Tz ijitoe East Africa, ijiunge na SADC

Tz ijitoe East Africa, ijiunge na SADC

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2008
Posts
2,502
Reaction score
743
ninaamini, ni muda muafaka kwa tz kujihusisha zaidi na wale walioonekana kama ndugu zetu zaidi, yaani raia wa sadc kuliko EAC. hili litakuwa pigo kubwa kwa wakenya, kwasababu hata kama kenya wameita mkutano wa common market kwa uganda na Rwanda, bidhaa zao zikipigwa kodi kubwa hapa tz, itakuwa adhabu kubwa sana kwao, ili rwanda na uganda wabakie kama masoko tu na watumwa wa bidhaa za kenya, sisi watz tutaendelea na kuelekeza mambo yetu zambia,congo, burundi, malawi na zimbabwe. africa kusini tusiisahau hata tukiwa watumwa wao kwa bidhaa hapa tz.

ni faida kuwa katika sadc kuliko kuwa katika east africa community. ngoja tuone wataishia wapi hao uhuru, kagame na m7.
 
Katika mambo ambayo Mh Idd Simba (alipokuwa waziri wa viwanda na biashara) huwa namkubali (pamoja na makandokando yake) ni pale aliposimama kumshawishi President Mkapa kuhusu hili suala la PTA/COMESA ambalo wakati ule lilionekana kudhoofisha au kupingana na EAC ikiwa ndio kwanza inafufuliwa, mwisho wa siku mzee Ben alikubali, nadhani matunda yake ndiyo haya wanapotokea manyang'au wanapotaka kutugeuka ndani ya EAC. Lakini Mh Zitto kabwe alishawahi kuishauri serikali mara nyingi tu kuwa DRC ishawishiwe kujiunga EAC pamoja na Comoro hasa baada ya kuisaidia kumtoa Kanali Bakari ili tuneutralize kura za block linaloonekana dhahiri kuwa la Kenya, Uganda na Rwanda.
 
Lakini mbona JK na wenzake walikuwa mstari wa mbele kuwasaidia jubilee kuingia madarakani na sasa naona wanawaletea dharau.
Lakini mkuu usisahau kuwa kujitoa maana yake Mh. Sitta anapoteza nafasi yake ya ajira na kuna VX si chache zinazoenda kwa jina la EAC, angalia kotekote!
 
ninaamini, ni muda muafaka kwa tz kujihusisha zaidi na wale walioonekana kama ndugu zetu zaidi, yaani raia wa sadc kuliko EAC. hili litakuwa pigo kubwa kwa wakenya, kwasababu hata kama kenya wameita mkutano wa common market kwa uganda na Rwanda, bidhaa zao zikipigwa kodi kubwa hapa tz, itakuwa adhabu kubwa sana kwao, ili rwanda na uganda wabakie kama masoko tu na watumwa wa bidhaa za kenya, sisi watz tutaendelea na kuelekeza mambo yetu zambia,congo, burundi, malawi na zimbabwe. africa kusini tusiisahau hata tukiwa watumwa wao kwa bidhaa hapa tz.

ni faida kuwa katika sadc kuliko kuwa katika east africa community. ngoja tuone wataishia wapi hao uhuru, kagame na m7.

Hakuna sababu ya kuvunja muungano kwavile tu unapita kwenye misukosuko. Tanzania tunatakiwa tuangalie mbele zaidi badala ya kuangalia tu wenzetu wanachofanya. Hiyo mipango ya Kenya, Uganda na Rwanda haituhusu, lakini tunatakiwa kupanga ya kwetu kwa manufaa yetu.

