Twitter breaks its silence on possibly unconstitutional FBI data requests

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Mtandao wa twitter kwa mara ya kwanza umeongelea kuhusu barua zilizotumwa kutoka Usalama wa Taifa (National Security Letters) zilizoambatana na amri ya ukimya (kutowajulisha wahusika wa akaunti wala jamii kwa ujumla) zinazohusu kuombwa taarifa za watumiaji wawili wa mtandao huo.

Akaunti za watumiaji hao zimesimamishwa lakini barua walizopokea kutoka serikalini zinataka taarifa za angalau miaka miwili ya kipindi mtumiaji mmoja alipokuwa akitumia mtandao huo, na kumbukumbu zote za matumizi ya mtandao za mtumiaji mwingine.

Mmoja wa viongozi wa mtandao huo amesema kuwa Twitter imewapa watumiaji hao kopi za barua hizo kutoka usalama wa taifa baada ya amri za ukimya (gag orders) kusitishwa lakini ingependa kutoa changamoto kwa serikali kuhusu mienendo yao hasa katika suala la uwazi.

Mbali na madai hayo ya kubana uwazi na uhuru wa kuongea, mawakili waliobobea katika faragha wanasema kuwa maombi ya taarifa hizo kutoka twitter ni kinyume na katiba. Pia wamesema makampuni hayo kuzuiwa kusema hadharani au kuwajulisha wahusika kuwa wamepokea barua za aina hiyo ni tatizo la muda mrefu.

========
- After the gag order lifted, Twitter questioned government practices that prevent Twitter from speaking more openly.

429f7fa4e001fc4c850257a475bace93.jpg

Twitter spoke out for the first time Friday regarding its federal case over large government data requests.

In a blog post, the company’s associate general counsel Elizabeth Banker wrote that the FBI lifted gag orders issued in 2015 and 2016 related to two national security letters that requested account data from two users.

The identity of the accounts in question are redacted but the letters request data for at least two years of account activity, such as email headers and browsing history, for one user and the entire account history, an unknown time period, of another.

Banker said Twitter has notified the users in question and provided them copies of the national security letters, but that it would like to challenge the government’s transparency practices.

We continue to believe that reporting in government-mandated bands does not provide meaningful transparency to the public or those using our service. However, the government argues that any numerical reporting more detailed than the bands in the USA Freedom Act would be classified and as such not protected by the First Amendment. They further argue that Twitter is not entitled to obtain information from the government about the processes followed in classifying a version Twitter’s 2013 Transparency Report or in classifying/declassifying decisions associated with the allowed bands. We would like a meaningful opportunity to challenge government restrictions when “classification” prevents speech on issues of public importance.

Beyond transparency claims, a Reuters report indicates the FBI’s data requests from Twitter may be unconstitutional, according to privacy advocates. The Electronic Frontier Foundation’s Andrew Crocker told Reuters that preventing tech companies from publicly disclosing some government data requests is an ongoing problem.

“This is an ongoing practice and it is significantly beyond the scope of what is intended,” he said. The EFF is representing some of the companies challenging the constitutionality of national security letters which usually come with gag orders.

U.S. government data requests outpace other countries and continue to climb, causing friction with tech companies. Following the 2013 NSA leaks, tech companies became increasingly vocal about the breadth and scope of law enforcement and intelligence agencies’ requests for consumer data, advocating for more transparency.

In its blog post, Twitter commended Google and Yahoo for speaking out recently about national security letters, emphasizing companies’ desire to protect consumers’ privacy and how the company fought for transparency.

We’re encouraged by the lifting of these two gag orders and those recently disclosed by Cloudflare, Google, the Internet Archive, and Yahoo!. However, Twitter remains unsatisfied with restrictions on our right to speak more freely about national security requests we may receive. We continue to push for the legal ability to speak more openly on this topic in our lawsuit against the U.S. government, Twitter v. Lynch.
 
