Nundu_Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 811
- 351
Kama inavyosomeka mada "Uafrika - Juu ya Yote Wafrika na Afrika", ni makala ninayoiandika, ili wote tutafakari, tujifunze na tuchunguze.
ASILI YA NENO AFRIKA
Asili ya neno "Afrika" ni neno linalotokana na neno la Kigiriki "Aphrike", kwa Kiingereza 'land that is free from cold and horror', kwa Kiswahili (tafsiri isio rasmi) 'ardhi ambayo hakuna baridi, iliyoshonana, kuogopesha na kutisha.
Neno "Afrika" linatokana na neno la Kilatini "Aprica", kwa Kiingereza "sunny", kwa Kiswahili 'Jua wakati wote'.
Pia, neno "Afrika" linatokana na neno la Phoenicians "Afar", kwa Kiingereza "dust' kwa Kiswahili "vumbi".
Phoenicians (Fonisia) hii ni jamii ya Kisemeti (Semitic). Wasemiti hawa ni wayahudi na waarabu.
NADHARIA KUHUSU AFRIKA
Asili hizi tatu za neno Afrika zimepelekea uwepo wa nadharia kadhaa kuhusu Afrika; kama ifuatavyo:
Kwanza, Nadharia ya Kirumi (The Roman Theory). Hii inaeleza neno Afrika linatokana na warumi ambao waliita eneo - ardhi walioigundua mkabara na bahari ya Mediteraniani baada ya wenyeji kabila la Beriberi waliokuwa wanaishi hapo, eneo la mji wa Carthage (sasa Tunisia).
Hatahivyo, hakuna maelezo yanayoeleza jina la moja kwa moja kwa kabila hilo lililokuwa linaishi eneo hili la Carthage. Inadhaniwa warumi waliita eneo hili 'Afri-terra', kwa Kiingereza 'the land of Afri'.
Nadharia ya Fonisia (The Phoenician Theory). Haya ni mawazo kwamba neno Afrika linatokana na maneno mawili ya Fonisia "friqi" na "pharika' yakitafsiriwa kwa Kiingereza 'corn' na 'fruit' - ambapo wafonisia waliita Afrika, ikitafsiriwa kwa Kiingereza 'the land of corn and fruit.
Hatahivyo, nadharia hii haina mvuto sana. Kwani juu ya yote, wafonisia ni jamii iliyoishi zamani sana katika miji ya pwani ya mashariki ya bahari ya Mediteraniani (maeneo ambayo sasa huitwa Syria, Lebanon na Israel).
Jamii hii walikuwa wavuvi na wafanya biashara waliokuwa wakisafiri maeneo mbalimbali hadi Misri ya zamani.
Nadharia ya Hali ya Hewa (The Weather Theory). Hii inahusu moja kwa moja hali ya hewa ya bara lenyewe la Afrika.
Nadharia inakubaliana na neno la Kigiriki "Aphrika", kwa Kiingereza 'the land that is free from cold and horror', neno la Kilatini " Aprca" kwa Kiingereza 'sunny' na neno la Kifonisia "Afar", kwa Kiingereza 'dust'.
Ingawa nadharia inaona sio sahihi kujumuhisha hali ya hewa, uoto na makazi ya nchi za Afrika kuwa ni sawa. Lakini ni kweli kuwa hali ya hewa ya Afrika ni joto, jua na vumbi ukilinganisha na mabara mengine ya dunia.
Nadharia ya Kiafrikusi (The Africus Theory). Hii inasema, bara liliitwa Afrika baada ya mtawala wa Kiyemeni aliyeitwa 'Africus' aliyevamia Afrika ya kaskazini mara nyingi katika karne ya pili kabla ya Kristo. Afrikusi alianzisha makazi yake kwenye bara aliyoyaita "Afrikyah". Akiwa na nia jina lake lijulikane aliamrisha bara liitwe jina lake, " Africus".
Hatahivyo, nadharia hii ni vigumu kuithibitisha, hata licha ya kuwa ni ya zamani sana.
Nadharia ya Kijiografia (The Geographical Theory). Hii inaeleza kwamba bara liliitwa jina Afrika kutokana na watu waliofika kwa shughuli za biashara kutoka eneo ambalo linatambulika kwa sasa kama India. Katika jamii ya "Sanskrit" na "Hindi", mzizi wa neno " Apara" au "Afrika" linamaanisha 'eneo linalofuata baada ya' kwa Kiingereza 'a place that comes after. Katika muktadha wa kijiografia (a place that comes after) ina maana ya eneo ambalo liko upande wa magharibi baada ya eneo linalotambulika kwa sasa kama India.