  1. Kuna msemo unaosema ukijenga watakuja, ni kwa nini hatukufikiria kujenga sisi wenyewe reli na barabara zetu siku nyingi k.m. mpaka Bukoba, kwa matumizi ya raia wetu na nchi jirani ili tuone kama Burundi, Rwanda, DRC na Uganda hawatazitumia kama zitawapa nafuu ya bei na muda kuliko Kenya-Mombasa?
  2. Kwa nini tusiongeze ubora wa utendaji wa bandari zetu zote pamoja na miundo mbinu ya kuzifikia ili ziwe bora na rahisi kutumia kuliko majirani zetu?
Kenya wana haki ya kuchukua advantage ya uzembe wetu, bahati nzuri bado tunao uwezo wa kubadili hiyo
hali kama tu tutakuwa makini, kwani jeografia ya Mombasa vs Tanga, Dar or Mtwara hazitabadilika. Lakini pia tujue kuwa muda hautusubiri na ndege wa asubuhi ndiye anayefaidi majongoo.
 
Tanzania ni mwanchama wa jumuiya za kimataifa na kimaeneo, ndiyo kusema Jumuiyaya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika(SADC). Jumuiya ya Afrika Mashariki ina nchi wabia tatu:Uganda, Kenya, na Tanzania.
Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianzishwa chini ya mkataba uliotiwa saini na nchi wabia Novemba 30, 1999.kwa kuanzia, Jumuiya itaunda umoja wa forodha na soko la pamoja ambazo mikataba yake inatarajiwa kukamilishwa kutiwa saini katika kipindi cha miaka minne kuanzia Novemba 1999.Hatua nyingine za ufungamanisho ni kuundwa kwa umoja wa mambo ya fedha na hatimaye uundaji wa shirikisho.Jumuiya ya Afrika Mashariki inanuia kuimarisha utengamano wa uchumi wa nchi hizi kwa kutoa vipaumbele, na kwa misingi ya vitendo, ikiwemo kufanikisha biashara kwa kulinganisha ushuru, malipo, usafiri, matembezi ya watu mipakani, na kusawazisha nyanja nyingtine zenye maslahi ya pamoja, kama vile siasa, jamii na utamaduni. Uanachama wa Tanzania SADC ulianzia pale ilipoanzishwa jumuiya hiyo mapema miaka ya 80.Jumuiya ya SADC ni ya nchi 13 ambazo ni Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Muaritius, Msumbiji, Namibia, Afrikaya Kusini, Swaziland, Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Wanachama wa SADC walitia sainihati za awali za mkataba wa biashara Januari 25, 2000,wenye lengo la kuanzisha eneo huru kwakuondoa vikwazo vya biashara na huduma, kuweka sheriazifaazo za biashara (kukataza kuuza kwa bei nafuu katika nchi nyingine bidhaa zisizotakiwa soko la nyumbani, ruzuku, kufidia ushuru na ulindajiwa biashara).Eneo huru la biashara la SADC linatarajiwa kuwa litaanzishwa katika kipindi cha miaka nane kuanzia Septemba, 2000.Tanzania pia imejifunga katika mipango mingine ya kimataifa, kama ile ya Shirika la Biashara Duniani(WTO), Afrika, Caribean-Pasifiki (ACP) na Umoja wa Ulaya (EU)
UANACHAMA NA NCHI JIRANI NA ZA KIMATAIFA KATIKA MAKUNDI YA KIUCHUMI
JUMUIYA YA MAENDELEO YA NCHI ZAKUSINI MWA AFRIKA (SADC)
Madhumuni:
Kukuza maendeleo ya uchumi unaojitegemea na muungano katika nchi za SADC pamoja na kuendeleza amani na usalama katika nchi hizo.
Mipango mikuu inayoendelea
Utekelezaji wa SADC programme of Action unajumuisha yafuatayo:-
¡§Mpango wa SADC wa Takwimu.
¡§Mpango wa SADC wa kudhibiti madawa.
¡§Mpango wa SADC wa jinsia
¡§Mpango wa SADC wa kufikia kilele cha uchumi (SADC EconomicSummit Programme).
¡§Itifaki kuhusu Ruksa na Upendeleo (Immunities and privileges).
¡§Itifaki kuhusu mifumo ya mgao wa mwenendo wa maji (shared water course systems).
¡§Itifaki kuhusu Nishati
¡§Itifaki kuhusu usafirishaji mawasiliano naHali ya Hewa.
¡§Itifaki kuhusu Biashara
¡§Itifaki kuhusu kupambana na Biashara ya Madawa ya kulevya (Combating Illicit and Drug Trafficking).
¡§Itifaki kuhusu madini.
¡§Itifaki kuhusu Elimu na Mafunzo.
¡§Itifaki kuhusu utalii.
Anwani:
Katibu wa SADC
Private Bag 0095
Government Enclave
Gabarone
BOTWASANA
Website: www.sadc.com
JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)
Madhumuni:
Kuimarisha ushirikiano wa uchumi, jamii, utamaduni, siasa, teknolojia na ushirikiano mwingine kwa kuleta maendeleosawa na ya kudumu ya nchi husika (Tanzania, Kenya, Uganda).
Mipango mikuu inayoendelea:
Kutathimini Mpango wa Maendeleo ya EAC kwa kipindi cha1999-2000 na kuridhia mpango wa maendeleo wa EAC kwa 2001-2005.Mipango inayoanzishwa na iliyopo inahusuyafuatayo:
¡§Kuanzisha pasi/pasipoti za kusafiria zilizo sawa kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na utoaji wa vitambulisho vya kitaifa.
¡§Kuanzisha nyumba ya biashara (Stock Exchange) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na soko la fedha (Capital Market).
¡§Kupunguza urasimu katika kutayarisha hati za wateja (simplification of customers documentation).
¡§Kupunguza viwango vya kodi kufuatana na mapendekezo ya ¡°Cross Border Initiative - CBI)¡±.
¡§Itifaki juu ya kupambana na Biashara ya Madawa ya kulevya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
¡§Itifaki juu ya kuwa na viwango vilivyosawa, bidhaa zilizo mathubuti, Hali ya Hewa na Uchunguzi (Standardisation, Quality Assurance Meteorology and Testing).
¡§Uchunguzi wa Sheria za taratibu kwa ajili ya mikutano ya Wakuu wa nchi (Observance of the rules of procidure for the summit of heads of state).
¡§Uchunguzi wa sheria za taratibu kuruhusu nchi za nje katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
¡§Uchunguzi wa sheria za taratibu za kuruhusu
¡§waangalizi/wachunguzi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
¡§Itifaki juu ya kuanzisha muungano wa ushuru wa forodha kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki iko katika hatua za mwisho.
Anuani:
Katibu wa Tume ya EAC
S.L.P. 1096
Arusha
TANZANIA
Website: http/hometwiga@.com/eac
 