Mababa na vilanja wa demokrasia duniani na wao wanaamini wanatakiwa waweze kupata taarifa za mtu yoyote wanayemshuku, ila sisi watz tunalilia uhuru usio na mipaka.
Mipaka wawekewe wote, anayeomba taarifa na anayeombwa. Si kila taarifa tu inayoombwa itolewe!
 
ndiyo maan mitandao hii inayo ongozwa na watu wenye kuelewa maana ya haki ya faragha ya mtumiaji,uhuru wa maoni na haki ya kulindwa kwa Mtu dhidi vitendo haramu vya vyombo vya dola wanapinga Ujinga huu ambao kwetu eti inaitwa kwa usalama wa Taifa ...hivi unaomba mawasiliano ya jumla ya mtu kwa mukhtadha gani...Picha zangu labda za uchi na Utupu na maneno ya mapenzi na mpenzi wangu zinaweza kuwa na manufaa gani kwa usalama wa nchi ...hapa ndipo inapowekwa mipaka...na mipaka hii lazima itafsiriwe proferentum dhidi ya anayeomba taarifa za mtumiaji....Napongeza sana Kampuni hii ni tofauti na Kampuni ile ambayo imeridhia kubeba kwenye kikapu siri za Mteja wake ilikuzitolea ushahidi Mahakamani na nadhani jambo hili ni lakupongezwa kama ambavyo tunatakiwa kuipongeza Jamii forum hususana Mkurugenzi wake kwa kulinda na kusimamia Uhuru wa Maoni na fargha za watumiaji wake......
 
Ni taarifa gani kwako ndio sahihi kuombwa na vyombo vya ulinzi, je unakubaliana na dhana ya lazima vyombo vya usalama viwe na uwezo wa kuomba hizi taarifa ?
 
ndiyo maan mitandao hii inayo ongozwa na watu wenye kuelewa maana ya haki ya faragha ya mtumiaji,uhuru wa maoni na haki ya kulindwa kwa Mtu dhidi vitendo haramu vya vyombo vya dola wanapinga Ujinga huu ambao kwetu eti inaitwa kwa usalama wa Taifa ...hivi unaomba mawasiliano ya jumla ya mtu kwa mukhtadha gani...Picha zangu labda za uchi na Utupu na maneno ya mapenzi na mpenzi wangu zinaweza kuwa na manufaa gani kwa usalama wa nchi ...hapa ndipo inapowekwa mipaka...na mipaka hii lazima itafsiriwe proferentum dhidi ya anayeomba taarifa za mtumiaji....Napongeza sana Kampuni hii ni tofauti na Kampuni ile ambayo imeridhia kubeba kwenye kikapu siri za Mteja wake ilikuzitolea ushahidi Mahakamani na nadhani jambo hili ni lakupongezwa kama ambavyo tunatakiwa kuipongeza Jamii forum hususana Mkurugenzi wake kwa kulinda na kusimamia Uhuru wa Maoni na fargha za watumiaji wake......
Siasa zinatengeneza wajinga wengi, usalama wa nchi ndio kipaumbele na sio picha zako za uchi, vyombo vya usalama lazima viwe na uwezo wa kupata taarifa za mtu yoyote wanayemshuku, mitandao mingi tu ya ujambazi nchini inakamatwa kwa sababu vyombo vya usalama vina access baadhi ya info, hata katochi kakipotea siku hizi unaweza rudishwa, msituletee sera za ajabu ili mradi tu zinafurahisha malengo yenu ya kisiasa.
 
Kama ni hivyo it is the other way round na Ujinga ni sifa ya Binadamu anaye penda kujifunza... ...unajipiga risasi mwenyewe....USALAMA WA NCHI MAANA YAKE NINI? NA USALAMA WA NCHI UNAANZIA WAPI NA KUISHIA WAPI? NA NANI ANAPIMA KIWANGO CHA USALAMA WA NCHI NA KUWEKA MPAKA WA HAKI YA FARAGHA YA MTU USIJIDANGANYE KWA KAULI ZA UJUMLA ZA USALAMA WA NCHI KAMA ZINAVYO TUMIKA HAPA NCHINI....hapa kwetu Usalama wanchi haujatenganishwa na usalama wa Viongozi wa chama Tawala ndiyo maana inatakiwa kuwepo kwa kipimo na definition iliyo bayana kwamba unaposema Usalama wa nchi una maana gani.Soma hoja in a wide sence na uelewe manytiki ya mfano wangu ...usikariri na kukaririshwa maneno hoja yangu nimeiuliza kitaalamu kuhusu mpaka na upana wa mpaka wewe unarukia na Taarabu ...Usinipe Majibu ya Jumla na ya hasira ...sina haja ya ugomvi ... nieleze Usalama wa nchi ni nini na ni wakati gani ambapo Usalama wa nchi unakuwa juu ya Haki ya faragha ya Mtu na niwakati Gani haki ya faragha inakuwa Juu ya Usalama wa Nchi ....Na nipe tofauti ya Usalama wa nchi kwa namna inavyo tumika hapa nchini kama huja jikanganya na usalama wa viongozi wa chama Tawala
 
Mipaka wawekewe wote, anayeomba taarifa na anayeombwa. Si kila taarifa tu inayoombwa itolewe!