Nadharia hizi zote zinatupa picha kwamba, eneo ambalo hii leo linaitwa bara la "Afrika" huenda halikuwa likikaliwa na watu. Na kwamba eneo hili lilikuwa kama "Shamba", ambalo watu walifika kuvuna rasilimali mbalimbali, kisha kuondoka na kurudi. Katika hali hiyo, wapo walioamua kufanya kabisa makazi. Hili lilifanyika kwa miaka mingi sana kabla ya Kristo.
Wana- anthropologist wamegundua mafuvu ya watu katika eneo hili linaloitwa Afrika yalioonyesha miaka 500, 000 kabla ya Kristo.
WAPI MWANADAMU ALIANZA KUISHI
Kuhusu wapi mwanadamu alianza kuishi kati ya maeneo ya dunia yanayotambulika hii leo kama mabara, ni hoja inayoturejesha kutazama na kufikiri kabla ya uelewa huu wa mabara, dunia ilikiwaje?
Kuna nadharia nyingi kuhusu wapi mwanadamu alianza kuishi. Zote, hatahivyo, zinapingana wapi, hasa mwanadamu alianza kuishi kati ya maeneo tunayoita hii leo mabara. Uthibitisho wa nadharia hizi juu ya wapi hasa mwanadamu alianza kuishi kati ya mabara ya hii leo, ni ule unaoegemea maeneo ya zamani sana katika mambo ya dini, utawala na ustarabu. Hatahivyo, uthibitisho huu hauwezi kuwa njia sahihi kwa sababu ya ukweli kwamba, mwanadamu, yaani mtu ni kiumbe chenye dini, utawala na ustarabu. Asieweza kukaa eneo moja.
Jambo la kuelewa ni hili: mwanadamu kadiri alivyosambaa maeneo mabimbali ya dunii; kama tunavyoshuhudia hii leo, alitoka katika chanzo na eneo moja.
TOFAUTI ZA RANGI SIO UBINADAMU NA UTU TOFAUTI
Tofauti za kirangi zinazoweza kuwako kutoka binadamu wa eneo moja hadi jingine hazina maana kwamba, wanadamu walitokana na chanzo, na eneo zaidi ya moja. Watu wote walitoka katika chanzo kimoja na eneo moja, wakasambaa maeneo mbalimbali ya dunia kwa sababu za kiuchumi.
Kuweko kwa watu wanaotofautiana katika rangi kutoka eneo moja hadi jingine na kwa ujumla, watu wanaoishi ukanda wa Kitropiki kuwa na ngozi nyeusi kuliko wale wanaoishi ukanda wa baridi, kunaelezwa kisayansi kama suala la MAZINGIRA, MIALE YA JUA (Sun Ultraviolet (UV) radiation) na pia vyakula.
Mazingira ya joto, miale mikali ya mwanga wa jua na vyakula jamii ya seafood husababisha kuzalishwa kwa wingi melanin mwilini. Kadiri Melanin inavyozalishwa kwa wingi mwilini ndivyo rangi ya mwili inazidi kuwa nyeusi.
Ni vema kuelewa kwamba, kuwako kwa tofauti za rangi kutoka eneo moja hadi jingine sio kuwako kwa tofauti za kibinadamu. Tofauti za rangi hazina maana ni tofauti za binadamu. Kwani wote ni watu wale wale na utu ule ule mmoja.
Kibailojia hatuoni mfumo wa mwili wa mzungu kwa mfano, ulivyoumbwa na unavyofanya kazi kama ni tofauti na mfumo wa mwili wa mwafrika ulivyoumbwa na unavyofanya kazi.
Jinsi vilivyo viungo vya mwili wa mzungu ndivyo, hivyo vilivyo viungo vya mwili wa mchina, mwafrika, mwarabu, mhindi na myahudi.
Mfumo wa ubongo wa mzungu ulivyo na unavyofanya kazi ndivyo, pia ulivyo na unavyofanya kazi mfumo wa ubongo wa mwafrika, mhindi, mchina, mwarabu na myahudi.
WAFRIKA NA AFRIKA
Wafrika na Afrika ndio hasa nia na lengo la makala haya.
Kwa kuanza, niseme, ni makosa na upotofu kuelewa kwamba Afrika na Wafrika ni sehemu isio eneo na jamii ya dunia. Afrika ni sehemu ya eneo la dunia na Wafrika ni sehemu ya jamii inayounda jamii ya dunia.
Kama sehemu ya eneo na jamii ya dunia, Wafrika hawawajibiki tu kwao, lakini pia kwa jamii nyingine ya dunia.
Wafrika tusifikiri na kuelewa kwamba, wao pasipo jamii nyingine ya dunia tunaweza kujitosheleza, kujikamilisha. Mwelekeo wa namna hii ni uovu unaoharibu ukweli wa mwanadamu.