tatizo sio kuwa EAC au SADC, tatizo ni viongozi wetu mbumbumbu wasiojua nini wanataka kwa faida ya taifa, kwani hata tukiamia huko SADC tukiendelea na watawala wa namna hii muda sio mrefu mtataka tuhamie Ecowas, hebu tujiulize sisi katika SADC tunauza nini? au ndo' tabia ile ya kuwa vimbelembele kwenye siasa za matifa mengine huku uchumi wetu ukiendelea kuteketea..?
TAFAKARI CHUKUA HATUA....

Exactly, no one is isolating anybody. This thing is just in your thoughts. Do your things right and all others will fall in place. If you build good roads, railways etc, these other countries will come in to use them provided there is the advantage of doing so compared to the alternative.
Even in SADC you may soon complain especially if you only end up there as a spectator. Countries with a bigger economic muscle there will naturally dominate the others and dictate the pace of things much to your chagrin.
 
tatizo sio kuwa EAC au SADC, tatizo ni viongozi wetu mbumbumbu wasiojua nini wanataka kwa faida ya taifa, kwani hata tukiamia huko SADC tukiendelea na watawala wa namna hii muda sio mrefu mtataka tuhamie Ecowas, hebu tujiulize sisi katika SADC tunauza nini? au ndo' tabia ile ya kuwa vimbelembele kwenye siasa za matifa mengine huku uchumi wetu ukiendelea kuteketea..?
TAFAKARI CHUKUA HATUA....

