Twitter wafuta akaunti ya Rais Trump

lembu

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
16,375
21,834
Rais wa Marekani Donald Trump amefungiwa kabisa akaunti yake ya Twitter kwasababu ya hatari ya kuchochea vurugu zaidi", kampuni hiyo imesema.

Kampuni ya Twitter imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kufuatiliwa kwa karibu kwa ujumbe wa Twitter wa akaunti ya @realDonaldTrump account".

Baadhi ya wabunge na watu mashuhuri wamekuwa wakitoa wito kwa miaka mingi mtandao wa Twitter umpige marufuku Bwana Trump.

Aliyekuwa mke wa rais Michelle Obama aliandika ujumbe kwenye Twitter Alhamisi akisema kituo cha ubunifu wa teknolojia duniani Silicon Valley kinastahili kuzuia uendelezaji wa tabia mbaya za Bwana Trump na kumfuta kabisa kama mtumiaji wa huduma hizo.

Kwanini Trump alipigwa marufuku?
Bwana Trump alifungiwa akaunti yake ya Twitter kwa saa 12 Jumatano baada ya kutoa wito kwa wafuasi wake kuvamia bunge ambao aliwaita "wazalendo".

Mamia ya wafuasi wake walivamia bunge wakijaribu kuvuruga kikao cha kuidhinisha ushindi wa Bwana Biden kama rais. Vurugu hizo zilisabbaisha vifo vya raia wanne na afisa mmoja wa polisi.

Mtandao wa Twitter baadaye ukaonya kuwa unaweza kumpiga marufuku Bwana Trump kuutumia kabisa ikiwa atakiuka tena kanuni za jukwaa hilo la mawasiliano.

Baada ya akaunti yake ya Twitter kuwezeshwa tena, Bwana Trump alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Ijumaa kuwa kampuni hiyo ilikuwa na mwisho kuchochea.

Katika moja ya ujumbe wake aliandika: "Wamarekani 75,000,000 Wazalendo walionipigia kura, Marekani Kwanza na Fanya Marekani kuwa Bora Tena, watakuwa na sauti inayosikiza siku zijazo. Hawatakosewa heshima au kuchukuliwa kwa uonevu kwa namna yoyote ile !!!"

Mtandao wa Twitter umesema ujumbe huo "unatafsiriwa kama ishara zaidi ya kuwa Rais Trump hana mpango wa kuhakikisha kunafanyika 'mabadilishano ya mamlaka kwa njia ya amani'".

Katika ujumbe mwingine rais aliandika: "Kwa wote ambao wameuliza, sitahudhuria hafla ya kuapishwa Januari 20."

Mtandao wa Twitter umesema kuwa ujumbe huo "umechukuliwa na wafuasi wake kadhaa kama dhibitisho la kwamba uchaguzi huo haukuwa halali".

Mtandao wa Twitter umesema ujumbe wote huo alioandika "unakiuka sera na kanuni katika uhamasishaji wa vurugu".

Tazama jinsi waandamanaji walivyovamia bunge Marekani

Maelezo ya video,

Uchaguzi wa Marekani 2020: Tazama jinsi waandamanaji walivyovamia bunge Marekani

Trump amesema nini baada ya kufungiwa?

Baada ya akaunti yake ya @realDonaldTrump kufungwa kabisa, Trump alituma ujumbe kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani POTUS akisema kuwa "ataangalia uwezekano wa kuwa na mtandao wao utakaowezesha mawasiliano siku za usoni" na kukosoa Twitter.

Hata hivyo, ujumbe wake ulifutwa katika jukwaa hilo la mawasiliano muda mfupi baada ya kuwekwa.

Donald Trump's tweets from POTUS account, 8 January 2021

Akijibu baada ya kupigwa marufuku, mshauri wa kampeni ya Trump 2020 Jason Miller ameandika kwenye Twitter "Inachukiza... ikiwa hujafikiria kwamba wewe ndio wa pili watakaekufuata, umekosea."
 
