Twin turbo zinafungukaje

Ni mahususi kwa diesel engine, petrol hutumia supercharger kama sikosei
Mzee teknolojia imebadilika. Kuna gari ya gasoline ni turbocharger, supercharger na plug-in hybrid pia. Gari hii ina 401HP, 0-60 in 5.3 seconds with top speed ya 140mph. Hii Volvo XC T8.
 
Kwa uelewa wangu mdogo, turbo inatokana na turbine engine, hizi ni teknolojia za kuunda engine ndogo yenye uwezo wa kuzalisha nguvu kubwa na kuongeza ufanisi (efficiency) wa matumizi ya mafuta. Hivyo ukiona gari inatoa moshi mwingi na gari hiyo ina engine yenye turbo, inamaana turbo hiyo haifanyi kazi sawa. Moshi mweusi ni matokeo ya mafuta ambayo hayajachomwa vizuri.

Turbo inafanya kazi kwa kutumia sensors. Sensors hizo husoma kinetic energy (velocity) ya moshi utokao katika exhaust pipe. Hivyo sensor zinaendana pia na RPM ya engine. Moshi unapofika katika level flani ya RPM, husababisha sensor kuruhusu turbines kuvuta hewa safi, iliyopozwa kuingia katika combustion chambers ili kuongeza mafuta yanayoendana na kiasi cha hewa na kuyaunguza, ili kutoa energy output inayohitajika na engine. At the same time, hewa iliyokwisha unguzwa hutolewa kupitia chamber nyingine nana kutolewa nje kupitia exhaust pipe. Kwa gari zenye intercooler, hewani safi hupitia kwenye intercooler kupoozwa zaidi, ili volume kuwa kubwa na kuongeza ufanisi zaidi katika kuchomwa kwake ktk engine.

Sasa twin turbo inamaana kuna turbo ya lower end and higher end RPM. Lower end, turbo imesetiwa kwa gear namba mbili, moja na unapokuwa katika 4wd. Higher end turbo sensor yake imesetiwa kwa gear namba 4, 5, na 6 kwa gari za kisasa, zenye uwezo wa kutoa output kubwa (Higher torque).
 
Kwa uelewa wangu mdogo, turbo inatokana na turbine engine, hizi ni teknolojia za kuunda engine ndogo yenye uwezo wa kuzalisha nguvu kubwa na kuongeza ufanisi (efficiency) wa matumizi ya mafuta. Hivyo ukiona gari inatoa moshi mwingi na gari hiyo ina engine yenye turbo, inamaana turbo hiyo haifanyi kazi sawa. Moshi mweusi ni matokeo ya mafuta ambayo hayajachomwa vizuri...

Also, you have to set a reference pressure level, which mostly is based on intake manifold pressure. Kwenye gari yangu, turbo nimeiseti ku build pressure mpaka 22psi.

Baada ya hapo pressure ina kuwa released through the waste gate (kimlango kidogo ambacho kiko kwenye exhaust side ya turbo na kinafunguliwa na "waste gate actuator"). Hii part ni muhimu ili kuhakikisha una control pressure buildup. Otherwise utafumua cylinder head gasket😄
 
Kwahiyo hapo kuna parts kama waste-gate actuator na boost controller ambazo ni umuhimu katika kucontrol ujazo wa hewa kwenye engine. Waste-gate inapokea pressure signal from boost controller, ambayo ndio inasetiwa kuiambia waste gate iistopishe turbo at a particular pressure of your choosing. Kwa mfano, mimi nimeseti turbo controller yangu to signal the waste-gate when intake manifold pressure reaches 22 psi.
 
Nyongeza, sorry kama ni nje ya maada...
Ukichange turbo ili upate power zaidi, basi jua inabidi ubadilishe mlolongo mrefu wa parts nyingine ambavyo vinatakiwa kusupport turbo kubwa. Hii inahitaji uwe na roho ngumu 😄...

Kwa mfano, Lazima ubadilishe:
Exahust system
Fuel Injectors
Fuel pump
Engine computer modification
Clutch plate and Pressure plate
Bigger intercooler
All turbo pipes
Manual/electronic boot controller

Na kadhalika...
 
