Twitter breaks its silence on possibly unconstitutional FBI data requests

Utawala wa Trump demokrasia na Katiba imewekwa pembeni kwanza. Tutaona mengi utawala wa huyu jamaa.

Mengi ya hayo tutakayoona, pia ni pamoja na kushindwa kwa fikra zake binafsi sana tu na kuwavunja na kuwakatisha tamaa wanaomshadadia....

Trump hawezi kupenyeza baadhi ya matamanio yake binafsi kama anavyofanya huyu wa hapa kwetu Tanzania.

Ni kwa sbb huko kuna very strong CHECK and BALANCE institutions ambazo haziwezi kuruhusu ujinga wa mtu mmoja uathiri taifa zima!!

Amini usiamini, baadhi ya Presidential executive orders zake zingine alizosaini zimeshapigwa stop tayari, haziwezi kutekelezwa mpaka kwanza wapime na kuona cons na pros!!
 
Mkuu with all due respect dhana ya usalama wa nchi ni kubwa na pana sana. Katika kumfuatilia mtu wakati fulani lazima watu wanafanya upelelezi wajue mpenzi wako ji nani, mnakutana wapi, mnatumia vyakula, au dawa gani na mnanunua wapi muda gani. Je una alama gani za mwilini ambazo zingine ni za faragha, wajue group la damu yako na mwenzio na nduguzo, ikilazimu DNA samples zako na watu wanaohusiana nawe. Una magonjwa gani ya kurithi, ya siri n.k. Huwezi kusanya hizi taarifa bila kuingilia haki ya faragha ya mtu. Lakini kwa sababu ya national security interests ni lazima haki hii iminywe kidogo. Wahalifu wengi wamekamatwa kwa kutumia vitu hivi, ambao wangekuja kuleta madhara makubwa kwa watu wengi labda mamia au maelefu kama pale WTC, Wall street Marekani, au Westgate na Garisa Kenya. Je huoni haki ya wengi kuishi au kutojeruhiwa au kupata ulemavu inazidi haki ya faragha ya few individual au many individuals? Maisha ya watu na faragha kipi kinatakiwa kipewe kipaumbele ktk mizania ya haki? Mambo haya ya kiupelelezi unaoingilia haki ya faragha ya mtu yamezuia matukio mengi mabaya kabla hayajatokea au kujirudia I am talking about preemtive measures using private informations of an individual person under the security radder(i.e.under investigation). Think Big. Kumbuka alivyopatikana Osama Bin Laden.


Umeanza vizuri ila umemaliza vibaya ...hayo Maswali yangu ungeyaelewa ungetambua kwamba kunatofauti kubwa sana ...tena sana ya ufafanuzi wako na uhalisia wa Usalama wa Nchi kama inavyotumika hapa nchini. Usalama hauhitaji kubeba dhana za kufikirika.Issue ya Osama nitofauti sana Kama mbingu na Ardhi hata sisi tulivuka kumsaka Idd Amin ...kule kwao uganda tukafanya tuliyo yafanya na nchi ikateleza haijarudi kwenye barabara hadi leo..... Ni meuliza Usalama wa Nchi(TAIFA) ni nini (Kiwango na Kipimo chake ni Kipi) na nani anapima na kuamua kwamba sasa hili ...linahusu usalama hatua fulani zichukuliwe....Je ni jambo gani linafanya au likifanyika tutaliona kama linatishia Usalama wa nchi....Kukosoa serikali inayo kuka Katiba....Kufanya Mikutano ya Kisiasa.... Kupinga Kauli za kibabe za watawala na vitisho kwa vyombo vya habari? kukosoa umangi meza na kiburi cha Utawala wa watawala?...Kile kilichofanywa na Marekani ni kinyume Kabisa cha sheria za Kimataifa achana na Haki za Binadamu.....Ukimya huu wa Pakistana ni kwasababu mkubwa akijamba amepumua.... Kimsingi lazima utofautishe na uchore mstari kati ya sencorship Uhuru wa Kupata habari...uhuru wa Maoni na Uhuru wa faragha za watu....HUWEZI KUWA NA USALAMA WA NCHI KAMA WANANCHI WENYEWE HAWAKO SALAMA.
 
Mababa na vilanja wa demokrasia duniani na wao wanaamini wanatakiwa waweze kupata taarifa za mtu yoyote wanayemshuku, ila sisi watz tunalilia uhuru usio na mipaka.
Hiyo haina shida hata kwetu tatizo hatuna watu wenye kifua wa kutunza siri katika kizazi hiki tofauti na miaka ya nyuma yaan mtu akikuambia ni askari au mwanausalama unamwamini na hata akiwa na taarifa za siri kuhusu wewe huwezi kuzisikia popote (kuanzia telephone operator, posta, na wanausalama wote walikuwa wanavifua). Lakini sasa hivi issue nyeti unaisikia live tu
 
ndiyo maan mitandao hii inayo ongozwa na watu wenye kuelewa maana ya haki ya faragha ya mtumiaji,uhuru wa maoni na haki ya kulindwa kwa Mtu dhidi vitendo haramu vya vyombo vya dola wanapinga Ujinga huu ambao kwetu eti inaitwa kwa usalama wa Taifa ...hivi unaomba mawasiliano ya jumla ya mtu kwa mukhtadha gani...Picha zangu labda za uchi na Utupu na maneno ya mapenzi na mpenzi wangu zinaweza kuwa na manufaa gani kwa usalama wa nchi ...hapa ndipo inapowekwa mipaka...na mipaka hii lazima itafsiriwe proferentum dhidi ya anayeomba taarifa za mtumiaji....Napongeza sana Kampuni hii ni tofauti na Kampuni ile ambayo imeridhia kubeba kwenye kikapu siri za Mteja wake ilikuzitolea ushahidi Mahakamani na nadhani jambo hili ni lakupongezwa kama ambavyo tunatakiwa kuipongeza Jamii forum hususana Mkurugenzi wake kwa kulinda na kusimamia Uhuru wa Maoni na fargha za watumiaji wake......
National security over everything, picha zako za utupu au privacy yako si chochote si lolote linapokuja suala la national security, fikiri kabla ya kuandika
 
Mengi ya hayo tutakayoona, pia ni pamoja na kushindwa kwa fikra zake binafsi sana tu na kuwavunja na kuwakatisha tamaa wanaomshadadia....

Trump hawezi kupenyeza baadhi ya matamanio yake binafsi kama anavyofanya huyu wa hapa kwetu Tanzania.

Ni kwa sbb huko kuna very strong CHECK and BALANCE institutions ambazo haziwezi kuruhusu ujinga wa mtu mmoja uathiri taifa zima!!

Amini usiamini, baadhi ya Presidential executive orders zake zingine alizosaini zimeshapigwa stop tayari, haziwezi kutekelezwa mpaka kwanza wapime na kuona cons na pros!!
Anatamani kuendesha Nchi kwa matamanio binafsi. Na Ile sera yake ya wagawe uwatawale.
 
Mababa na vilanja wa demokrasia duniani na wao wanaamini wanatakiwa waweze kupata taarifa za mtu yoyote wanayemshuku, ila sisi watz tunalilia uhuru usio na mipaka.

yes wanataka tuanze kuvurugana , ili baade waje watuuzie silaha na kuchukua resilimali zetu , lakini sisi tuko kama mazuzu , kushangilia tuu
 
Back
Top Bottom