Ua langu liko mbali

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
IKO SIKU ITAFIKA, UA NITAKUJA SHIKA
1. Ua langu liko mbali, Salamu ninazituma,
Japo kuwa niko mbali, mtu asijelichuma,
Utakuwa ukatili, Moyo uje kuniuma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

2. Ua langu lapendeza, maji nimelimwagia,
Namshukuru Muweza, uzuri kalijalia,
Akili yangu kupoza, ninapolifikilia,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

3. Ua langu maridadi, rangi nzuri lajaliwa,
Nikaiweka ahadi, hilo langu litakuwa,
Watakuwa mashahidi, siku ile itakuwa,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

4. Ua langu tofauti, mfanowe sijaona,
Marekani katikati, jingine kweli hakuna,
Ndipo nikajizatiti, mwingine hatolivuna,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

5. Ua langu la milele, ndotoni mwangu daima,
Na wanionee gele, wale wataka kuchuma,
Sasa napiga kelele, Jamani mrudi nyuma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

6. Ua langu kushamiri, sitaacha linyauke,
Leo nawapa habari, karibu huko nizuke,
Na wale wenye kiburi, aibu ije washike,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

7. Ua langu limedumu, kwa mvua na jua kali,
Wabaya wakalaumu, mwenye lake yuko mbali,
Wakabaki kushutumu, Nyikani eti hajali,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

8. Ua langu ndilo zuri, hakika nawaambia,
Lapita hilo waridi, sifa ninawatajia,
Rangi zake mashuhuri, Manani kalijalia,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

9. Ua langu linang'ara, jua linapochomoza,
Usifanye masikhara, hilo ua lapendeza,
Kati ya hivyo vinara, ua langu latokeza,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

10. Ua langu nasifia, wewe wangu mimi wako,
Mola atatujalia, niwe ubavuni mwako,
Rafiki kushangilia, furaha yangu ni yako,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

11. Ua langu nakuaga, kalamu yangu yagoma,
Mtama sitaumwaga, wengine wasijechuma,
Pale nitapokanyaga, walo sema watakoma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
 
mwanakijiji utafikiri mloka,kweli umejahaliwa katika hiyo fani,unajua hii imenigusa sana,ukichukulia ni kweli nipo ughaibun ila nina ua langu nyumbani na nimejizatiti kulichuma mwenyewe tu.yaani hapa mwili wote unanisisimka,duh imetulia
 
Mwana huu utamu nilikuwa sijautafutia muda wa kuusoma ila leo sasa ndio nimejuwa kwanini watu wanatoa Thanks. Kweli Ua limetulia na Mungu akubariki wewe na Ua mdumu daima.
 
Wakijiji kweli wajua,ua kulisifia
Matambo umetoa,sauti tumesikia
Kweli litafurahia,sifa kukumwagia
Lakini zingatia,hiki nachokwambia,

karibu au kwa mbali,ua linanukia
Si harufu ya wali,samaki au bamia
Haifanani asali,dagaa kwenye gunia
Hata ukiwa mbali,kweli inavutia

Tabu ya ua la mbali,ni hii nayokwambia
We enda zako safari,lobaki latuvutia
Lilivojazia hatari,mate yachuruzikia
Hata likiwa ngangari,Ni rahisi kuibia

Nalo lapata hisia,Kama ilivo zabibu
Laweza kuvumilia,lingoje uje karibu
Ila siku zaishilia,halimuoni tabibu.
Nasi twamfarijia,Tuondoe nazo tabu

Kwa undani lafikiri,mbali huko ulipo
Maua kwa utitiri,utakua wachumapo
Jinsi ulivo rijali,Huwezi vumiliapo
Ua likiwa mbali,lazima ipo hatari

Miezi kenda yapita,Ua kati lachanua
Wapiga simu yaita,Ua labaki kulia
Wakazana shituka,Nini ua lalilia
Kati ua lafutuka,Chako sio kwambia
Ua likiwa mbali,lazima ipo hatari
 
Wa kijiji naomba uwe unatukumbusha na vitu vya wakongwe kama kina saadan kandoro.

Nakumbuka kuna tungo moja ina ubeti mmoja unasema

ukatendewa ubaya,nawe ukatenda wema
yawe yako mazoea, maisha dumu daima
kwa mola nakuapia, utakuwa na heshima
binadamu tenda wema, japo utendwe ubaya.

Ni raha tupu.
 
IKO SIKU ITAFIKA, UA NITAKUJA SHIKA
1. Ua langu liko mbali, Salamu ninazituma,
Japo kuwa niko mbali, mtu asijelichuma,
Utakuwa ukatili, Moyo uje kuniuma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

mie wala sijipi moyo,
ua langu lishakuwa tunda,
nachelea kuibiwa,
ka' yalomsibu bw' Bushiri!

Siogopi kuja bambwa, na yeye bwana Bushiri,
Ni fumbo lilifumbwa, tunda sitalighairi,
Hata akileta Mbwa, nalifunguia safari,
Kula tunda kwa kuiba, kwa nini huko kutamu?
 
IKO SIKU ITAFIKA, UA NITAKUJA SHIKA
1. Ua langu liko mbali, Salamu ninazituma,
Japo kuwa niko mbali, mtu asijelichuma,
Utakuwa ukatili, Moyo uje kuniuma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

2. Ua langu lapendeza, maji nimelimwagia,
Namshukuru Muweza, uzuri kalijalia,
Akili yangu kupoza, ninapolifikilia,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

3. Ua langu maridadi, rangi nzuri lajaliwa,
Nikaiweka ahadi, hilo langu litakuwa,
Watakuwa mashahidi, siku ile itakuwa,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

4. Ua langu tofauti, mfanowe sijaona,
Marekani katikati, jingine kweli hakuna,
Ndipo nikajizatiti, mwingine hatolivuna,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

5. Ua langu la milele, ndotoni mwangu daima,
Na wanionee gele, wale wataka kuchuma,
Sasa napiga kelele, Jamani mrudi nyuma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

6. Ua langu kushamiri, sitaacha linyauke,
Leo nawapa habari, karibu huko nizuke,
Na wale wenye kiburi, aibu ije washike,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

7. Ua langu limedumu, kwa mvua na jua kali,
Wabaya wakalaumu, mwenye lake yuko mbali,
Wakabaki kushutumu, Nyikani eti hajali,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

8. Ua langu ndilo zuri, hakika nawaambia,
Lapita hilo waridi, sifa ninawatajia,
Rangi zake mashuhuri, Manani kalijalia,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

9. Ua langu linang'ara, jua linapochomoza,
Usifanye masikhara, hilo ua lapendeza,
Kati ya hivyo vinara, ua langu latokeza,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma.

10. Ua langu nasifia, wewe wangu mimi wako,
Mola atatujalia, niwe ubavuni mwako,
Rafiki kushangilia, furaha yangu ni yako,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma

11. Ua langu nakuaga, kalamu yangu yagoma,
Mtama sitaumwaga, wengine wasijechuma,
Pale nitapokanyaga, walo sema watakoma,
Ua langu Ua langu, mwenyewe nitalichuma
Superb!!!!!!
 
Back
Top Bottom