Afrika ukilinganisha na maeneo mengine ya dunia nyakati hizi, utagundua ndio eneo pekee duniani ambalo bado lina rasilimali nyingine. Ardhi yenye rutuba, rasilimali chini ya ardhi, bahari, maziwa, mito na watu wenye nguvu ya mwili.
Hapo hapo, utagundua pia Afrika ni eneo moja kati ya maeneo yaliyokaliwa na kutawaliwa na mataifa mbalimbali. Utabaini kwamba, eneo hili linalofahamika hii leo kama Afrika, wakaazi wake ni mchanganyiko wa jamii mbalimbali.
Afrika imedhihirika kuwa ndiyo eneo lililo nyuma zaidi kimaendeleo ukilinganisha na maeneo mengine ya dunia, licha ya utajiri wake mkubwa wa rasilimali.
Wakaazi wa eneo hili, yaani Wafrika ndio jamii inayokabiliwa na matatizo mengi ukilinganisha na jamii nyingine duniani.
Pia imeonekana kwamba, jamii iliyo ya kiafrika, lakini inayoishi nje ya bara la Afrika inakabiliwa na matatizo sawa na Wafrika wa Afrika.
Wafrika tunakabiliwa na matatizo ya Ndoa, Maadili, Elimu, Uongozi na Uchumi. Matatizo mengine ni Njaa, Wizi, Vurugu, Mafarakano na vita.
Lakini, je, haya matatizo chanzo chake ni nini?
Kwa nini kuna matatizo ya ndoa? Kwa nini Afrika tatizo la maadili ni kubwa? Kwa nini umasikini ni mkubwa sana Afrika? Kwa nini Afrika viongozi wanang'ang'ania sana madaraka? Kwa nini Afrika haipati manufaa ya elimu? Ni nini hasa kinasababisha kuwepo kwa haya matatizo Afrika?
Jibu la maswali haya ni DINI. Makosa ya wafrika ni dini.
Dini ndio chanzo cha matatizo yote niliyoyabainisha hapo juu.
Nitaeleza kwa kutazama na kufafanua wafrika wanavyoishi na kushikilia AMRI YA KWANZA YA MUNGU (Mche Bwana, Mungu Wako, Usiabudu miungu wengine), Amri ya sita ya Mungu (Usizini) na Amri ya Tisa ya Mungu (Usitamani mwanamke asie Mke wako). Hii ya sita na ya tisa ni ndoa.
Kimsingi Amri hizi mbili za Mungu ndio yalipo matatizo ya wafrika. Wafrika tunavyoishi na kuelewa dini na Amri za Mungu kunaakisi hivi tulivyo katika familia, jamii na taifa.
Aidha, kwa ujumla, Amri 10 za Mungu zinamkusudia mtu kwa Mungu na hapo hapo, kwa ajili ya maadili na uchumi.
Hizi, hakuna hata Amri moja isio kwa ajili ya maadili na uchumi.
MCHE BWANA, MUNGU WAKO, USIABUDU MIUNGU WENGINE
Amri hii imekumbatia Imani, Matumaini na Mapendo.
Mungu aliumba mtu akampatia akili ya ufahamu na akili ya kina. Akili ya ufahamu inaona na kuelewa kwa kutumia milango mitano ya fahamu. Na akili ya kina inatumia Imani.
Hivyo, basi, wafrika tunaamini nini? Tamaa yetu iko katika nini? Tunapenda nini?
Wafrika tunaamini miungu na sio Mungu. Tunakataa Mungu kwa dhana kwamba tulikuwa na dini yetu ya asili. Tunatumikia na kujitoa kwa miungu.
Tukiwa tuna akili tunashindwa kuelewa kama ulimwengu - ardhi, maji, anga, mimea, mwanga , jua, hewa, wanyama, giza na sisi wenyewe - dunia tumeumbwa. Sisi tumefanyika, na hivi vimefanyika kwa ajili yetu.
Wafrika imani, matumaini na mapendo yetu yapo kwa miungu - vitu na watu.
Wafrika ambao tumebatizwa - ni wakristo, utawaona wanatumikia na kushiriki ibada za asili na waganga, wanapiga ramli na bao. Utawaona wanatoa vitu vyao kwa waganga na matambiko ya asili.
Lakini, je, wafrika tunajua dini asili ni nini na ilifanyikaje? Tunajua gharama zake? Tunajua waganga, wapiga ramli na bao ni akina nani na wanafanyaje kazi? Madhara yake, je, tunayajua?
Ni hakika kabisa, wafrika hatumtumikii Mungu. Imani, matumaini na mapendo ya wafrika yapo kwa miungu. Tunamkataa Kristo kwa dhana na mawazo kwamba tulikuwa/ tuna dini yetu ya asili.
Je, ni nani aliyeachiwa mamlaka ya dini ya asili ya wafrika?
