Uadilifu vs Uaminifu vs Uongozi. . . .Tunajidhalilisha!!

Uadilifu vs Uaminifu vs Uongozi. . . .Tunajidhalilisha!!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Katika mabara yote kasoro Africa,unapokuwa kiongozi katika ngazi yoyote kijamii na serikalini na ukagundulika una mahusiano nje ya ndoa yako,unaingia matatizoni na unapoteza wadhifa wako.Ni wachache sana waliosalimika.
"
Inaonekana wenzetu hawa wanajua thamani ya ndoa na uzito wake na wanajua ni namna gani mtu anaeitwa mume au mke alivyo na thamani na uzito mkubwa kwenye jamii
"
Kimsingi hawa wenzetu wanamhesabu mtu alieshindwa kuiheshimu ndoa yake hawezi kuiheshimu kazi au wadhifa wake kijamii au kiserikali.
"
Nakubaliana nao
"
Nakubaliana nao kwa kuwa kiongozi yoyote yule na wa kundi lolote kama haiheshimu familia yake ni vigumu sana kuheshimu watu wengine.Pia ni aibu sana kiongozi kuwa na tabia za hovyo namna hii.Kutoa toa nguo hovyo mbele ya wanawake/wanaume tena wasio na idadi ni kudhalilisha utu wako,mkeo/mumeo,familia yako na zaidi unaowaongoza
"
Nadhani umefika wakati kiongozi yoyote yule atakaegundulika anafanya mambo haya ya aibu avuliwe wadhifa wake mara moja
"
Nadhani hii itasaidia kuokoa ndoa za viongozi na kuwaokoa mabinti wadogo na vijana kuharibiwa masomo yao na maisha kwa ujumla
"
Wakati wa bunge vyombo vya habari huripoti wingi wa wanawake wanaouza miili yao kujazana kwenye viunga vya mji wa Dodoma,wanafuata nini,na ni kwa nini iwe wakati wa bunge?
"
Hivi kiongozi anashindwa kuheshimu kipato chake na kukitapanya hovyo kwa changudoa au vijana wadogo,hivi unadhani ataheshimu vipi fedha za miradi ya maendeleo?Ikifika wakati wa kufanya uteuzi unadhani hatawateua mahawara zake?
"
Nadhani tuzinusuru ndoa za hawa watu na jamii yetu kwa kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote kijamii na kiserikali wanaotia aibu kwa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao!
 
Na itabidi mtu yoyote akitaka wadhiwa wowote ajipime katika uaminifu na uadilifu kwa familia yake
"
Hatuwezi kuwa na meneja wa benki ambae amemtelekeza mkewe kwa kumuona mfanyakazi mpya kwenye tawi la benki anayoisimamia na kumuwakia tamaa.
"
Anatakiwa ajiheshimu,amuheshimu mkewe,kazi yake familia na jamii kwa ujumla
"
Kama hawezi aachie ngazi!
 
Mume wangu mpenzi, mada kama hizi si rafiki na majority ya MMU members.
Lakini pia pamoja na kuwa umeiweka MMU, ilipaswa pia kukaa siasa; maana umebase kwenye maadili ya uongozi, ingawa na huko huenda ikasomwa lakini haitachangiwa sana.

Nakubaliana na wewe; na kwa maoni yangu watu wenye mahusiano mengi wana shida ya kutojiamini na kujikubali wenyewe. So kwa kutumia au pesa au wadhifa basi anatafuta kukubaliwa (kuwa admired hata kiuongo uongo) na watu wengine.

Chukulia watu wazima walioko kwenye mid life crisis; wana wasiwasi sana kuhusu kuzeeka na kushindwa kuwa na nguvu kama ujanani; hivyo basi wanatafuta vibinti vidogo at least wajiaminishe au kujidanganya kuwa bado 'wanadai'.

Wenye shida ya nguvu za kiume, mifano ni mingi tu; wanatoka na wanawake wengi wengi tu, halafu hao wadada wanakuja wanatoa siri zao "jamaa hana kitu yule, atakunyonya tu unaondoka na mpunga wako".

Haya turudi kwenye hali ya kawaida, umeachwa na mwanaume au mwanamke; confidence inashuka, ili kuirudisha wengi huanzisha mahusiano mapya au hata kujirahisisha kwa watu wengine ili wajione kuwa bado wanakubalika.

Kwa mifano hiyo michache, ninaona uhusiano wa mashusiano ya ngono kutumika katika kuboost confidence; sasa kwa kiongozi ambaye anavua pants zake hovyo hovyo ni wazi kuwa yeye mwenyewe hajiamini na sidhani kama kutojiamini ni sifa nzuri kwa kiongozi.
 
Mai waifu,najua tatizo la hapa,lakini hali hii haiwezi kutufanya tusiambiane mambo ya msingi
"
Kaunga ,mahusiano ni suala pana sana unapozungumzia viongozi haimaanishi ni siasa zinazohusu serikali tu.
"
Hapa nazungumzia mahusiano ya viongozi,hatuwezi kuipeleka mada hii huko,na MOD atakaeipeleka huko hatakua ameitendea haki
"
Lakini pia kwa maana ya siasa hata hapa MMU tunafanya politic pia.Kitendo cha kujibishana tunakua tunafanya siasa.Tofauti ni aina ya siasa tu(source Iron Lady ,nakubaliana nae)
"
Hivyo hapa tunafanya siasa za MMU!
 
Last edited by a moderator:
Habari ni nzuri na ina mantiki ndani yake...lakini je, nani wa kumvisha paka kengele???
Katika mataifa ya wenzetu viongozi wao wana maadili ya uongozi na kiongozi akutwapo na kashfa yoyote ya mahusiano ni rahisi kujiwajibisha.
 
Habari ni nzuri na ina mantiki ndani yake...lakini je, nani wa kumvisha paka kengele???
Katika mataifa ya wenzetu viongozi wao wana maadili ya uongozi na kiongozi akutwapo na kashfa yoyote ya mahusiano ni rahisi kujiwajibisha.

Tutengeneze katiba nzuri yenye kuwagiza viongozi kuziheshimu ndoa zao!
 
wezi wa epa/bot etc, walioweka fedha uswizi hawajawajibishwa mpaka leo. yule former PM anataka kujisafisha ili awanie uraisi 2015.... obvious infractions kama hizi haziwezi kutatuliwa ndio sembuse infidelity kwenye ndoa. wazo lako ni zuri lakini it's too far away it can't be practical. labda kwa wajukuu wetu and even then i doubt it >;
 
Blaine usijali,tunaweza bila tatizo lolote suala ni kuamua tu!
 
Last edited by a moderator:
Tutengeneze katiba nzuri yenye kuwagiza viongozi kuziheshimu ndoa zao!

Hilo litawezekana vipi wakati sheria ya kufunga ndoa ipo chini ya uangalizi wa IMANI, na katiba inatambua uwepo wa imani lakini haiingilii utendaji kazi wake.
 
Back
Top Bottom