Umenena mkuu!Tatizo tunaangalia mambo kwa mtazamo finyu wa kisiasa tu na kusahau kuwa sisi wenyewe ndio tatizo.Hata tukihamia SADC,kwa 'michakato yetu isiyoisha' tutaendelea kulialia tu kuwa tunatengwa.
 
ninaamini, ni muda muafaka kwa tz kujihusisha zaidi na wale walioonekana kama ndugu zetu zaidi, yaani raia wa sadc kuliko EAC. hili litakuwa pigo kubwa kwa wakenya, kwasababu hata kama kenya wameita mkutano wa common market kwa uganda na Rwanda, bidhaa zao zikipigwa kodi kubwa hapa tz, itakuwa adhabu kubwa sana kwao, ili rwanda na uganda wabakie kama masoko tu na watumwa wa bidhaa za kenya, sisi watz tutaendelea na kuelekeza mambo yetu zambia,congo, burundi, malawi na zimbabwe. africa kusini tusiisahau hata tukiwa watumwa wao kwa bidhaa hapa tz.

ni faida kuwa katika sadc kuliko kuwa katika east africa community. ngoja tuone wataishia wapi hao uhuru, kagame na m7.

Tatizo kubwa lililopo ni kwamba Wakenya wanataka kumilikishwa ardhi ya Tanzania, wamekuwa na hasira wanapoona tunakataa kuingiza sera hiyo katika makubaliano. Hakika SADC poa kabisa sisi tunafit kokote kule.
 
tatizo sio kuwa EAC au SADC, tatizo ni viongozi wetu mbumbumbu wasiojua nini wanataka kwa faida ya taifa, kwani hata tukiamia huko SADC tukiendelea na watawala wa namna hii muda sio mrefu mtataka tuhamie Ecowas, hebu tujiulize sisi katika SADC tunauza nini? au ndo' tabia ile ya kuwa vimbelembele kwenye siasa za matifa mengine huku uchumi wetu ukiendelea kuteketea..?
TAFAKARI CHUKUA HATUA....

I have asked that question before and would like to know really what does TZ sell in SADC? Atleast TZ sells toothpaste to EAC member states. To me South Africa uses the other counties in SADC for its own benefit. Even Tanzania breweries is owned by SAB Miller. Funny thing is, when Kenya wanted to build an Airport in Taita Taveta, Tanzania's legislatures rushed to the EAC parliament to oppose the plan saying it would be a competition to Kilimanjaro Int Airport and it amounts to economic sabotage, but now they are planning to build the Bagamoyo port btn Msa and Dar...so which of the 2 will go under?
 
Mdau kbm Tanzania Ipo Jumuiya ya Ulaya tena mmmh! Imejifunga?
 
Last edited by a moderator:
Hakuna sababu ya kuvunja muungano kwavile tu unapita kwenye misukosuko. Tanzania tunatakiwa tuangalie mbele zaidi badala ya kuangalia tu wenzetu wanachofanya. Hiyo mipango ya Kenya, Uganda na Rwanda haituhusu, lakini tunatakiwa kupanga ya kwetu kwa manufaa yetu.

  1. Kuna msemo unaosema ukijenga watakuja, ni kwa nini hatukufikiria kujenga sisi wenyewe reli na barabara zetu siku nyingi k.m. mpaka Bukoba, kwa matumizi ya raia wetu na nchi jirani ili tuone kama Burundi, Rwanda, DRC na Uganda hawatazitumia kama zitawapa nafuu ya bei na muda kuliko Kenya-Mombasa?
  2. Kwa nini tusiongeze ubora wa utendaji wa bandari zetu zote pamoja na miundo mbinu ya kuzifikia ili ziwe bora na rahisi kutumia kuliko majirani zetu?
Kenya wana haki ya kuchukua advantage ya uzembe wetu, bahati nzuri bado tunao uwezo wa kubadili hiyo
hali kama tu tutakuwa makini, kwani jeografia ya Mombasa vs Tanga, Dar or Mtwara hazitabadilika. Lakini pia tujue kuwa muda hautusubiri na ndege wa asubuhi ndiye anayefaidi majongoo.