Mkuu kuna point umeikosa kidogo hapo. Msemo wa turbo kufunguka unamaanisha pale turbo inapoanza kuleta hewa zaidi kwenye engine. Unapowasha engine kama RPM ni kidogo, turbo japo inazunguka ila inaongeza nguvu kidogo saana (insignificant) kwenye engine.

Ila kwenye RPM kubwa, hewa inayotoka kwenye exhaust inakuwa nyingi pia so inaweza kuzungusha turbines za turbo kwa kasi zaidi na hivyo kuongeza hewa safi na nguvu zaidi kwenye engine.

Kueleza kirahisi hii concept, gari huwa linatoa moshi zaidi pindi "ukipiga resi" kuliko likiwa silence. So unapopiga resi inamaana rpm inapanda na hewa chafu inatoka kwa wingi hivyo turbines za turbo zinazunguka kwa nguvu zaidi pia na kusababisha hewa nyingi kuingia kwenye engine. Hapo ndio tunasema turbo imefunguka.
upo sawa kabisa skupingi kwa sababu kazi ya turbo ni kuongeza hewa kwa wingi kwenye cylinder na turbo inafanya kazi vizuri rpm ikiwa juu ndo tunasema turbo imefungua
 
Nyongeza, sorry kama ni nje ya maada...
Ukichange turbo ili upate power zaidi, basi jua inabidi ubadilishe mlolongo mrefu wa parts nyingine ambavyo vinatakiwa kusupport turbo kubwa. Hii inahitaji uwe na roho ngumu 😄...

Kwa mfano, Lazima ubadilishe:
Exahust system
Fuel Injectors
Fuel pump
Engine computer modification
Clutch plate and Pressure plate
Bigger intercooler
All turbo pipes
Manual/electronic boot controller

Na kadhalika...
Ubadili hata kama hizo parts hazina defects zozote?
 
Ningependa kuchangia uzoefu wangu…

Twin turbo ina tumika kwa sababu ya Kupunguza turbo lag. Turbo lag ni kule kuchelewa kufunguka kwa turbo wakati gari ina panda kasi. Ukitaka gari iwe na nguvu unaweka turbo. Ukiweka turbo kubwa basi na power inaongezeka zaidi. Tatizo ni kwamba turbo kubwa ina chelewa kufunguka. Inachelewa kwasababu inahitaji kujenga pressure kubwa ya exhaust ili izungushwe kwa haraka.

Ingini ya gari ujenga pressure zaidi katika RPM ya juu. Na gari hua inachukua mda kufika RPM ya juu. Kuchelewa huku ndiko kuna sababisha kuchelewa kwa turbo kufunguka ili ianze kuiongezea power ingini. Ingini ikifika RPM ya kuifungua turbo, basi power inakuja kwa ghafla..booom. Power inaingia kwa nguvu na kwa ghafla, unaona kama vile "you suddenly being pulled on the chair", yaani kama vile tumbo linakatika hivi :)

Sasa tatizo ni kwamba, wateja wengi wa sports car hua hawapendi hiyo feeling ya “kukatika tumbo”. Kwahiyo basi, watengeneza magari wanaweka turbo ya pili ambayo ni ndogo na inafunguka mapema katika RPM ya chini. Kwasababu turbo ndogo haina power kama kubwa, basi mfunguko wake sio wa ghafla sana. Hii turbo ndogo ikifunguka mapema itaendelea kufunguka mpaka pale RPM ya ingini imepanda kiasi cha kutosha kufungua turbo ya pili ambayo ni kubwa. Turbo kubwa inafunguka na kumpokea mwenzake na kuendelea kujenga power zaidi. Matokeo yake ni kwamba dereva ana sikia "mfunguko nyororo" (smooth spooling).

Kwa ufupi basi, turbo mbili zinawekwa ili kuunda a "turbo system" ambayo inafanya mfunguko wa turbo usiwe wa ghafla. Tena basi, ni lazima zichaguliwe turbo ambazo zina endana ili kufanya mfunguko wa kushirikiana ulio nyororo yaani smooth. Moja kuwa moja ndogo.

Katika hobby hii, mimi nimeshabadili turbo kama nne katika gari yangu. Kwa wale mnao zijua turbo, mimi nilianza na T25, nika weka 16G, B16G, mpaka 20G. Nina spare ya FP20GRED ambayo nitaiweka pale nitakapoichoka 20G niliyonayo hivi sasa. Natumaini nimeweka mchango mzuri.


Asanteni na msisahau kutambika au angalao kuwashukuru mababu na mabibi zetu.
Bro...unajua hadi unakera aseesafii
 
Ubadili hata kama hizo parts hazina defects zozote?
Ndio, lazima ubadili ili kufikia power unayo itaka. Kitu kikubwa ambacho engine computer inafanya ni kumechisha air na petroli ili zikiingia kwenye engine ziilipuke vizuri kikemia (correct air/fuel ratio). Sasa ili kupata the right air/fuel ratio lazima injector zimachi na turbo. Ukiweka turbo kubwa basi injector nazo lazima ziwe kubwa. Lakini injector kubwa nazo zinahitaji fuel pump kubwa. Fuel pump kubwa nayo inahitaji umeme wa kutosha kwahiyo lazima ubadilishe wiring syste ili umeme uwe wa uhakika kwenye pump kubwa.

Pump kubwa nayo inahitaji fuel regulator mpya, maana original iliyokuja na gari haito himili pressure ya pump kubwa. Kwahiyo lazima uweke fuel pressure regulator ambayo unaweza adjust mwenyewe (mimi natumia ya kampuni na Fuel-Labs).

Hapo bado hujagusa mahitaji ya kupooza engine (bigher radiator, bigger intercooler, na hata water injection). Pia transmission lazima uiimarishe ili iweze kuhimili power/torque....

.... kwahiyo mlolongo wa kubadilisha parts unakua mrefu sana🤣🤣🤣🤣
 
Ndio, lazima ubadili ili kufikia power unayo itaka. Kitu kikubwa ambacho engine computer inafanya ni kumechisha air na petroli ili zikiingia kwenye engine ziilipuke vizuri kikemia (correct air/fuel ratio). Sasa ili kupata the right air/fuel ratio lazima injector zimachi na turbo. Ukiweka turbo kubwa basi injector nazo lazima ziwe kubwa. Lakini injector kubwa nazo zinahitaji fuel pump kubwa. Fuel pump kubwa nayo inahitaji umeme wa kutosha kwahiyo lazima ubadilishe wiring syste ili umeme uwe wa uhakika kwenye pump kubwa.

Pump kubwa nayo inahitaji fuel regulator mpya, maana original iliyokuja na gari haito himili pressure ya pump kubwa. Kwahiyo lazima uweke fuel pressure regulator ambayo unaweza adjust mwenyewe (mimi natumia ya kampuni na Fuel-Labs).

Hapo bado hujagusa mahitaji ya kupooza engine (bigher radiator, bigger intercooler, na hata water injection). Pia transmission lazima uiimarishe ili iweze kuhimili power/torque....

.... kwahiyo mlolongo wa kubadilisha parts unakua mrefu sana🤣🤣🤣🤣
Nimekuelewa chief. Ila swali langu lililenga kuelewa hoja ya kubadili hizo parts zingine endapo nimeweka turbocharger mpya yenye specs zilezile kama za turbocharger iliyopata defects.
 
Nimekuelewa chief. Ila swali langu lililenga kuelewa hoja ya kubadili hizo parts zingine endapo nimeweka turbocharger mpya yenye specs zilezile kama za turbocharger iliyopata defects.
Sorry,...hapana. nipale tuu unapoongeza turbo. Nahata hivyo una badilisha pole pole, kimoja kimoja pale unapoona kifaa kimeishiwa nguvu au hakihimili nguvu mpya ya gari. Ila mwisho wasiku inakubidi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom