Launch Control (LC) na umuhimu wake (Automotive Engineering)

charldzosias

JF-Expert Member
Nov 10, 2013
2,448
3,334
Habari zenu wakuu,

Kuna kitu ningependa tupeane elimu kwa kiasi chake. Pale nitakapokosea msisite kunielekeza maana mimi pia najifunza hapa kwa wanajamvi na ma injinia mliotukuka humu JF.

Launch control system hii husaidia gari ikamate ardhi,inasambaza uzito uwiane katika gari,inasaidia gari itulie barabarani pale unapokanyaga Throttle pedal to rev up, ili upate maximum boost ya kuondoka bila ya kupata vikwazo kama wheel spin na mambo mengine mengi.

Kuna baadhi ya gari huja ikiwa na hii set up ila nyingi huwa ni second hand inputed device.

Mechanism ya ufanyaji kazi wake upo kama ifuatavyo:

Ukisha ENGAGE LC mode, moja kwa moja driver anakanyaga brake pedal kabla ya kukanyaga pedal ya mafuta yaani Throttle pedal.

Hapa huwa kuna mambo mengi yanaendelea kwa wakat mmoja jambo la kwanza gari itapiga rev na kuna device inayohesabu rev ratings. so kuyaforce yapate TRACTION. Pindi ukiachia breki basi gari itaondoka kama Risasi, bila ya kuyumbayumba au kuteleza.

Kuna kitu kinaitwa ECU. Kwa kila gari ipo na ni kama ubongo wa gari. Hichi kifaa kina control engine kiujumla na hichi kifaa huwa kinapitishwa kwa ma ENGINEER kupewa access mbalimbali. Mfano Mapping na mambo mengine yahusuyo na LC pia.

Tukija kwa upande wa ECU (Electrical Control Unit) au kwa jina lingine ni Control box, ambayo kupitia setting za LC hichi kifaa huwa kinaprogramiwa na mtaalamu, so pindi driver akiachilia brake tu moja kwa moja inakuwa kama ni trigger inayopeleka taarifa kwa ECU kuwa huu ndio muda muafaka wa kudepreese clutch. Hivyo gearbox inatenganishwa, na gears zinaingia hivyo gari inaondoka.

Hili zoezi halihatarishi Engine yako kutokana na kuwa na kifaa ambacho kinaenda sambamba na LC kifaa hicho kinafahamika kama REV CUT/REV LIMITER ambayo kazi yake ni ku monitor mizunguko ya crankshaft isiwe mingi kupelekea kuharibu engine, so ukiwa una Rev engine hii rev-cut ina balance usifike redline za RPMS 'ROUNDS PER MINUTES'. Hii mechanism huwa ishapigiwa mahesabu na mtaalam aliyeprogram ECU.

Zoezi hili hupelekea gari kutoka 0 - 60kph ndani ya sekunde 2.5 tu!

Tukija katika upande wa gearbox hapa kuna ishu ya dual-clutch system, ambayo huwa kuna clutch mbili ndani ya gearbox shell.

Hali hii hupelekea vitu vingi kwenda sawa na kutoleta matatizo pindi clutch moja ikiwa depressed bas pia inapokelewa na clutch nyingine, jambo linalopunguza joto (heat) katika engine pia inapunguza uwezekano wa ku damaje gearbox pindi ukiwa na single clutch system.

Pia twin clutch system hupelekea kuingia na kuvuliwa gear kwa haraka zaidi bila ya mishtuko ya hard shifting inayopelekea matatizo katika drivetrain.

Tukija upande wa TURBOCHARGERS wakat driver aki engage LC option, na kuanza ku launch, turbo pia huwa activated na kuanza kuzunguka kwa kasi zaidi hali inayopelekea kupata maximum boost pale utakapoachia brake pad, haya mambo yote yanakuwa programmed katika ECU programming maneuvers.

Hitimisho: Hii option ina faida nyingi

- Kutomaliza matairi
- Kutohalibu mfumo wa clutch
- Kutoua gearbox
- Matumizi mazuri ya mafuta
- Kupata speed nzuri
- Pia haipo stressed
- Inazuia ajali zile za front wheel spin up

Mwenye nyongeza aongezee. Tuendelee kujifunza, zaidi shukrani. Mtanisamehe kwa uandishi wangu usiovutia.
 
Mkuu, umeeleza kwa undani saana hiyo kitu. Ila ungeweka na mifano ya baadhi ya gari zenye huo mfumo. Maana kuna watu hatuchelewi kujaribu kukanyaga Impreza zetu mpaka tuone hiyo 0 - 60 ya 2.5 secs.
 
oh.. Nimekuelewa ndugu.. Nilitaka niweke video pia ila ntafanya hvyo..
Kuhusu aina ya gari.. Zipo gari chache sana zenye hii option ikiwa installed direct kutoka kiwandani.. Mfano ni recent high perfmance sport cars. Imprezza pia unaweza ku install as second hand device bila wasiwasi... Then kuna imprezza ambazo ni Triptonic 'MANUMATIC' huwa tamu sana..
 
Ooh! Kumbe inaweza kuwa installed. Mie nilijua ni feature ya gari za kisasa tu. As nimeiona kwenye highend sport na supercars. Na Kibongobongo zinapatikana?
 
Ooh! Kumbe inaweza kuwa installed. Mie nilijua ni feature ya gari za kisasa tu. As nimeiona kwenye highend sport na supercars. Na Kibongobongo zinapatikana?

zipo ingawa tunaagiza nje.. If uktak kuweka hii ki2 nakushaur atleast uwe na wastan ya nguvu ya farasi 280 katika bonet yako i mean above 280hp..

Coz aim ni ku2lia ktk road na ku resist too much power itakayokutoa nje.. Sasa ukiw maybe na 160hp kuna haja ya Lc? So maybe ufanye Tune up ya injin yako ukiwa na hp kubwa sasa unakuja kumaliza na Lc..

Kuna ku-map gari
kuna ku-tune injin specs
kuna kuforce boost bars ufike hata 2.5 bars usumbue mji
kuna kufunga madude kama Rev -cut..
Kuna kuweka system ya kuondoa lags ktk turbo.. Na kama turbo hauna ununue.. Yaan zoez la kwanza ni dhumuni ya kuweka Lc.. Dhumun linaambatana na uwezo wa gari na matumiz yake kiujumla.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom