U-Kamanda wa CCM

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,076
2,443
Wakuu,

Mara kwa mara nimekuwa nikisikia kwenye vyombo vya habari kuwa mtu fulani amesimikwa kuwa Kamanda wa CCM. Na siku za hivi karibuni kuna amesimikwa Kamanda wa UVCCM Kibaha.

Ningependa kufahamishwa hiki cheo cha U-Kamanda, ni nini hasa nafasi/madhumuni/malengo yake katika Chama Cha Mapinduzi?

BE
 
Mkuu halafu cha ajabu hao makamanda wenyewe ni wazee wazima kama yule wa mchafukoge sijui jibaba kabsaa
 
Mkuu halafu cha ajabu hao makamanda wenyewe ni wazee wazima kama yule wa mchafukoge sijui jibaba kabsaa

Yeah - ukiachana na Shy-Flower, ambaye amesimikwa Kamanda wa Kijito-Mchuzi hivi majuzi wengi wao ni wazee sana kiasi kwamba mantiki ya neno Kamanda inapotea!

wakuu,

mara kwa mara nimekuwa nikisikia kwenye vyombo vya habari kuwa mtu fulani amesimikwa kuwa kamanda wa ccm. Na siku za hivi karibuni kuna amesimikwa kamanda wa uvccm kibaha.

ningependa kufahamishwa hiki cheo cha u-kamanda, ni nini hasa nafasi/madhumuni/malengo yake katika chama cha mapinduzi?

be

kuhamasisha ushindi kwa gharama yeyote ile....kwa mwaka wa uchaguzi kama huu una malengo ya ubunge ..thats why....
 
si bado wako kwenye vita!!!kamanda ndo wapiganaji hasa katika vita!! Hivyo kuitwa kamanda, ina maana ni mpiganaji!! Sidhani kama ni cheo specific unachoweza kuweka katika CV!!!
 
Hii simple hata wewe ukiwa na fweza basi una andaa watu unamwaga mpunga unaandaa wapambe alafu unaandaa mgeni lasmi unagawa fweza kwa vyombo vya habari basi mtu unapewa shavu Kamanda wa vijana Baba_Enock unasimikwa hapo ni fweza tu hakuna kingine unapewa promo.
 
Mkuu halafu cha ajabu hao makamanda wenyewe ni wazee wazima kama yule wa mchafukoge sijui jibaba kabsaa

Yaani hawa CCM wamechoka kweli kuna huyu wa kinondoni alisimikwa mbele ya IDD AZAN..anaitwa KIMWANA SHIRRALLY mmama mtu mzima kabisa sijui hata imetokeaje...mmmmh yaani siku nilipomwona nikaangalia mara mbili mbili huyu Mamam mzima kabizsa na wajukuu jamani!!!kamanda katokea wapi??
 
Ninavyofahamu kusimikwa kua "kamanda wa UVCCM" zamani ilikua inamaanisha msimikwa anakua mlezi wa Umoja uo(kama nikikosea nisahiishe) ndio maana kulikua na makamanda vikongwe kama Mzee kawawa(R.I.P) na Mzee Malecela.Walikua wanapewa watu waliobobea kwenye chama, Kwa sasa naona "ukamanda" umezingirwa na sanaa nyingi za kisiasa.Matokeo yake yoyote mwenye vijisenti anaweza kua kamanda. Kuna haja kwa wahusika kutafuta maana mpya ya cheo hicho.
 
Ukamanda ni njia rahisi ya kuonesha kuwa unakubalika na vijana na ukiwa tayari kugombea basi tayari una kaujiko. Utaona makamanda wengi leo hii ni wale ambao wanatarajia hata kugombea majimbo ambayo wao tayari ni makamanda!
 
- Ni uhuru wa wananchi kujiamulia mambo yao katika vyama vyao vya siasa bila kuingiliwa na serikali, yaani ni demokrasia at large!

Respect.

FMEs!
 
Huu ni utaratibu ndani ya chama cha CCM cha kutambua michango ya baadhi ya wanachama wake...ni heshime zaidi kuliko cheo.....hata mimi naupata hvi karibuni....
 
Hiki Cheo kipo kwenye katiba ya UVCCM au CCM?

knighthood? or what? bado sijapata jibu toshelezi!
 
Najaribu ku-compile hii list labda nitapata kujua wajibu wa Ma-Kamanda wa CCM:-
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Kamanda wa UVCCM - Mzee Rashid Kawawa (RIP)

1. Ally Maswanya kamanda wa vijana wa ccm wa wilaya Urambo
2. George Kakunda kamanda wa vijana wa ccm wa wilaya ya Sikonge
3. Amos Makalla kamanda wa vijana wa ccm wa wilaya ya Mvomero
4. Hezekiah Chibunje kamanda wa vijana wa ccm wa Mkoa wa Dodoma,
5. Zabein Mhita yeye ni kamanda wa vijana wa ccm wa Kondoa Kaskazini
6. Job Ndugai, kamanda wa vijana wa ccm wa Kongwa
7. Laurent Hoya kamanda wa vijana wa ccm wa Chamwino
8. Mathias Mushuti kamanda wa vijana wa ccm wa Muleba
9. David Mathayo kamanda wa vijana wa ccm Same
10. Adam Simba kamanda wa vijana wa ccm wa Mkoa wa Kilimanjaro
11. Christopher Awina kamanda wa vijana wa ccm wa Hai
12. Aggrey Marealle kamanda wa vijana wa ccm wa Moshi Mjini
13. Suleimani Suma kamanda wa vijana wa ccm wa Mwanga
14. Regina Chonjo kamanda wa vijana wa ccm wa Moshi Vijijini
15. Getrude Mongella kamanda wa vijana wa ccm wa Mkoa wa Mwanza
16. Didas Masaburi kamanda wa vijana wa ccm Ilala
17. Haroun Kondo kamanda wa vijana wa ccm Kilombero
18.
 
Ukamanda ni njia rahisi ya kuonesha kuwa unakubalika na vijana na ukiwa tayari kugombea basi tayari una kaujiko. Utaona makamanda wengi leo hii ni wale ambao wanatarajia hata kugombea majimbo ambayo wao tayari ni makamanda!

Na wale makomredi je???
 
Kazi yao kubwa ni kuchekesha. in ashangaza kwa chama kikongwe kama hicho na kinachodai kuwa serious kinakuwa na mambo ya ajabu na ya kipuuzi kabiksa kama haya. Ndiyo maana nchi imekwama.

Kama una haja ya kuona cartoon ya bure, ngoja siku CCM wanafanya Mkutano wao Mkuu (general Congress) kule Kizota Dodoma. Hawa makamanda kutoka nchi nzima huwekwa pamoja wakiwa wamevaa 'sare' zao. Nimeweka mabano bcoz siyo sare per se kwani kila moja ina mshono wa peke yake na huunganishwa kwa ile rangi tu ya green, ambayo nayo hutofautiana.

Kutokana na umri wa wengi wao, huwezi kuacha kuvunja mbavu jinsi wanavyoonekana -- ni vikaragosi vimekwisha kazi! na ngojea basi wanapoimba. Akina Tom na Jerry ni wanafunzi tu kwa kuvunjisha watu mbavu.
 
Hapo umenena, Mvuta Ganja. Ni vichekesho vitupu, nothing but sheer stupidity. labda pia ni namna ya CCM kuingiza watu wengi katika mkao wa kuila ile national cake, katika ngzi za chini.
 
Back
Top Bottom