It won't happen during our time on earth...serikali bado ni mbabe katika kila eneo. Mwisho wa siku hizo taarifa watazipata tu hakuna namna.
 
Kama ni hivyo it is the other way round na Ujinga ni sifa ya Binadamu anaye penda kujifunza... ...unajipiga risasi mwenyewe....USALAMA WA NCHI MAANA YAKE NINI? NA USALAMA WA NCHI UNAANZIA WAPI NA KUISHIA WAPI? NA NANI ANAPIMA KIWANGO CHA USALAMA WA NCHI NA KUWEKA MPAKA WA HAKI YA FARAGHA YA MTU USIJIDANGANYE KWA KAULI ZA UJUMLA ZA USALAMA WA NCHI KAMA ZINAVYO TUMIKA HAPA NCHINI....hapa kwetu Usalama wanchi haujatenganishwa na usalama wa Viongozi wa chama Tawala ndiyo maana inatakiwa kuwepo kwa kipimo na definition iliyo bayana kwamba unaposema Usalama wa nchi una maana gani.Soma hoja in a wide sence na uelewe manytiki ya mfano wangu ...usikariri na kukaririshwa maneno hoja yangu nimeiuliza kitaalamu kuhusu mpaka na upana wa mpaka wewe unarukia na Taarabu ...Usinipe Majibu ya Jumla na ya hasira ...sina haja ya ugomvi ... nieleze Usalama wa nchi ni nini na ni wakati gani ambapo Usalama wa nchi unakuwa juu ya Haki ya faragha ya Mtu na niwakati Gani haki ya faragha inakuwa Juu ya Usalama wa Nchi ....Na nipe tofauti ya Usalama wa nchi kwa namna inavyo tumika hapa nchini kama huja jikanganya na usalama wa viongozi wa chama Tawala
Ni muda wote usalama wa nchi unakuwa juu ya haki ya faragha ya mtu yoyote, kama hakuna usalama hata hiyo haki yako ya faragha hutaiona, mnaingiza siasa zenu za majitaka ktk mambo ambayo hayahitaji siasa, vipi wewe umeshafanikisha kuvunjwa kwa line ngapi za Voda ?
 
Mkuu unabsha na mtoto na hawez kujibu hayo maswali
 
Ni muda wote usalama wa nchi unakuwa juu ya haki ya faragha ya mtu yoyote, kama hakuna usalama hata hiyo haki yako ya faragha hutaiona, mnaingiza siasa zenu za majitaka ktk mambo ambayo hayahitaji siasa, vipi wewe umeshafanikisha kuvunjwa kwa line ngapi za Voda ?
Bado uko la nne b? Jaribu kuwa unapitiapitia sehemu tofauti ujue uhuru,haki kiundani
 
