Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
IKO SIKU ITAFIKA, UA NITAKUJA SHIKA
1. Ua langu liko mbali, Salamu ninazituma,
Japo kuwa niko mbali, mtu asijelichuma,
Utakuwa ukatili, Moyo uje kuniuma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.
2. Ua langu lapendeza, maji nimelimwagia,
Namshukuru Muweza, uzuri kalijalia,
Akili yangu kupoza, ninapolifikilia,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
3. Ua langu maridadi, rangi nzuri lajaliwa,
Nikaiweka ahadi, hilo langu litakuwa,
Watakuwa mashahidi, siku ile itakuwa,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
4. Ua langu tofauti, mfanowe sijaona,
Marekani katikati, jingine kweli hakuna,
Ndipo nikajizatiti, mwingine hatolivuna,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.
5. Ua langu la milele, ndotoni mwangu daima,
Na wanionee gele, wale wataka kuchuma,
Sasa napiga kelele, Jamani mrudi nyuma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
6. Ua langu kushamiri, sitaacha linyauke,
Leo nawapa habari, karibu huko nizuke,
Na wale wenye kiburi, aibu ije washike,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
7. Ua langu limedumu, kwa mvua na jua kali,
Wabaya wakalaumu, mwenye lake yuko mbali,
Wakabaki kushutumu, Nyikani eti hajali,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.
8. Ua langu ndilo zuri, hakika nawaambia,
Lapita hilo waridi, sifa ninawatajia,
Rangi zake mashuhuri, Manani kalijalia,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
9. Ua langu linang'ara, jua linapochomoza,
Usifanye masikhara, hilo ua lapendeza,
Kati ya hivyo vinara, ua langu latokeza,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.
10. Ua langu nasifia, wewe wangu mimi wako,
Mola atatujalia, niwe ubavuni mwako,
Rafiki kushangilia, furaha yangu ni yako,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
11. Ua langu nakuaga, kalamu yangu yagoma,
Mtama sitaumwaga, wengine wasijechuma,
Pale nitapokanyaga, walo sema watakoma,