Hoja zako ni nzito na ni vigumu sana kutofautiana nazo lakini ni kisiasa zaidi na si kisayansi zaidi.
Kuna sababu nyingi za kujitoa kwenye huo muungano, zilizo wazi na zilizochificha lakini ni kikubwa ni hila za wenzetu:
1) Wanaonyesha haraka sana kutaka ku'fast-track' mambo na kikubwa ni kutaka kutuambukiza 'pressure' za matatizo yao ambayo hawataki kuyapatia ufumbuzi ndani ya mipaka yao!
2) Nchi mbili zimejikita kwenye u'dictator' na u'fashisti' wa kudumu ambao sio wa kuondoka leo wala kesho na mbili zina matatizo ya ukabila sugu ambao kabla haujaondoka utaambukiza ugonjwa mbaya nchi wanachama.
3) Nchi tatu wanachama wanaunda umoja wa wazi mno ndani ya jumuia na wanaonyesha mno uchu wa kuwa na 'UPPER HAND' kwa mambo ya kiuchumi na kisiasa na hapo, nafikiri, patakuwa eneo la migogoro kila siku.(tusisahau matatizo ya muungano wa Tanzania ambao tayari tunakumbana na matatizo kibao ambayo hatujayapatia ufumbuzi na sijui kama itakuwa leo au kesho.)
4)......... 5)................. HII LIST NI NDEFU MNO NA KILA MWANA JAMVI NAMUOMBA KWA UANGALIFU AJARIBU KUIJAZA KWA WAKATI WAKE MAANA HAPA TUNAANGALIA MUSTAKABALI WA NCHI YETU NA HATUWEZI WAACHIA WATU WACHACHE WALETE USHABIKI WA KISIASA NA KUKARIRI MANENO YA KINA NKURUMA NA KUTUINGIZA KWENYE
MAJANGA!
KUANZIA NA KIKAO KIJACHO CHA WAKUU WA NCHI TUNAMUOMBA SANA RAIS WETU ASIJITWISHE LAWAMA INGINE KWENYE AWAMU YAKE YA MWISHO KWA KUSAINI MIKATABA HATARISHI KWA TANZANIA KAMA MUUNGANO WA KISIASA NA SARAFU YA JUMUIA.
KENYA IS TOO CORRUPT TO HAVE MONETARY UNION WITH AND I HATE THE TWO DICTATORS IN A POLITICAL UNION! LET THIS 'JUMUIA' REMAIN AS LIGHT AS IT CAN BE FOR THE TIME FOR, TO ME, IT STINKS OF TROUBLE ('NDOA NDOANA' BULLSHIT!)
IT IS TIME WE CALL A SPADE A SPADE OR NEVER!

 
Hoja zako ni nzito na ni vigumu sana kutofautiana nazo lakini ni kisiasa zaidi na si kisayansi zaidi.
Kuna sababu nyingi za kujitoa kwenyehuo muungano, zilizo wazi na zilizochificha lakini ni kikubwa ni hila za wenzetu:
1) Wanaonyesha haraka sana kutaka ku'fast-track' mambo na kikubwa ni kutaka kutuambukiza 'pressure' za matatizo yao ambayo hawataki kuyapatia ufumbuzi ndani ya mipaka yao!
2) Nchi mbili zimejikita kwenye u'dictator' na u'fashisti' wa kudumu ambao sio wa kuondoka leo wala kesho na mbili zina matatizo ya ukabila sugu ambao kabla haujaondoka utaambukiza ugonjwa mbaya nchi wanachama.
3) Nchi tatu wanachama wanaunda umoja wa wazi mno ndani ya jumuia na wanaonyesha mno uchu wa kuwa na 'UPPER HAND' kwa mambo ya kiuchumi na kisiasa na hapo, nafikiri, patakuwa eneo la migogoro kila siku.(tusisahau matatizo ya muungano wa Tanzania ambao tayari tunakumbana na matatizo kibao ambayo hatujayapatia ufumbuzi na sijui kama itakuwa leo au kesho.)
4)......... 5)................. HII LIST NI NDEFU MNO NA KILA MWANA JAMVI NAMUOMBA KWA UANGALIFU AJARIBU KUIJAZA KWA WAKATI WAKE MAANA HAPA TUNAANGALIA MUSTAKABALI WA NCHI YETU NA HATUWEZI WAACHIA WATU WACHACHE WALETE USHABIKI WA KISIASA NA KUKARIRI MANENO YA KINA NKURUMA NA KUTUINGIZA KWENYE
MAJANGA!
KUANZIA NA KIKAO KIJACHO CHA WAKUU WA NCHI TUNAMUOMBA SANA RAIS WETU ASIJITWISHE LAWAMA INGINE KWENYE AWAMU YAKE YA MWISHO KA KUSAINI MIKATABA HATARISHI KWA TANZANIA KAMA MUUNGANO WA KISIASA NA SARAFU YA JUMUIA.
KENYA IS TOO CORRUPT TO HAVE MONETARY UNION WITH AND I HATE THE TWO DICTATORS IN A POLITICAL UNION! LET THIS 'JUMUIA' REMAIN AS LIGHT AS IT CAN BE FOR THE TIME FOR, TO ME, IT STINKS OF TROUBLE ('NDOA NDOANA' BULLSHIT!)
IT IS TIME WE CALL A SPADE A SPADE OR NEVER!