ndiyo maan mitandao hii inayo ongozwa na watu wenye kuelewa maana ya haki ya faragha ya mtumiaji,uhuru wa maoni na haki ya kulindwa kwa Mtu dhidi vitendo haramu vya vyombo vya dola wanapinga Ujinga huu ambao kwetu eti inaitwa kwa usalama wa Taifa ...hivi unaomba mawasiliano ya jumla ya mtu kwa mukhtadha gani...Picha zangu labda za uchi na Utupu na maneno ya mapenzi na mpenzi wangu zinaweza kuwa na manufaa gani kwa usalama wa nchi ...hapa ndipo inapowekwa mipaka...na mipaka hii lazima itafsiriwe proferentum dhidi ya anayeomba taarifa za mtumiaji....Napongeza sana Kampuni hii ni tofauti na Kampuni ile ambayo imeridhia kubeba kwenye kikapu siri za Mteja wake ilikuzitolea ushahidi Mahakamani na nadhani jambo hili ni lakupongezwa kama ambavyo tunatakiwa kuipongeza Jamii forum hususana Mkurugenzi wake kwa kulinda na kusimamia Uhuru wa Maoni na fargha za watumiaji wake......
Mkuu with all due respect dhana ya usalama wa nchi ni kubwa na pana sana. Katika kumfuatilia mtu wakati fulani lazima watu wanafanya upelelezi wajue mpenzi wako ji nani, mnakutana wapi, mnatumia vyakula, au dawa gani na mnanunua wapi muda gani. Je una alama gani za mwilini ambazo zingine ni za faragha, wajue group la damu yako na mwenzio na nduguzo, ikilazimu DNA samples zako na watu wanaohusiana nawe. Una magonjwa gani ya kurithi, ya siri n.k. Huwezi kusanya hizi taarifa bila kuingilia haki ya faragha ya mtu. Lakini kwa sababu ya national security interests ni lazima haki hii iminywe kidogo. Wahalifu wengi wamekamatwa kwa kutumia vitu hivi, ambao wangekuja kuleta madhara makubwa kwa watu wengi labda mamia au maelefu kama pale WTC, Wall street Marekani, au Westgate na Garisa Kenya. Je huoni haki ya wengi kuishi au kutojeruhiwa au kupata ulemavu inazidi haki ya faragha ya few individual au many individuals? Maisha ya watu na faragha kipi kinatakiwa kipewe kipaumbele ktk mizania ya haki? Mambo haya ya kiupelelezi unaoingilia haki ya faragha ya mtu yamezuia matukio mengi mabaya kabla hayajatokea au kujirudia I am talking about preemptive measures using private informations of an individual person under the security radder(i.e.under investigation). Think Big. Kumbuka alivyopatikana Osama Bin Laden.
 
ndiyo maan mitandao hii inayo ongozwa na watu wenye kuelewa maana ya haki ya faragha ya mtumiaji,uhuru wa maoni na haki ya kulindwa kwa Mtu dhidi vitendo haramu vya vyombo vya dola wanapinga Ujinga huu ambao kwetu eti inaitwa kwa usalama wa Taifa ...hivi unaomba mawasiliano ya jumla ya mtu kwa mukhtadha gani...Picha zangu labda za uchi na Utupu na maneno ya mapenzi na mpenzi wangu zinaweza kuwa na manufaa gani kwa usalama wa nchi ...hapa ndipo inapowekwa mipaka...na mipaka hii lazima itafsiriwe proferentum dhidi ya anayeomba taarifa za mtumiaji....Napongeza sana Kampuni hii ni tofauti na Kampuni ile ambayo imeridhia kubeba kwenye kikapu siri za Mteja wake ilikuzitolea ushahidi Mahakamani na nadhani jambo hili ni lakupongezwa kama ambavyo tunatakiwa kuipongeza Jamii forum hususana Mkurugenzi wake kwa kulinda na kusimamia Uhuru wa Maoni na fargha za watumiaji wake......
The issue in question here is how does the security institutes obtain the warrant to access someone's private information. Je wanahamua tu kulazimisha kupata hizo taarifa au wanapata kibali cha mahakama baada ya kuwa wamejieleza vya kutosha sababu na kuwaridhisha jopo la majaji, na Je ikiwa hivyo taarifa haitavuja na kuathiri mwenendo wa upelelezi? Na hapa ndio maana unaona tweeter waliwekewa zuio la kisheria kutomjulisha mteja wao anayechunguzwa. Unajua haya mambo ya usalama the few people know about it then the high chances of successiful investigation or mission execution. Kuna mambo mengine ukifanya politics tu basi hautafanya kwa ufanisi. Politicians wengi interest yao ni maslahi yao binafsi kwanza na yale mengine ya haki na bra bra zingine ni njia tu ya kujipatia mtaji wa kufanikisha malengo yake binafsi.
 
Huku kwetu wanao ikosoa serikali ndio hatari kwa nchi na ndio wanaotafutwa hii haikubaliki.

lakini kwa maana halisi ya usalama wa nchi mitandao inabid itoe ushirikiano kwa mfano kama kuna suspection ya uhalifu au ugaidi. na sio tu kwa sababu nimemsema vibaya kiongozi wangu au taasis fulani halaf mnanitafuta kwa kisingizio cha usalama wa nchi.
 
Utawala wa Trump demokrasia na Katiba imewekwa pembeni kwanza. Tutaona mengi utawala wa huyu jamaa.
 
Back
Top Bottom