabiashara watakubaliana na mie kuwa fedha ya kijapan (Yen) Imekuwa na nguvu hasa ukilinganisha na US dollar kwa muda mrefu sasa. Pia ukiangalia Tsh nayo pia imepoteza nguvu (depreciate) kwa muda sasa kwa upande wa dollar. Maaana yake ni nini? Kwa kifupi ni kuwa bidhaa kutoka Japan hasa magari ambapo wengi wetu huagiza kutoka nje nayo pia yamekuwa ghali. Swali, ukiondoa Japan amabpo kwa sasa hivi ambapo exchange rates imekuwa mbaya zaidi (for fifteen years ukilinganisha na US dollar), soko gani jingine linaweza kuwa favourable kuagiza magari?
 
Wakuu hebu tuwekeeni na maadresi za wauzaji hapa tulinganishage mabei, tumezoea japan tu!
 
Ni kweli Yen imekuwa na nguvu sana dhidi ya USD kwa sasa na hii imesababisha export yao kushuka maana vitu vya Japan vimekuwa ghali zaidi na inasemekana hii ni mojawapo ya sababu za kuenguliwa kwenye nafasi ya pili ya nchi yenye uchumi mkubwa duniani na China. China wao wamefix pesa yao kuwa chini ili waweze ku-export zaidi ndo maana pamoja na wafanyabishara wengi sana wakiwemo wa-Tanzania kununu sana vitu China ila cha ajabu hakuna bureau de change hata moja TZ inayouza Yuan ya China.

Mahali pengine unapoweza kupata gari kwa bei rahisi ni Uingereza japo Paundi nayo imekwea juu lakini bei zao bado ziko chini. Tatizo kubwa, wauzaji wa Uingereza hawana mitandao mingi yenye kuonyesha magari na bei zake kama ilivyo kwa Japani. Wao mpaka uwe na mtu unayemfahamu huko ili akusaidie kuulizia kwa wauzaji. Nina rafiki zangu wawili wamenunua huko kwa bei nafuu zaidi kuliko Japan.
 
Nina kauzoefu kidogo na Uingereza. Tatizo la uingereza ili upate nafuu inabidi uanze kutafuta mtu ili muweke kwenye container pamoja. Lakini pia ni takribani miezi minne sasa Pound nayo inachanja mbunga hata dhidi ya dollar. Ingawa matarajio ni kuwa pound itachemsha muda si mrefu kutokana na implementation ya sera yao ya kupunguza matumizi. Hapo ndio unafuu utapatikana. Cha msingi tusubiri taarifa ya kiuchumi ya robo hii ya mwaka inaweza ikarahisisha bei kwa kiasi fulani. South Africa??? Huwezi kuuziwa ya wizi kweli? Maana Afrika yetu mh!!! Wenye kauzoefu wa middle east mnasemaje?
 
Ni bora kufikiria pia ubora wa magari na ulaji wa mafuta/vipuli. Maana gari laweza kuwa na bei ndogo mwanzoni lakini ukalipia mno kulifanya libaki barabarani.
 
Back
Top Bottom