Wangeita Democracy! Mwaka huu marekani imeumbuka. Thanks God hata mpumbavu wao Tundu Lissu chali
 
Uongozi wa Twitter umeifungia maisha akaunti ya Twitter ya Rais wa Marekani anayemaliza muda wake ndg. Donald Trump kwa kuhamasisha fujo na migomo katika jiji la Washington wiki iliyopita. Akaunti ya Donald Trump yenye jina la @realDonaldTrump (twitter.com) ndio akaunti ya sita duniani kuwa na followers wengi ikiwa inafuatiliwa na takriban watu milioni 90. Akaunti hiyo ukiitembelea sasa unakutana na neno "ACCOUNT SUSPENDED"

Tweets zilizopelekea Twitter kumfungia Trump ni hizi hapa

On January 8, 2021, President Donald J. Trump tweeted:

“The 75,000,000 great American Patriots who voted for me, AMERICA FIRST, and MAKE AMERICA GREAT AGAIN, will have a GIANT VOICE long into the future. They will not be disrespected or treated unfairly in any way, shape or form!!!”

Shortly thereafter, the President tweeted:

“To all of those who have asked, I will not be going to the Inauguration on January 20th.”

Source: blog.twitter.com

My Take

Je ingekuwa hizi tweets zingefanywa kwenye nchi hizi zetu za pembezoni Twitter wangefunga akaunti?
"Banned"

Wasema hovyo huishia kula ban tu, mbona hiyo inaeleka siku zote?

View attachment 1672858
 
Niliona uzi mmoja ivi ukimsifia kua yuko vizuri kidemokrasia na Ni mfano wa kuigwa sasa vipi Tena?🤣🤣🤣🤣
 
Elites wananeemeka na kundi hili kwenye video la wananchi.

Hao wakilinganishwa na wa huku kwetu ni middle class safi. Kungekuwa na room za dola 10-15 kwa mwezi kama huku kwetu wangeweza kuafford ila sasa utakuta huko apartment ni dollar 200 kwenda juu
 
Ipo na wameisema, yaani kutumia platform yao katika mazingira yanayohatarisha maisha ya wengine!
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi.

Sasa katika kuelewa malengo ya hawa twitter, mawazo haya yamenijia kichwani.

Sasa watu wakiwa kwenye hatari, waliopembeni au wao wenyewe wasipaze sauti ili wasaidiwe kutoka kwenye hatari hiyo? Aisee, Twitter ni "madictator in the disguise"! Inajulikana wazi kuwa Trump na wamarekani wenzake karibu 90% wako kwenye hatari ya demokrasia yao na haki ya kujieleza kupokwa! Halafu twitter wanafunguia wamarekani hawa wasiseme hatari hiyo...nini hii sasa!

Tukisema twitter na wenzake ni sehemu ya 1% ya wamarekani wanaofaidi kutokana na mateso ya karibu asilimia 90% ya wamarekani mnakuja juu!
 
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi.

Sasa katika kuelewa malengo ya hawa twitter, mawazo haya yamenijia kichwani.

Sasa watu wakiwa kwenye hatari, waliopembeni au wao wenyewe wasipaze sauti ili wasaidiwe kutoka kwenye hatari hiyo? Aisee, Twitter ni "madictator in the disguise"! Inajulikana wazi kuwa Trump na wamarekani wenzake karibu 90% wako kwenye hatari ya demokrasia yao na haki ya kujieleza kupokwa! Halafu twitter wanafunguia wamarekani hawa wasiseme hatari hiyo...nini hii sasa!!!

Tukisema twitter na wenzake ni sehemu ya 1% ya wamarekani wanaofaidi kutokana na mateso ya karibu asilimia 90% ya wamarekani mnakuja juu!
Ww badala ya ufikirie hali ya Tz inavyokuwa ngumu unajadili nchi zisizokuhusu eti madikteta Twitter. Inashangaza sana.
 
Back
Top Bottom