Amri ya kwaza ya Mungu inaelekeza kiumbe kufanya haya kwa Muumba (Mungu):
Kuabudu, sala na sadaka. Je, wafrika tunaabudu nini? Sadaka zetu tunazitoa wapi? Utaona wafrika tukiabudu vitu au watu, viumbe. Utaona tukitoa sadaka zetu kwa wafumu, wapiga ramli na matambiko ya asili. Huko ndiko iliko mioyo ya wafrika.
Amri ya sita (usizini) na ya Tisa (usitamani mwanamke asie mke wako) - Ndoa.
Amri ya sita inakataza uzinzi na inakataza uasherati, punyeto, urawiti, usagaji, picha chafu za ngono na matendo yote machafu, matumizi ya kondumu na kadhalika.
Ya tisa, inakataza mwanamume asitamani mwanamke asie mke wake na hapo hapo inakataza mwanamke asitamani mwanamume asie mume wake.
Amri hizi mbili zote zinaelekeza watu wasijihusishwe na namna yoyote iliyokatazwa isipokuwa ile tu iliyo halali, ndio ndoa.
Kukaidi makatazo ya amri ya sita na ya tisa ni kuvunja amri zote, ni kumkataa Mungu.
Ndoa ni sakramenti. Mwasisi wa sakramenti ya ndoa ni Mungu mwenyewe kwa ajili ya mwanadamu: mume na mke.
Kwa kuwa ndoa ni kwa ajili ya mwanadamu: mume na mke haiwezi kuwa ndoa isipokuwa kwa njia ya Kanisa lake.
Hii maana yake ni kwamba muunganiko wa mume na mke bila sakramenti ya ndoa ni hasa wa kibaiolojia tu.
Mamlaka ya sakramenti yamepewa Kanisa. Makreli ndio wanao uwezo wa kutoa sakramenti ya ndoa, kufungisha ndoa.
Hapa ni kusema, nje ya Makreli, Kanisa hakuna mtu mwingine aliye na uwezo wa kufungisha ndoa - kutoa sakramenti ya ndoa.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, wafrika wengi tulizaliwa/ tumezaliwa na tunazaliwa nje ya ndoa, nje ya mpango wa Mungu - si halali.
Wafrika wengi tunazaliwa bila wazazi wetu kufunga ndoa. Hivyo, hatuna muunganiko wa kiroho na Mungu pia wazazi wetu. Muunganiko tulionao ni wa kibaiolojia.
Hapo awali nimesema, Kanisa, yaani makreli ndio wana mamlaka ya kutoa sakramenti ya ndoa, kufunga ndoa na sio mtu mwingine.
Je, makreli ni nani?
Ni mtu "aliyetengwa" na "kuingizwa" kwa kufanyiwa tendo la kidini na la kiliturujia la sakramenti, wakfu na baraka ambalo humpatia mtu kipaji cha Roho Mtakatifu kinachomwezesha kutekeleza "uweza mtakatifu", ambao hauwezi kutoka mahali pengine isipokuwa kwa Mungu kwa njia ya Kanisa lake.
Je, kama tumefunga ndoa aliyetufungisha ni mkreli? Yaani kwamba, hayo mamlaka ya kufungisha, kutoa sakramenti ya ndoa ameyatoa kwa nani?
Wafrika tuliishi/ tumeishi na tunaishi bila ndoa. Tunaishi uasherati. Tulizaliwa/tumezaliwa na tunazaa watoto katika uasherati.
Niweke wazi kwamba, mume na mke kuishi pamoja kama mke na mume bila kufunga ndoa, kuwa na sakramenti ya ndoa, sio ndoa ni uasherati. Muunganiko huo hauna Mungu, hivyo ni dhambi, ni makosa.
Madhara yatokanayo na kuishi bila sakramenti ya ndoa ni kutokuwepo muunganiko wa kiroho kati ya wazazi na wototo. Wazazi hawana mamlaka juu ya watoto wao. Uharibifu wa akili na maadili mabaya.
Ndoa kama sakramenti, yaani inatoka kwa Mungu, ina sheria zake. Je, tunaziishi sheria za ndoa na za Mungu?
Kwetu sisi wafrika hatuishi sakramenti ya ndoa. Hatuishi na kushikilia sheria ya ndoa na Mungu.
Tunaishi sheria ya miungu - wafumu, wapiga ramli na bao.
Ni kawaida katika familia ya kiafrika baba kuwa na mtoto nje ya ndoa na mama nae.
Sisi wafrika tunamkataa Kristo. Tunafanya dhambi na makosa makubwa kufikiri na kuelewa kwamba ukristo ni dini ya wazungu.
Kama tutaendelea kumpinga Kristo kwa dhana na mawazo kwamba tulikuwa/tuna dini yetu ya asili na Ukristo ni dini ya wazungu ili watutawale, tutaendelea kuwa na matatizo karne na karne.