Kujiondoa kwa jazba hakutasaidia hasa unapotilia maanani kuwa viongozi waliopo, Uhuru, Kagame na M7, wataondoka na nchi zitabaki palepale. Muhimu kwetu ni kuwa wabunifu na kuchukua hatua ambazo na sisi zitatufanya tuweze kushindana vema zaidi kuliko kuchukia tu wenzetu wanapofanya mambo kwa maslahi yao.
 

Tatizo kubwa lililopo ni kwamba Wakenya wanataka kumilikishwa ardhi ya Tanzania, wamekuwa na hasira wanapoona tunakataa kuingiza sera hiyo katika makubaliano. Hakika SADC poa kabisa sisi tunafit kokote kule.

This is laughable and plain stupid. Go on and join SADC and see if you won't start complaining there too.
 
Kujiondoa kwa jazba hakutasaidia hasa unapotilia maanani kuwa viongozi waliopo, Uhuru, Kagame na M7, wataondoka na nchi zitabaki palepale. Muhimu kwetu ni kuwa wabunifu na kuchukua hatua ambazo na sisi zitatufanya tuweze kushindana vema zaidi kuliko kuchukia tu wenzetu wanapofanya mambo kwa maslahi yao.

Sio kujiondoa kwa jazba, la hasha, ila kuahirisha/au kujitoa kabisa kwenye mambo ya 'monetary and political union' na kubakia na uhusiano mwepesi kama tulionao kwenye jumuia ya SADC!
Narudia tena kuingia kwenye common currency na 'matapeli' wa Kenya ni hatari sana labda kama wakikubali benki kuu ya jumuia na full control ya sarafu yawe Tanzania. Ni wazi mno kwamba mtu atakaye 'control' coin ya jumuia ndiye atakayeyumbisha jumuia apendavyo kama matatizo yanayowakumba watumiaji wa euro (ambao ni mataifa ya ulimwengu wa kwanza!)
Kuhusu shirikisho la kisiasa ni wazi mno kwamba litawezekana kwa unafiki wa kisiasa tu kwani nafikiri mengi tunaya 'experience' hata sasa. Isitoshe nchi zetu haziko 'sychronized' kisiasa maana wenzetu wengine bado wamo kwenye mifumo ya kijima ya marais wa maisha!
 
mbona uingereza imejiunga na EU lakini ni kwa mambo kadhaa tu, si kwa kila kitu. mfano ni kwenye pesa yake ya pound starling na kwenye schengen visa. hata tz tunaweza kuendelea kuwa marafiki na kujiunga na wenzetu lakini kwa reservations kadhaa. kwamfano ardhi lisiwe jambo la wote. kama watasema kuwa kama hatutaki kushare ardhi basi sisi hatutakiwi basi hao watakuwa hawataki ushirikiano na sisi bali wanataka tu ardhi....
 
Back
Top Bottom